Thursday, November 21, 2013

KAMA ULIKOSAMAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA YAFANYIKA JANA JIJINI DAR ES SALAAM.

Displaying Pix - 1.jpg
Naibu Waziri wa Fedha Bi. Saada Mkuya akizungumza na  wadau wa sekta mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika  leo jijini Dar es salaam.




KWA HABARI KAMILI BONYEZA HAPO CHINI-----------   
       
  
          Ikiwa ni takribani miaka 20 tangu kuasisiwa kwa Siku ya Takwimu Afrika, Serikali imesema ipo haja ya kufanyika kwa tathmini ya ufuatiliaji wa takwimu zinazotolewa na mchango wake katika  kupanga mipango ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini.

            Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyowashirikisha wadau wa sekta mbalimbali  leo jijini Dar es salaam, Naibu Waziri wa Fedha Bi. Saada Mkuya amesema kuwa maendeleo bora huchangiwa na upatikanaji na matumizi ya takwimu Bora zenye kuelezea uhalisia wa jamii husika.

        Amesema Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zinazothamini mchango wa takwimu katika maendeleo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa matumizi ya takwimu sahihi yanapewa  kipaumbele katika kutatua kero mbalimbali nchini zikiwemo za ulinzi wa raia na mali zao, elimu, Afya, Kilimo na ufugaji.

           Bi. Saada amesema kuwa kutoakana na umuhimu wa takwimu wapo baadhi ya watanzania wanaodhani kuwa takwimu zinatumiwa na serikali pekee jambo ambalo si sahihi na kuwataka kuondoa fikra hizo kutokana na umuhimu na mchango wake kuanzia ngazi ya familia.

        “Ni vema sote tukaelewa matumizi ya takwimu sahihi na mchango wake katika maendeleo kuanzia ngazi ya familia pia kuondoa mtazamo kuwa takwimu zinatumiwa na serikali pekee na kusahau kuwa takwimu zinagusa maisha ya kila siku ya watu na zina umuhimu mkubwa sana katika kupanga mipango ya maendeleo” Amesema.

           Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza kabla ya ufunguzi wa maadhimisho hayo amesema kuwa Tanzania kama  zilizvyo nchi nyingine za bara la Afrika huadhimisha Siku ya Takwimu Afrika  kwa kuwa Ofisi yake pamoja na majukumu mengine inaendelea kuboresha na kuimarisha matumizi ya takwimu nchini.

        Dkt. Chuwa  amesema  kuwa  takwimu ni maisha ya kila siku ya mwanadamu na zina umuhimu katika nyanja zote na kuongeza kuwa wabunge wanahitaji takwimu ili kupanga mipango ya maendeleo ya majimbo yao, serikali nayo inahitaji takwimu ili iweze kutekeleza mipango ya maendeleo na kutoa huduma stahiki kwa wananchi vilevile mashirika mbalimbali yanahitaji takwimu sahihi ili yaweze kuwahudumia wananchi.

          Kwa upande wake mwakilishi kutoka Benki ya Dunia Bw. Thomas Daniel Witz akitoa salam za Benki ya dunia wakati wa maadhimisho hayo amesema kuwa Benki ya dunia na washirika wa maendeleo wanatambua na kuthamini mafanikio makubwa yaliyopatikana katika ukusanyaji na utoaji wa takwimu nchini Tanzania.

          Amesema takwimu zinazotolewa zinaongeza uwazi na uwajibikaji na kuongeza uwezo wa nchi kupanga mipango ya maendeleo kwa wananchi wake.
“Napenda kuchukua fursa hii kuipongeza Tanzania kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa maendeleo na mafanikio makubwa ya utoaji wa takwimu ambazo sasa zinaiwezesha serikali na wadau kupanga mipango yao ya maendeleo”

Displaying Pix -4.jpg
Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini Thobias Andengenye  ambaye alikuwa miongoni mwa wachangiaji wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kuhusu mchango wa takwimu katika kufanikisha majukumu ya Jeshi la Polisi nchini.

  Naye Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini Thobias Andengenye  ambaye alikuwa miongoni mwa wachangiaji wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini amesema jeshi la polisi linathamini mchango wa takwimu katika kufanikisha majukumu yake.             Amesema takwimu zinalisaidia jeshi la polisi kutekeleza majukumbu mbalimbali yakiwemo ya ujenzi wa vituo vya polisi, kurahisisha mgawanyo wa ajira kufuatana na mahitaji ya wilaya na mikoa, uimarishaji wa mafunzo kulingana na uhitaji pamoja na kutambua ongezeko la makosa na namna ya kukabiliana nayo katika maeneo mbalimbali nchini.
 
Displaying Pix - 2.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza kabla ya ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika. Amesema kuwa Ofisi yake pamoja na majukumu mengine inaendelea kuhimiza matumizi ya takwimu kutoka katika vyanzo sahihi kwa mipango ya maendeleo.

No comments: