Tuesday, November 13, 2012 


MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amependekeza kuvunjwa kwa Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwani badala yake kupambananayo inaipalilia.

Akifungua tawi ya Chadema Kata za Katesh linalopakana na ofisi za Takukuru Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara juzi, Mbowe alisema taasisi hiyo imeshindwa kazi.

Mbowe alisema Takukuru imeshindwa kudhibiti hata rushwa ya wazi ndani ya CCM kwenye chaguzi ambazo zilifanyika hivi karibuni.

“Hakuna ambaye hakujua rushwa ndani na CCM na jinsi ambavyo imeathiri chama hicho, lakini Takukuru wameshindwa kupambana na rushwa hiyo badala yake wanailea,” alisema Mbowe.

Alisema Rais Jakaya Kikwete ambaye anasimamia Takukuru iliyopo kwenye wizara yake, ameshindwa kuibana ndiyo sababu hata yeye amekuwa akilalamika.

Pia, Mbowe alifungua matawi kata za Endasaki na Ganana, alisema kutokana na Takukuru kushindwa kupambana na rushwa, isipovunjwa chama hicho kikiingia madarakani kitawatimua watendaji wote wa taasisi hiyo ili wafanye kazi nyingine.

Alisema Takukuru imeshindwa hata kusaidia kurejesha mabilioni ya fedha za Watanzania ambayo yamefishwa nchini Uswis.

“Hawa Takukuru walipaswa kuanza kufanya uchunguzi juu ya fedha hizo baada ya kupata taarifa na kusaidia taifa kuzipata, lakini wamekaa kimya,” alisema Mbowe.

Alisema kutokana na ukimya huo, ndiyo sababu Chadema kupitia Naibu Katibu Mkuu wake, Kabwe Zitto waliomba serikali kufanya uchunguzi na kutoa taarifa bungeni juu ya walioficha fedha na utaratibu wa kuzirejesha.

“Bunge lijalo, kama wasipoleta taarifa ya maana juu ya fedha za Uswis tunajua la kufanya, nadhani mmeona jinsi hoja hii ilivyoungwa mkono na watu wengi,”alisema Mbowe.

Awali, Mbowe alizitaka ofisi hizo za Chadema, alizofungua kuwa kimbilio la wanyonge kutoa kero zao na kusaidiwa badala ya kuwa maeneo ya kukaa viongozi pekee

RIPOTI KAMILI YA UCHSGUZI WA CCM DODOMA HII HAPAMwenyekiti
Kura zilizopigwa             2397
Kura zilizoharibika           0
Kura za HALli 2397

Makamu wa Tanzania Bara
Kura zilizopigwa             2397
Kura zilizoharibika           0
Kura za HALli                 2397

Malamu wa Zanzibar
Kura zilizopigwa             2397
Kura zilizoharibika           0
Kura za HALli 2397
WAKATI matokeo ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya  CCM (Nec), yakiwa yamevuja baadhi ya wapambe wa wagombea walioshinda  wameanza kusherehekea, huku wengine wakitambiana.

Hata hivyo, matokeo hayo yamekuwa machungu kwa baadhi ya vigogo walioanguka wakiwamo mawaziri, wabunge na watu maarufu.

Mwenyekiti  wa CCM, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuunda sekretarieti mpya baada  ya uchaguzi wa mwenyekiti na makamu mwenyekiti Bara na Zanzibar  utakaofanyika leo.

Kwa upande wa Zanzibar,

Kura zilizopigwa             2268
Kura zilizoharibika           55
Kura za HALli                 2213
matokeo hayo  yanaonyesha kuwa walioshinda ni pamoja na Mbunge wa Uzini, Mohamed Seif  Khatib; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Ali Mwinyi 1576, Waziri  wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee, Abdulhakim Chasama na  Waziri wa  Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha 1603.

Wengine   ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan 1525, Khadija  Hassan Aboud 1625, Bhaguanji Mansuria, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na  Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa  1850 na Khamis Mbeto.


Watu maarufu  walioangukia pua katika uchaguzi huo ni Naibu Waziri wa Ushirikiano wa  Afrika Mashariki, Dk Abdallah Juma Sadallah, mtoto wa Rais Mstaafu,  Abdallah Mwinyi ambaye pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Mbunge wa Viti  Maalumu, Kidawa Salehe na Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Abdisalaam  Issa Khatib.

Walioshinda Bara

Kura Zilizopigwa    2389
Kura Zilizoharibika  52
Kura halali            2337

Majina ya wajumbe wa Nec  walioshinda bara na kura walizopata katika mabano ni Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira aliyeongoza kundi  hilo kwa kupata kura 2,135, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na  Teknolojia, January Makamba (2,093), Mwekahazina wa CCM, Mwigulu Nchemba  (2,012), na Katibu wa UVCCM, Martine Shigela (1,824).

Wengine ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William  Lukuvi (1,805), Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard  Membe (1,455), Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David  Mathayo (1,414), Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome (1,207), Katibu  Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (1,174) pamoja na Waziri wa Habari,  Utamaduni, Vijana  na Michezo, Fenela Mukangara (984).

Wakati  walioshinda Bara na wapambe wao wakitambiana, majina makubwa  yaliyoanguka katika uchaguzi huo ni pamoja ni Mbunge wa Afrika  Mashariki, Shy-Rose Bhanji, Mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama, Richard  Hiza Tambwe na Mbunge wa zamani wa Muleba Kaskazini, Ruth Msafiri.

Wednesday, November 7, 2012

RATIBA YA MICHEZO YA JUMAMOSI lig kuu england

RATIBA YA MICHEZO YA JUMAMOSI NOV 10 YA LIGI YA ENGLAND
Everton v Sunderland Goodison Park 17:00
Southampton v Swansea St. Mary's Stadium 17:00
Stoke v QPR Britannia Stadium 17:00
Reading v Norwich Madejski Stadium 17:00

Wigan v West Brom The DW Stadium 17:00
Arsenal v Fulham Emirates Stadium 17:00
Aston Villa v Man Utd Villa Park 19:30