Thursday, May 9, 2013

HUYU NDIE MRIDHI WA FAGASON MAN U ANATISHA SOMA HISTORIA YAKE HAPA

    KLABU ya Manchester United inajiandaa kumtangaza David Moyes Alhamisi jioni kuwa kocha wake mpya.
     Ferguson asubuhi ya Jumatano alitangaza kuhitimisha miaka yake 27 ya kufanya kazi Old Trafford na ataaga katika mchezo dhidi ya West Brom Mei 19.
BIN ZUBEIRY kupitia Sportsmail inafahamu kwamba United itamtangaza rasmi mrithi wa Sir Alex Ferguson baada ya kufikia naye makubaliano Na hiyo inamaanisha kwamba, mtu huyo hatakuwa Jose Mourinho, licha ya mazungumzo yake na Chelsea kubuma wiki hii.
     Mjumbe wa bodi ya United, Sir Bobby Charlton - inaaminika anavutiwa zaidi na Moyes kutokana na kazi yake nzuri Everton na namna anavyojitolea katika kutengeneza timu. Mscotland huyo alikutana na Mwenyekiti wa Everton, Bill Kenwright ofisini kwake mjini London jioni ya jana.
Catch me if you can: David Moyes appeared in good spirits as he left Bill Kenwright's offices
David Moyes
Nichukue kama wewe unaweza: David Moyes akiwa mwenye furaha wakati anatoka ofisini kwa Bill Kenwright' jana
David Moyes
David Moyes
Mlango mmoja umefungwa: David Moyes akiwasili na kuondoka ofisini kwa Bill Kenwright
Enlarge Heading for United? David Moyes (right) leaves Everton's Finch Farm training complex today driven by his agent brother Kenny
Anakwenda United? David Moyes (kulia) akiondoka Uwanja wa mazoezi wa Everton, Finch Farm jana akiendeshwa na mdogo wa wakala wake, Kenny
PIC..TONY SPENCER 07875497050 DAVID MOYES LEAVES EVERTON TRAINING GROUND TODAY(WEDS)
PIC..TONY SPENCER 07875497050 DAVID MOYES LEAVES EVERTON TRAINING GROUND TODAY(WEDS)
Mabosi wa Old Trafford wanaamini kwamba kocha huyo wa Everton anaweza kurithi nafasi itakayoachwa wazi na Fergie Mwisho wa msimu.
Moyes anamaliza mkataba wake na Everton mwisho wa msimu huu na bado hakuna makubaliano ya mkataba mpya ndani ya Goodison Park.
Moyes, (50), aliwahi kusema kwamba anataka kusubiri mpaka mwisho wa msimu kabla ya kuamua kama anaongeza mkataba Goodison Park alipokaa kwa miaka 12 ama la.
Atakuwa na furaha kufanya kazi na Ferguson, ambaye amepata shavu kwenye Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo.
Moyes anapewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya Ferguson kutokana na kutokutetereka akiwa na Everton na mapenzi yake kwa klabu hiyo.
Tabia yake ya kukuza vipaji ni kitu kingine ambacho kinampa pointi za juu kwenye mchakato huu wa kumpata mbadala wa Ferguson.
Mkuu wa Manchester United, David Gill alikiambia kituo cha MUTV: “Tulijua siku hii itakuaja na tumekuwa tukijiandaa kwa hilo. Bodi itasikiliza maoni ya Sir Alex na Sir Bobby (Charlton)  kwa maoni yao.”
Charlton aliongelea kuhusu kukerwa na uvumi kwamba Mourinho atamrithi Ferguson. 
Alisema: “Mourinho ni kocha mzuro, lakini hili ndilo naweza kulisema, anaongea sana kitu ambacho sikipendi. Japokuwa ni kocha mzuri.”
Hatahivyo, Gill alisema kwamba mtu atakaye mrithi Ferguson lazima awe na uzoefu wa kutosha wa soka la England na Ulaya, hili linaweza kumnyima nafasi Moyes. Moyes anauzoefu mdogo sana kwenye soka la Ulaya.
Mourinho, ambaye anatarajiwa kuondoka Real Madrid wakati wa kiangazi amekuwa akihusishwa sana na kurudi Chelsea. 
Ujio wake Stamford Bridge unaonekana kugonga mwamba baada ta Roman Abramovich kukataa kumlipia ada yake ya kuvunja mkataba na Real Madrid na malipo ya wafuasi wa Mourinho.
Abramovich alimlipa Mourinho na wafuasi wake kiasi cha pauni milioni 17 baada ya kuwatimua mwaka 2006, na sasa hivi inasemekana ilikumchukua Mourinho kutoka Madrid ni lazima kumlipia kiasi cha pauni milioni 20, lakini dau hilo linakaribisha mazungumzo.
Mourinho bado anapewa nafasi kubwa ya kumrithi, Rafa Benitez, Stamford Bridge, lakini Chelsea wanataka kusimamia zaidi usajili wa wachezaji, kuliko ilivyokuwa mara ya kwanza alipotua kutoka Porto mwaka 2004.
Moyes, Mscotland mwenzake Ferguson amekuwa akiiongoza Everton kwa zaidi ya miaka 10 na ni kocha wa tatu kwa kukaa muda mrefu zaidi kwenye Ligi Kuu England.
Akiwa Everton hajatetereka  na amekuwa na mapenzi ya kweli na timu hiyo.
Hata hivyo kuna maswali juu ya ubora wake kuongoza timu kubwa – kikosi chake cha Everton hakijawahi kuzifunga Manchester United, Chelsea, Arsenal au Liverpool ugenini licha ya kujaribu mara 44.
Lakini akiwa na bajeti kubwa kwenye timu kama Man United, ni wazi Moyes anauwezo wa kufanya makubwa Old Trafford.
Yuko tayari kufanya kazi huku akiangaliwa kwa karibu na Ferguson ambaye atakuwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi. Moyes pia anauwezo wa kukuza vijana , kitu ambacho Man United wanakiamini sana.

No comments: