Monday, May 27, 2013

spurs yatoa paundi milioni 10 kumsajili david villa

vila 279c1
Mshambuliaji wa Barcelona, David Villa anatakiwa Tottenham kwa Pauni Milioni 10
KLABU ya Tottenham imeanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili kwa Pauni Milioni 10, mshambuliaji wa Barcelona David Villa na pia wamefufua nia yao ya kumsajili mchezaji wanayemtaka kwa muda mrefu, Leandro Damiao.

Andre Villas-Boas aliibua nia ya kumsajili ya Villa mapema mwezi huu na sasa klabu yake nchini Hispania iko tayari kuisikiliza Spurs katika mpango wao wa kumnasa mkali huyo wa mabao kwa ajili ya msimu ujao.
Klabu hiyo ya Nou Camp iko tayari kumuuza mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania ambaye amejikuta katika wakati mgumu kupata namba katika kikosi cha kwanza na anaweza akauzwa kwa Pauni Milioni 12. Chanzo: binzubeiry

No comments: