MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI MAELEZO ASSA MWAMBENE |
Waandishi wa habari nchini
wametakiwa kutambua kuwa na wao wana wajibu mkubwa wa kulinda amani ya nchi badala ya kuandika
habari ambazo zinaweza kuigawa nchi kwa misingi ya kidini,kisiasa kikabila ama
kikanda
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa idara ya
habari maelezo bw ASSA MWAMBENE wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
gazeti moja la leo liitwalo MAWIO lililochapisha
habari ambayo kwa mujibu wa mkurugenzi huyo amesema ni habari ambayo inachochea
udini serekalini
Amesema katika gazeti hilo limeeleza kuwa
viongozi wa madhehebu wa kikristo wamepitisha azimio kuwa wasitishe uhusiano
wao na serikali kwa kuwa serikali inawatenga wakristo huku likiweka picha kadhaa
za viongozi wa dini jambo ambalo amesema ni uchochezi mkubwa na lazima ukemewe
ili nchi iendelee kuwa na amani
Amesema lazima waandishi watambue kuwa
viongozi wa dini ni watu ambao wanalea roho za watu na wanaheshimika sana na waumini wao hivyo
kitendo cha kuwachafua kwenye vyombo vya habari ni kuwashushia hadhi na heshima
walionayo kwa waumini wao
Aidha katika hatua nyingine bw MWAMBENE amesema idara ya
habari maelezo inamtaka mhariri wa gazeti hilo
kufika mara moja katika ofisi zao ili kutoa utetezi juu ya habari hiyo kabla
sheria haijachukua mkondo wake
PICHA NA MAKTABA
No comments:
Post a Comment