Friday, May 17, 2013

HUZUNI--- MWANAUME MMOJA AMEANGUKA GHAFLA AKIWA ANATEMBEA NA KUFARIKI HAPO HAPO MAENEO YA POSTA SAMORA JIONI HII

BAADHI YA WASAMARIA WEMA WAKISAIDIA KUTOA MSAADA YA KUNYANYUA MWILII HUO KWA AJILI YA KUPELEKWA MAHALI HUSIKA
POLISI WALIOFIKA WAKISAIDIANA NA WANANCHI KUHIFADHI MWILI WA MTU HUYO
 Mwanaume  mmoja ambaye hakujulikana mara moja anakotoka lakini wengine wakisema ni mfanyakazi wa tra maeneo ya posta ameanguka ghafla mtaa wa samora na kufariki hapohapo bila kujulikana tatizo ni nini
mtu huyo ambaye alikuwa anatembea kawaida lakini ghafla alianguka bila kuguswa na mtu yeyote na watu walipomfwata walikuta tayari amefariki dunia
ni tukio la kusikitisha sana kwani alikuwa mtu wa kawaida tu ametoka kazini lakini mauti yakamkuta akiwa anatembea 
 WANANCHI MAMIA WALIOJITOKEZA KUSHANGAA TUKIO HILO LA HUZUNI SAA LILILOTOKEA MAENEO YA POSTA MTAA WA SAMORA JIONI YA LEO
 MWILI WA MAREHEMU HUYO UKIWA NDANI YA GARI LA POLISI TAYARI KUONDOLEWA MAENEO HAYO
 
 hadi tunarusha habari hii bado hatujajua alikuwa anasumbuliwa na nini
 

No comments: