Thursday, July 4, 2013

WIZARA YA AFYA YATOA AJIRA ZA KUMWAGA



 
       Katika kupambana na upungufu wa wafanyakazi katika secta ya afya,serikali imefanikiwa kutoa ajira kwa watumishi wa afya 8869 katika mamlaka mbalimbali za afya nchi nzima ili kupunguza tatizo hilo

         Hayo yamesemwa na msemaji wa wizara ya afta nchini bw NSACHRIS MWAMAJA leo wakati akizungumza na wanahabari kuhusu hatua ambazo serikali inazichukua kupambabna na tatizo la rasilimali watu katika secta ya afya.

        Bw MWAMAJA amesema kuwa ili kuboresha huduma ya afya nchini na utendaji kazi wake ni lazima kuhakikisha kuwa rasilimali watu inakuwepo ya kutosha hivyo wizara imeamua kupambana na tatizo hilo kwa kuhakikisha inaajiri  watumishi wa kutosha nchini

        Amesma kuwa watumishi walioajiriwa ni katika nyanja zote ikiwemo wauguzi,madactari,wakemia,wafamasia,watunza kumbukumbu wa afya,maafisa afya mazingira pamoja na maafisa wafiziotherapia.

        Aidha amewataka watumishi hao waliopata nafasi hizo kuhakikisha wanaripoti katika vituo vyao vya kazi mara moja na kuanza kazi ili kupunguza tatizo hilo

      Katika hatua nyingine Bw MWAMAJA amesema kuwa pamoja na jitihada hizo za serikali za kupunguza tatizo hi;lo lakini bado tatizo hilo ni kubwa kwani kwa sasa dactari mmoja anahudumia wagonjwa 18500 jambo ambalo amesema bado ni changamoto kubwa.

No comments: