Thursday, April 18, 2013

KAMA HUJASAJILI SIMU SASA HAKUNA HUDUMA




[caption id="attachment_942" align="aligncenter" width="477"]MKIURUGENZI MKUU WA TCRA PROFESA JOHN NKOMA AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO MKIURUGENZI MKUU WA TCRA PROFESA JOHN NKOMA AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO[/caption]

HABARI NA EXAUD MTEI

Watumiaji wa mitandao ya simu na watanzania kwa ujumla wametakiwa kuhakikisha wanasajili laini zao kabla ya kuzitumia kama serikali ilivyoagiza kwani kutokufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria na adhabu yake ni kubwa.

         Hayo yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa mammlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA profesa JOHN NKOMA wakati akizungumza katika mkutano na wamiliki wa mitandao ya simu na wanahabari leo jijini dare s salaam kuhusu maendeleo ya mchakato wa kusajili simu za mikononi kwa watumiaji

          Profesa NKOMA amesema mamlaka imebaini kuwa bado kuna watanzania wanaomiliki laini za simu ambazo hazijasajiliwa jambo ambalo amesema ni kinyume na sheria za nchi na adhabu zake ni kubwa ikiwemo faini ya hadi laki tano au kifungo.

           Hata hivyo prof NKOMA amewaagiza wamiliki wa mitandao ya simu Tanzania kuhakikisha wanaendelea na zoezi hilo la kusajili laini za simu huku akisema kuanzia sasa mtumiaji wa simu hatoweza kupata huduma yoyote ya simu kama atakuwa hajasajili simu yake katika mtandao husika.

        Aidha amewaomba watanzania kuunga mkono sera hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi wakati a kufanya usajili hukuakisema kufanya hivyo ni kwa faida ya mtumiaji pekee



 

 

No comments: