Thursday, May 16, 2013

WIKI YA MAWASILIANO DUNIANI YAZINDULIWA RASMI LEO JIJINI DAR ES SALAAM




Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA leo imefungua Rasmi Sherehe ya wiki ya Mawasiliano Duniani jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika Ufunguzi huo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Prof John Nkoma, amesema kuwa, katika Maadhimisho hayo wamelenga kuimarisha Mawasiliano katika Vyombo vya Usafiri, na Barabarani.
Nkoma amesema kuwa, watahakikisha kuwa wanasimamia ipasavyo, mawasiliano ya Barabarani ili kupunguza ajali zinazoweza kutokea na zisizokuwa na Mpango ambapo watasimamia katika ununuzi wa Vifaa vya kupimia Mwendo kasi vilivyo na kiwango.

Amesema kuwa anatoa Rai kwa Madereva wote Tanzania, kutumia Teknolojia ya Mawasiliano vizuri ili kupunguza ajali zinazoweza kujitokeza kizembe.

Ameendelea kusema kuwa Madereva wengi wanaendesha Magari wakiwa wanazungumza na Simu jambo ambalo linaweza kusababisha ajali kwa asilimia Kubwa.

Prof Nkoma akisikiliza Mada wakati wa ufunguzi wa sherehe hizo zilizofanyika leo katika Ukumbi wa Mlimani Cty jijini Dar es Salaam.

No comments: