Sunday, July 7, 2013

MAAJABU..MWARABU ASHIKWA AKIMBAKA TAHIRA HUKO RUVUMA




           JESHI la polisi mkoani Ruvuma linamshikiria mfanyabiashara mmoja Jamali Nassoro (67) mwenye asili ya kiarabu mkazi wa eneo la Making'inda katika manispaa ya Songea kwa tuhuma za kumbaka na kumsababishia ujauzito wa mimba ya miezi 5 msichana mwenye umri wa miaka 27 ambaye anadaiwa kuwa na ugonjwa wa utindio wa ubongo(TAILA) ambaye jina lake tunalo limehifadhiwa.



          Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma George Chiposi alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo mwenye asili ya kiarabu limetokea hivi karibuni baada ya wazazi wa msichana kubaini kuwa mtoto wao yupo tofauti kimaumbile na kuchukuwa jukumu la kwenda kumpima ambako vipimo vilionesha kuwa ni mjamzito wa miezi 5.

         Chiposi alisema kuwa wazazi wa msichana huyo baada ya kubaini mtoto wao ni mjamzito walimuhoji ili kujuwa ni nani aliyemfanyia unyama huo ambapo licha ya kuwa msichana huyo ni tahira alieleza kwa shida kuwa alikamatwa kwa nguvu na kulazimishwa kutoa nguo yake ya ndani na Nassoro ambaye alimtaka ampelekee maji ya kuoga chumbani kwake.

Alifafanua zaidi kuwa wazazi wa msichana huyo ambao hakutaka kuwataja majina yao walifanya upelelezi wa kina ambao uliwalidhisa kuwa tukio hilo limefanywa na mfanya biashara huyo ambaye alikuwa amekaribishwa kuishi kwenye nyumba yao baada ya kutengana na mke wake wakati akisubiri kugawana mali walizochuma kwa pamoja.

          Alieleza zaidi kuwa mtuhumiwa Nassoro kwa hivi sasa anashikiliwa na polisi lakini yupo hospitali ya serikali ya Mkoa Songea(HOMSO) ambako amelazwa akidai kuwa anasumbuliwa na BP ya kushuka na kwamba Jumatatu ijayo anatarajiwa kufikishwa mahakamani na hata kama atakuwa hajaruhusiwa atasomewa mashtaka yake yanayomakabili akiwa amelala kitandani kwenye hospitali hiyo kwani upelelezi wa tukio hilo umeshakamilika.

            Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa Songea (HOMSO) Dkt. Benedkto Ngaiza amethibitisha kumpokea mfanyabiashara huyo Jamali Nassoro ambaye alipelekwa hopitalini hapo akiwa chini ya ulinzi mkali na amelazwa wodi ya wanaume namba saba akiwa anaendelea kupata matibabu.
VIA/demashonews

No comments: