Thursday, July 4, 2013

SERIKALI YASISITIZA SAFISA JIJI YA WAMACHINGA HAIKUWA NGUVU YA SODA INAENDELEA



         
         Kufuatia tamko lililotolewa na serikali kuhusu kuwaondoa wafanyabiashara wadodo wadogo katika maeneo yasiyo rasmi kwa kufanyia biashara halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeendelea kuthibiti wafanyabiashara hao.

             Akizungumza na Radio Upendo Afisa uhusiao na elimu kwa umma wa manispaa ya Ilala Bi TABU SHAIBU amesema mpango huo ni endelevu ambao ulianza kwa shule za msingi baada ya tamko kutoka kwa mkuu wa mkoa na kuagiza kila kiongozi awajibike katika eneo analosimamia.

          Amesema ili kuendeleza mpango mkakati wa  kuliweka jiji la dar es salaam katika hali ya usafi kila mfanyabiashara asiyekuwa na kibali maalum hataruhusiwa kufanya biashara katika eneo lolote na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa kila atakayekaidi amri hiyo.

           Hata hivyo Bi SHAIBU amewashauri wananchi kuzingatia usafi katika sehemu wanazoishi ikiwa ni pamoja na kuwapatia watoto wao elimu ya utunzaji  wa mazingira ili gharama ambazo zingetumika kufanya usafi katika maeneo hayo zitumike katika shughuli nyingine za kijamii.

No comments: