Friday, July 19, 2013

WAZIRI GHASIA AZINDUA BODI YA USHAURI YA DATS,AJIRA ZAAHIDIWA KWA VIJANA WA DAR

WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA  ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA HAWA GHASIA AKITOA HOTUBA YAKE 

HAPA WAZIRI AKIMKABIDHI VIFAA VYA KAZI MWENYEKITI MPYA WA BODI HIYO BW DAVID MFINANAGA

           Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa serikali za mitaa tamisemi mh  HAWA GHASIA amesema kuwa mradi wa mabasi yaendayo kwa kwasi unaokuja dar es salaam utasaidia kuwaajiri vijana wengi jambo litakoalosaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana jijini dar es salaam        Kauli hiyo ameitoa leo jijini dar es salaam katika hafla fupi ya uzinduzi wa bodi ya ushauri ya DATS yenye lengo la kusimamia na kutoa ushauri kwa serikali na Wadau kuhusu mradi huo mkubwa unaoendeshwa jijini dar es salaam         Mh GHASIA amesema serikali iliyo madarakani kupitia chama cha mapinduzi ccm imekuwa ikiwaahidi vijana ajira na kusema kuwa moja kati ya ajira hizo ni kuwepo kwa mabasi hayo yaendayo kwa kasi na kuwataka vijana kuchangamkia nafasi hizo pindi tu mradi huo utakapokamilika            Naye mwenyakiti mpya wa bodi hiyo ya ushauri ya DATS bw DAVIDI MFINANGA amesema kuwa bodi yake itahakikisha inafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kusimamia mradi huo na kuwaomba watanzania kuupokea kwa mikono miwili mradi huo kwani ni jambo la kujivunia kuwa na mabasi kama hayo katika jiji la dar es salaam        Katika hafla hiyo pia waziri GHASIA amewakabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia kazi wajumbe hao wa bodi mpya ya DATS

WAJUMBE WA BODI  YA DATS NAO WALIKABIDHIWA VIFAA HIVYO

No comments: