Tuesday, May 21, 2013

NYUMBA ZABOMOLEWA DAR,WAHUSIKA WAPANGA KUANDAMANA HADI KWA PINDA


Ni sehemu ya Nyumba kubwa iliyokuwepo katika Maeneo ya  Kitongoji cha Mkombozi kijiji cha Kivule jijini Dar es Salaam, iliyobomolewa  na Polisi kwa Madai kuwa wananchi hao hawaruhusiwi kukaa katika Maeneo hayo, ambapo Nyumba zaidi ya 300 zilibomolewa na wahanga hao wamepanga kwenda kwa Waziri Mkuu kupata haki yao baada ya kuomba msaada katika ngazi zote za Chini na kutopata Msaada wowote.



Takriban Wakazi zaidi ya 500 katika kijiji cha Mkombozi kata ya Kivule Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam wasiokuwa na makazi ya kuishi baada ya Kubomolewa nyumba zao na  Polisi kwa madai ya kuwa hawastahili kuishi maeneo hayo wanajiandaa kufanya Maandamano ya kwenda katika Ofisi ya waziri Mkuu kupeleka malalamiko yao kwa ajili ya kupata haki yao.

Akizungumza katika kikao cha wakazi hao Katibu  wa wahanga hao, Mwanaharakati  Julius  Zephania, alisema kuwa,  wanaamini kuwa haki yao ipo ila ni swala la wao kuipigania.

Zefania alisema kuwa, siku ya kwenda kwa Waziri mkuu imekaribia ambayo wanaamini kuwa, ndio mkombozi wao ambapo alimwomba waziri mkuu watakapofika wawaikiliza na kuwahurumia kwani nao ni wananchi kama walivyo watu wengine.

Naye Mwenyikiti wa wahanga hao, Bw, Habibu Iddi amesema kuwa, sababu zilizofanywa wao kubomolewa nyumba zao ni kwamba hawaruhusiwi kukaa katika Eneo hilo na kwamba  anayewanyanyasa ni mtu mmoja walio mtaja kwa Majina ya Jordan Rugimbana ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kinondoni ambaye anadai kuwa Eneo hilo ni lake.

“Tunamshangaa sana huyu mtu kutubomolea nyumba zetu , sasa sisi umefika wakati wetu wa kupata haki yetu na ni lazima tufike kwa  Waziri Mkuu kwani tunaamini ndiye pekee anayeweza kutusikiliza. MAASINDA ilimtafuta Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Bw,  Joseph Gasaya ambapo amesema kuwa, swala hilo ameshalifikisha katika ngazi za juu lakini bado anazungushwazungushwa ambapo alisema kuwa ni haki ya wananchi wake kwenda Mahakamani.

 
 


No comments: