Tuesday, June 18, 2013
BOMU LA ARUSHA MTOTO ATOA USHUHUDA ASEMA ALIPIGWA RISASI NA BOMU
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye ametoa tamko kuwa chama chake kina ushahidi wa kutosha wa watu waliohusika na tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa kampeni wa chama hicho.
Dk Kisanga alisema huyo ni mmoja wa watoto watano, waliojeruhiwa wakati wakitoka madrasa huko Kaloleni, jirani na Uwanja wa Soweto kulipokuwa na mkutano na alifariki jana asubuhi hospitalini hapo.
Alisema watoto wengine wawili ambao ni ndugu; Fatuma na Sharifa Jumanne wamepelekwa Nairobi kwa matibabu zaidi baada ya miili yao kukutwa na vyuma. Dk Kisanga aliwataja watoto wengine waliojeruhiwa kuwa ni Fahad Jamal (7) ambaye yupo ICU akisubiri timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na hali yake kutoruhusu kusafirishwa. Pia yupo Abubakar Adam (11) ambaye amejeruhiwa mguuni na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa, Mount Meru.
Mtoto aeleza kupigwa risasiAdam alisema jana kuwa alipigwa risasi na mtu aliyekuwa amevalia sare za polisi, wakati akitoka madrasa akiwa na ndugu yake, Fahdi katika eneo la Soweto.
Alisema akiwa njiani, aliona watu wakimkimbiza mtu na ghafla alishangaa kupigwa risasi na kuanguka chini.
Muuguzi wa zamu, katika katika wodi ya watoto katika Hospitali ya Mount Meru, Asha Semdeli alisema jana kuwa mtoto huyo ana vyuma viwili katika mguu wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment