Thursday, November 21, 2013

HUYU NDIYE ALIYEPORA LAPTOP YA DK MVUNGI ANATAFUTWA UKIMWONA TOA TAARIFA MAPEMAPICHA YAKE NDIYO HII HAPA

MAMISHNA WA POLISI  KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM AKIONYESHA PICHA YA MTUHUMIWA ABDUL THABIT MAIGA AMBAYE NDIYE MWENYE LAPTOP HIYO



      Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kuwasaka wale wote wanahusika kwa namna moja au nyingine kusababisha kifo cha Dr. Sengondo Mvungi aliyevamiwa tarehe 03/11/2013, kujeruhiwa na kusababisha kifo chake. Katika tukio hilo pia viliibiwa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kompyuta ya marehemu (laptop aina ya HP).
           
            Hadi sasa watuhumiwa waliokwisha kamatwa ni 10 ambao tayari majina yao yalishatolewa mapema, hata hivyo katika upelelezi wa kina imegundulika kwamba kompyuta ya marehemu inamilikiwa isivyo halali na mtuhumiwa aitwaye ABDUL  S/O THABIT MAIGA CHIEF, umri MIAKA 20, mkazi wa VINGUNGUTI.
           
            Jeshi la Polisi Kanda Maalum linaendea kufanya jitihada kubwa kwa lengo la kuipata “laptop” hiyo pamoja na simu moja ya marehemu.  Sasa imegundulika kuwa  mtuhumiwa tajwa hapo juu ndiye anayeimiliki isivyo halali. Kuna dalili kuwa mtuhumiwa huyo amegundua kwamba anatafutwa  hivyo anakwepa kukamatwa na anajificha maeneo tofauti tofauti ya jiji ikiwa ni pamoja na kusafiri sehemu mbalimbali hapa nchini kukwepa mkono wa sheria.
          
             Laptop hiyo ni muhimu sana katika kukamilisha upelelezi wa shauri hilo na katika taratibu za kipolisi mtuhumiwa wa aina hiyo anatakiwa kutafutwa  kwa mujibu wa PGO No 238.
           

PICHA YAKE NDIO HII HAPA JAMANI

No comments: