Wednesday, May 15, 2013

WADAU WA MASWALA YA AJIRA NA KAZI WAKUTANA LEO KUHUSU KUJADILI SWALA ZIMA LA AJIRA


Wadau watafiti wa Maswala ya Ajira na Kazi wakiwa Kwenye Picha ya Pamoja baada ya Mkutano uliokuwa unajadili kuhusu kufanya Utafiti wa Maswala ya Ajira na Kazi.
        Wadau wa tafiti wa hali ya nguvu kazi na ajira nchini Tanzania wamekutana katika mkutano leo uliofanyika katika Hoteli ya Peacok jijini Dar es salaam mkutano wenye lengo la kujadili kwa pamoja upatikanaji wa ajira nchini na kupanga jinsi ya kufanya tafiti juu ya upatikanaji wa ajira nchini.
         
        Akisoma hotuba ya katibu mkuu wa wizara ya kazi na ajira mwakilishi wake katika ufunguzi huo Bw Ally Ahmed amesema Tanzania bado inapita katika kipindi kigumu sana katika maswala ya ajira hususani kwa vijana hivyo ni lazima watafiti mbalimbali wajitokeze kufanya tafiti na hatimaye kutoa sulihisho la upatikanaji wa ajira nchini
Ameongeza kuwa nchini Tanzania zaidi ya asilimia 75.1 ya watu wenye uweo wa kufanya kazi wanajihusisha na shguhuli zilizo katika secta isiyo rasmi.
          
       Aidha amewaomba wadau hao wa tafiti kuhakikisha wanajadili kwa pamoja na baadae kutoka na tafiti ambazo zitasaidia kuondokana na tatizo la ajira nchini huku akiahidi serikali kuwasaidia kwa hali na mali kuhakikisha wanafanikiwa katika suala hilo
Kwa mujibu wa wadau hao maeneo muhimu watakayoyajadili na mwishoni kuyafanyia tafiti ni hali ya ajira nchini,hali ya kipato nchini,pamoja na hali ya ajira kwa watoto.

Wakiwa pamoja katika Pozzz

No comments: