Thursday, July 18, 2013

WIZI WA MAKONTENA WAPUNGUA BANDARINI

NAIBU MENEJA MAWASILIANO WA TPA  BI JANET RUZANGI (KATIKATI)AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM KUHUSU UFANYAJI KAZI WA MAMLAKA HIYO YA BANDARI TANZANIA PEMBENI YAKE NI WAFANYAKAZI WA MAMLAKA HIYO WALIOAMBATANA NAYE
     MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA IMESEMA KUWA KW A SASA WIZI WA MAKONTENA KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM UMEKWISHA KABISA.
               
              HAYO YAMESEMWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM NA  NAIBU MENEJA MAWASILIANO  WA MAMLAKA HIYO JANET ROZANGI  WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM KUHUSU SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA MAMLAKA HIYO
          
              BI RUZANGI AMESEMA KUWA KUANZIA MWAKA JANA KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM  HAKUJATOKEA WIZI WA KONTENA HATA MOJA JAMBO AMBALO AMWSEMA NI MAFANIKIO MAKUBWA YA MAMLAKA HIYO KATIKA KUPAMBANA NA TATIZO LA WIZI BANDARINI
           
        AMESEMA KUWA ULINZI UMEIMARISHWA SANA KATIKA BANDARI NA MATOKEO YAKE NI KUPUNGUA KWA WIZI KATIKA BANDARI HIYO.
              
               AIDHA AMESEMA KUWA MATUKIO YA WIZI YAMEPUNGUA KUTOKA MATUKIO 21 MWAKA 2011 HADI KUFIKIA MATUKIO 7 MWAKA 2012 .AMESEMA KUWA  HADI KUFIKIA MWEZI JUNI MWAKA 2013 NI MATUKIO MATATU TU YA WIZI WA MALI YALIYOTOKEA.
           
          HATA HIVYO TANGU MWEZI JUNI 2012 HADI SASA HAKUNA WIZI WOWOTE WA KONTENA ULIOTOKEA KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM

No comments: