.

CAF CHAMPIONZ LIGI: DROO YA MAKUNDI YAFANYIKA! CHEKI MAKUNDI YALIVYOKAA HAPA

CAF_DROO


LEO huko Jijini Cairo, Misri, imefanyika Droo ya hatua ya Makundi ya Mashindano ya CAF ya CHAMPIONZ LIGI na

Mabingwa Watetezi Al Ahly wataanza utetezi wa Taji lao kwa kucheza Ugenini na wenzao Mahasimu wao wakubwa wa huko Misri Zamalek ambao wamepangwa pamoja kwenye Kundi A.

Hii ni mara ya pili kwa Miaka miwili mfululizo kwa Miamba hiyo ya Misri kupangwa Kundi moja kwenye michuano hii na safari hii wako pamoja na Orlando Pirates ya South Africa na Timu mpya kwenye Mashindano haya AC Leopards ya Congo ambayo Mwaka jana ilitwaa Kombe la Shirikisho.

Kundi B lina Timu za Esperance ya Tunisia, ambayo ndio ilitolewa Fainali na Al Ahly kwenye michuano hii Mwaka jana, na nyingine ni Coton Sport ya Cameroon, Sewe Sport ya Ivory Coast na Recreativo de Libolo of Angola, ambao ndio waliwatupa nje ya michuano hii waliokuwa Mabingwa wa Tanzania, Simba Sports Club.

Mechi za Makundi zitachezwa kwa Mtindo wa Ligi wa Nyumbani na Ugenini na Washindi wawili wa juu wa kila Kundi watasonga Nusu Fainali.

Mechi za Makundi zitachezwa kuanzia Julai hadi Septemba huku Nusu Fainali ikitarajiwa kuwa Oktoba.

DROO:

KUNDI A

Al Ahly (Egypt)

AC Leopards (Congo)

Orlando Pirates (South Africa)

Zamalek (Egypt)

KUNDI B

Esperance (Tunisia)

Coton Sport (Cameroon)

Recreativo de Libolo (Angola)

Sewe Sport (Ivory Coast)

 

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.