Tuesday, November 19, 2013

TASWIRA ZA PICHA KATIKA MAZISHI YA DKT. MVUNGI - KIJIJI CHA CHANJALE MWANGA KILIMANJARO HAPO JANA....TAZAMA HAPA

 Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha Josephat Lobullu (kulia) na Askofu wa Jimbo la Same Rogath Kimaryo wakiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi. Ibada hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chanjale wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa pia na Askofu Damian Dallu (katikati) wa Jimbo la Geita JUmatatu, Novemba 18, 2013.
endelea hapo chini------

 Mke wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba marehemu Dkt. Sengondo Mvungi, Bi. Anna Mvungi akiweka shada la maua katika kaburi la mume wake wakati wa mazishi kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013.
 Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi wakati wa mazishi kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro JUmatatu, Novemba 18, 2013.
 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi likishushwa kaburini wakati wa mazishi yaliyofanyika kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro  JUmatatu, Novemba 18, 2013.

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda, mkewe Mama Tunu, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba na viongozi wengine wakifuatilia ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi. Mazishi hayo yalifanyika kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro JUmatatu, Novemba 18, 2013.

 Familia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi ikifuatilia ibada ya mazishi iliyofanyika katika kijijini cha  Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013.
Askofu Damian Dallu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita akiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba marehemu Dkt. Sengondo Mvungi katika makaburi ya familia kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013.(picha  na
Omega S. Ngole,
Principal Information Officer,
Constitutional Review Commission (Tanzania),

No comments: