Monday, November 18, 2013

MZEE NELSON MANDELA BADO YUPO CHINI YA MADAKTARI 22, SASA HIVI ANAPUMUA BILA MSAADA WA MASHINE.


Nelson Mandela, Winnie, Jacob Zuma 
           Mzee Nelson Mandela (katikati) akisaidiwa na rais Jacob Zuma kushoto na Winnie Mandela katika picha ya hivi karibuni.
                 CAPE TOWN. 
RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela anapumua bila ya msaada wa mashine ingawa hawezi kuzungumza kwa sasa.



endelea chini------
            Mke wa zamani wa kiongozi huyo, Winnie Madikizela-Mandela aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa (AFP), kuwa Mandela yuko chini ya uangalizi wa madaktari 22.
Winnie alisema kiongozi huyo anasumbuliwa na homa ya mapafu.
Alisema Mandela hawezi kuzungumza kwa kuwa amewekewa mipira mdomoni ili kuondoa maji kwenye mapafu yake.
“Kwa kweli hawezi kutamka neno lolote, pia sauti yake imekauka. Anawasiliana kwa ishara zaidi. Madaktari wanaamini sauti yake itarudi,” alisema.
Winnie alisema Mandela hivi sasa anatambua watu kitu ambacho kinawapa moyo. Kiongozi huyo wa kwanza mweusi Afrika Kusini, aliruhusiwa kutoka hospitali, Septemba Mosi, mwaka huu baada ya kulazwa kwa miezi mitatu.
Awali, Winne alikanusha madai kwamba mumewe huyo wa zamani alikuwa akiendelea kupumua kwa msaada wa mashine: “Nimesikia hizi taarifa kuwa Mandela anapumua kwa mashine. Habari hiyo si ya kweli.”
“Hivi sasa mkazo mkubwa ni kuhakikisha kuwa Mandela anawekwa katika hali ya usafi wa hali ya juu ili kuhakikisha hadhuriwi na vijidudu vya magonjwa mbalimbali. Chumba chake ni kama Chumba cha Wagonjwa Mahututi cha Hospitali (ICU).”

Mandela, ambaye alitumikia kifungo cha miaka 27 jela kabla ya kutoka na kuendeleza harakati za kudai haki kwa wote Afrika Kusini, alichaguliwa kuwa Rais wa taifa hilo mwaka 1994

No comments: