Monday, April 15, 2013

SAKATA LA KUTEKWA KWA VIONGOZI SASA LAHAMIA JUKWAA LA KATIBA,HOFU YATANDA KWAO,WAOMBA MSAADA KWA VYOMBO VYA USALAMA

[caption id="attachment_870" align="aligncenter" width="477"]BW RUTAGEBDA WA JUKWAA LA KATIBA AKIELEZEA JINSI VIONGOZI WAKE WALIVYOTAKA KUTEKWA NA WATU AMBAO HAWAKUJUA WALIKUWA WANATAKA NINI BW RUTAGEBDA WA JUKWAA LA KATIBA AKIELEZEA JINSI VIONGOZI WAKE WALIVYOTAKA KUTEKWA NA WATU AMBAO HAWAKUJUA WALIKUWA WANATAKA NINI[/caption]

SAM_6785 SAM_6787

picha ya pili ni waandishi wa habari waliokuwa wanasikiliza sakata hilo leo na chini ni wadau wa jukwaa la katiba wakisikiliza kwa makini sakata hilo

HABARI NA EXAUD MTEI

Sakata la kutekwa na kutesa kwa watu mbalimbali sasa limehamia jukwaa la katiba . Jukwaa la katiba Tanzania limeviomba vyombo vya usalama ikiwemo polisi na vyombo vingine kuhakikisha vinalinda usalama wa viongozi wa jukwaa hilo kutokana na kile walichokidai ni kutishiwa maisha kwa viongozi wa jukwaa hilo mnamo ijumaa ya wiki iliyopita.

           Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam leo mjumbe wa kamati ya utendaji wa jukwaa hilo bw HEBRON MWAKAGENDA amesema mnamo tarehe 12 ya mwezi nne mwaka huu ofisini kwao kulikuja gari yenye namba T126 CCG yenye watu sita waliokuwa wakiwataka viongozi wa jukwaa hilo waondoke nao bila kujitambulisha majina yao na wanakotoka, jambo ambalo amesema walinzi walifanikiwa kuwazuia huku akisema kitendo hicho kimewapa wasiwasi na kuomba ulinzi kutoka vyombo vya usaklama

            Bw mwakagenda kuwa ameongeza kuwa baada ya tukio hilo kutokea jukwaa limetoa taarifa kwa vyombo mbalimbali vya usalama ikiwemo kituo cha polisi mabatini,ofisi ya kamanda wa polisi kinondoni,na pia kumtaarifu ispecta jenerali wa polisi IGP SAID MWEMA.huku akisema jukwaa halitaogopa kufanya kazi yake kutokana na tishio hilo.

           Aidha pamoja na hatua hizo walizochukua mjumbe huyo amewawaomba wasamaria wema kutoa taarifa kwao au jeshi la polisi wanapopata taarifa zozote za njama dhidi ya viongozi wa jukwaa au viongozi wengine ili waweze kufanya kazi zao kwa uhuru

 

 

No comments: