Tuesday, June 18, 2013

WADAU WATAKIWA KULINDA HAKI ZA MTOTO


Watanzania wamekumbushwa kutambua kuwa kila mwanajamii ana jukumu la kulinda,kuheshimu,kusimamia na kutekeleza haki za mtoto badala ya kuwaachia wazazi wa watoto hao jambo ambalo limetajwa kuchangia kupotea kwa haki za watoto
          Hayo yamesemwa na  kamishna msaidizi wa ustawi wa jamii anayeshughulika na haki za watoto bw RABIKIRA  MUSHI katika maadhimisho ya mtoto wa africa yaliyoandaliwa na kituo cha sheria na haki za binadamu na kuadhimishwa jijini dar es salaam
          Katika maadhimisho hayo ambayo watoto kutoka zaidi ya shule 60 jijini dar es salaam  wameshiriki bw RABIKIRA amesema kuwa mambo kama kuwatumikishha watoto ni kosa kisheria na ni lazima serikali isimame kidete kuchukua hatua kali kwa wale wote wanaofanya mambo hayo
          Akitolea mfano baadhi ya watoto ambao wamekuwa wakifungiwa ndani na wazazi wao kutokana na mapungufu yao ikiwemo ulemavu ametaka jamii kufichua wazazi wanaofanya hivyo ili sheria ichukue mkondo wake
Naye mkurugenzi wa  kituo hicho bi HELLEN KIJO BISIMBA akizungumzia ushiriki wa watoto katika katiba mpya amesema lazima tume ya katiba itambue kuwa na watoto nao wanahitaji kushirikishwa katika mchakato wa kupata katiba mpya kwani nao wana mambo wanahitaji yawepo ndani ya katiba mpya ambayo yanawagusa
       Katika hatua nyingine bi HELLEN ameiomba tume ya  katiba kumtafsiri mtoto kuwa ni yupi ili atambulike tofauti na ilivyo sasa kwenye rasimu ya katiba mpya ambayo amesema haijamtafsiri mtoto.




No comments: