Tuesday, July 9, 2013

KULIPA BILI DAWASCO SASA KWARAHISISHWA

BAADH YA WAWAKILISHI WA MAKAMPUNI HAYO YA SIMU NA BENKI WAKIWA KATIKA UZINDUZI HUO

BW JACKSON MIDALA MABAYE NI AFISA MTENDAJI MKUU WA DAWASCO AKIONYESHA BAADH YA MASHINE ZITAKAZOTUMIKA KATIKA KULIPIA BILI

   Shirika la maji safi na maji taka dar es salaam DAWASCO limezindua rasmi mpango wake kwa wateja  kulipa malipo ya huduma ya maji  kwa kutumia technologia jambo ambalo litasaidia kurahisisha huduma hiyo kwa wateja wake

         Akizumgumza katika uzinduzi huo afisa mtendaji mkuu wa DAWASCO bwJACKSONI MIDALA amesema kuwa njia hiyo itawafanya wateja wengi kuweza kulipia bili ya maji kwa urahisi na haraka zaidi tofauti na ilipokuwa hapo awali ambapo wateja walilazimika kufika katika ofisi zao kwa ajili ya malipo

          Katika huduma hiyo wateja wa maji dar es salaam wataweza kulipa bili zao kwa kutumia mitandao yote ya simu Tanzania pamoja na baaadhi ya benki hapa nchini ambapo mfumo huo umeelezwa kusaidia kupunguza msongamano uliokuwepo katika maofisi ya dawasco wakati wa kulipa bili

          Aidha Bw MIDALA amesema kuwa wapo wateja na wananchi waopotoshwa kuwa huduma hiyo sio salama ambao amewatoa wasiwasi na kusema kuwa huduma hiyo ni salama na ni njia nzuri zaidi kulilo iliyokuwa inatumika hapo awali.
WAANDISHI WA HABARI WALIOHUDHURIA WAKISIKILIZA KWA MAKINI 

No comments: