Thursday, June 6, 2013

MUUNGANO WA SERIKALI TATU WAANZA KUPINGWA

BAADHI YA WAASISI WA CHAAMA CHA TPP WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI JJINI DAR ES SALAAM MUDA MFUPI ULIOPITA
    Chama cha siasa cha TPP Tanzania people party kimetoa maoni yake juu ya rasimu ya katiba mpya iliyotolewa na tume ya mabadiliko ya katiba tannzania mapema wiki hii na kukosoa kipengele cha kuwa na muungano wa serikali tatu kwa maelezo kuwa kitaongeza vitendo vya ufisadi serikalini.
      Akizungumza na waandish wa habari jijini dare s salaam moja kati ya waasisi wa chama hicho bw BW ALECK CHEMPONDA amesema kuwa uwepo wa serikali tatu utaongeza wingi wa mawaziri na viongozi wa serikali ambao kwa kiasi kikubwa utachangia matumizi mabaya ya rasilimali ya serikali ikiwemo mishahara yao.
       Aidha amesema ni muda sasa wa mabaraza ya katiba kkukaa na kujadili rasimu hiyo kiundani ili Tanzania iweze kupata katiba imara na sio kuweka ushabiki wakati huu
       Katika hatua nyingine kiongozi huyo amekanusha uvumi uliokuwa unaenea kwenye vyombo vya habari kuwa chama hicho kimefutwa katika orodha ya vyama vya siasa na kusema sio kweli kwani chama hicho kipo imara na kinajiandaa na chaguzi zijazo

BW CHE MPONDA AMBAYE NI MUASISI PIA WA CHAMA HICHO

No comments: