Friday, June 7, 2013

STARS YAAPA KUIUA MOROCCO KESHO



KOCHA wa Taifa Stars, Kim Poulsen, amesema watahakikisha wanashambulia mwanzo mwisho kwenye mechi ya kuwania kufunzu Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Morocco, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Marrakesh, Morocco.
Boniface Wambura ambaye ni Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ameliambia gazeti hili kuwa, Kim amepanga kutumia mfumo wa kushambulia mwanzo mwisho ili ahakikishe wanafunga mabao ya mapema zaidi.
“Kocha anasema kuwa atatumia mfumo wa kushambulia mwanzo mwisho lengo ni kupata mabao ya mapema zaidi na kisha kuyalinda katika kipindi cha pili.
“Wachezaji wote wapo fiti, (Erasto) Nyoni amerejea na alifanya mazoezi kama kawaida lakini mwalimu anatarajia kumuanzisha (Thomas) Ulimwengu ambaye atacheza pacha na (Mbwana) Samatta, tutarejea nyumbani Jumapili,” alisema Wambura.


No comments: