Thursday, May 23, 2013

umbea kidogo----MAHAKAMA YARUHUSU DK SLAA NA JOSEPHINE KUOANA




       Kutokana na kesi iliyokuwa imefunguliwa na Aminiel Mahimbo vs Josephine Mushumbusi kesi ya rufaa ya kupinga talaka iliyotolewa na mahakama ya mwanzo Sinza katika kesi ya ndoa namba 4/2012 , baada ya kesi hiyo kutupiliwa mbali na mahakama ya hakimu mkazi mahakama ya wilaya ya kinondoni ndugu Wambura, katika kesi ya rufaa namba 32/2012.

       Ametoa uamuzi huo baada ya kuridhika kwamba kulikuwa na ushahidi wa kutosha kwa mahakama ya mwanzo kutoa talaka hiyo na hivyo Josephine ni mtalikiwa rasmi.

       Kutokana na hukumu hiyo, Josephine ana haki ya kuolewa na mtu mwingine kwa kuwa ni mtalakiwa.

No comments: