.

ZITO KABWE ATIMULIWA RASMI CHADEMA,STORY KAMILI HII HAPANa Karoli Vinsent
     
 Hali ya kisiasa ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema imefikia pabaya baada ya kumvua uwongozi wa juu Zitto Kabwe.
endelea hapo----------


   Zitto ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini,ikumbukwe mwanzoni mwa Novemba mwaka huu aliingia katika malumbano na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuhusiana na masuala ya posho, akituhumiwa na 

    Lema kuwa anakataa posho za vikao bungeni, lakini anapokea posho kutoka mashirika mbalimbali
Dar es Salaam. Suala la hatma ya Naibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe ndilo lililotawala katika siku ya pili ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho na kusababisha mvutano mkali miongoni mwa wajumbe.

    Pamoja na ukweli kuwa kulikuwa na ajenda kadhaa zilizokuwa zimepangwa kujadiliwa katika kikao hicho cha siku mbili kilichofanyika Dar es Salaam, suala la Zitto ndilo lililochukua muda mrefu zaidi kujadiliwa.

    Habari za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho ambayo imeifikia habari24 kuwa kikao hicho zilieleza kuwa wajumbe waligawanyika makundi mawili, baadhi wakipendekeza Zitto avuliwe nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu kwa maelezo kuwa anakwenda kinyume na taratibu za chama hicho na wengine wakipinga hatua hiyo kwa maelezo kuwa haina tija.

   Mpaka saa moja usiku jana jioni ambapo habari 24 ilizipata ni kuwa  kikao hicho kilikuwa bado kikiendelea na suala hilo lililokuwa chini ya ajenda ya hali ya siasa nchini.

    Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi wa chama hicho, Benson Kigaila aliahidi kuwa taarifa rasmi ya kikao hicho ingetolewa baadaye na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Tuhuma za Zitto

     Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, mwanzoni mwa Novemba mwaka huu aliingia katika malumbano na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuhusiana na masuala ya posho, akituhumiwa na Lema kuwa anakataa posho za vikao bungeni, lakini anapokea posho kutoka mashirika mbalimbali nchini.
Pia, aliingia katika malumbano na chama chake baada ya kutumia kofia yake ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kutuhumu vyama vya siasa kuwa hesabu zake hazikaguliwi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

    Kauli ambayo jana Kigaila aliitolea ufafanuzi na kueleza kuwa Chadema kimekaguliwa na hesabu zake tayari zipo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
Hekaheka za jana

     Mvutano wa jana ulianza baada ya Mbowe kufungua kikao hicho saa 4:00 asubuhi.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilizoifika habari 24  zilieleza kuwa baadhi ya wajumbe, wakiwamo wabunge, walitaka Zitto avuliwe nafasi aliyonayo na kuwa mwanachama wa kawaida, huku wengine wakipinga hatua hiyo kwa maelezo kuwa Zitto hakuwepo katika kikao hicho na kwamba alipaswa kusikilizwa.
“Baada ya hali kuwa hivyo, Mbowe alipendekeza kuwa Zitto asijadiliwe kwa kuwa hakuwepo katika kikao hicho,” kilieleza chanzo cha habari hizo.

     Zitto alikuwa katika safari ya kikazi huko Sudan Kusini akiwa amefuatana na wajumbe wa PAC.

    Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Zitto alitafutwa na alituma salamu kwa wajumbe wa kikao hicho akiwaeleza kuwa alikuwa njiani na kuahidi kuwa angehudhuria mara tu baada ya kuwasili.
“Zitto alituma ujumbe kuwa anakuja katika kikao, kilikuwa na ajenda nyingi lakini suala lake lilijadiliwa kwa kirefu sana,” kilieleza chanzo chetu. Licha ya ombi la Mbowe, bado wajumbe walishinikiza kuendelea kumjadili Zitto hivyo ni kusababisha kuchelewa kujadiliwa kwa ajenda nyingine.

    Tangu juzi, siku ya kwanza ya kikao hicho, ulinzi uliimarishwa nje ya Jengo la Ubungo Plaza na jana walinzi wa chama hicho, Red Brigade waliwatimua waandishi wa habari waliokaribia eneo hilo wakisema hayo ni maagizo kutoka kwa uongozi wa juu.
Yaliyojadiliwa

    Katika ufafanuzi wake kwa waandishi wa habari jana jioni, Kigaila alisema kikao hicho kilichoanza juzi, kimejadili mambo mbalimbali. Alisema juzi kikao hicho kilijadili muhtasari wa vikao viwili vya dharura vya Kamati Kuu vilivyofanyika hivi karibuni.
“Tumejadili taarifa ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki, Zanzibar unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni... tunathibitisha kuwa tutashiriki,” alisema.
“Kulikuwa na taarifa ya hesabu za chama zilizokaguliwa na kupelekwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na taarifa za fedha za utendaji kuanzia Kamati Kuu iliyopita mpaka Kamati Kuu ya sasa,” alisema Kigaila.

   Huku akionyesha kitabu cha ukaguzi wa fedha mwaka 2010/11 na 2011/12 alisema: “Kamati Kuu imeridhika kuwa chama kimekaguliwa na hatuna deni kwa msajili.
Ajenda za jana

   Alisema kikao cha jana kilijadili ajenda za uboreshaji wa jengo la makao mkuu pamoja na kupanga upya kurugenzi za chama hicho pamoja na nguvu kazi ya makao makuu ili kuweza kutekeleza vizuri majukumu yake.
“Ajenda inayoendelea hivi sasa ni ya uundaji wa programu ya `Chadema ni Msingi’, ambayo lengo lake ni kukijenga chama katika ngazi za chini kabisa. Huu ni mpango mkuu wa chama wa `Vuguvugu la Mabadiliko’ (M4C). Ajenda ya mwisho itakuwa ni kujadili hali ya kisiasa nchini.”
Zitto atinga usiku

     Zitto alifika katika kikao hicho jana saa 2.24 usiku akiwa na walinzi wanne na habari kutoka ndani zinasema kwamba mara baada ya kuingia, ajenda ya kumjadili ilirejea. Ilielezwa kwamba alipewa nafasi ya kujitetea baada ya kusomewa ‘mashtaka’ yaliyokuwa yakimkabili.

   Mwandishi wa blog hii aliyekuwa katika eneo hilo anasema baada ya kurejeshwa kwa agenda hiyo malumbano makali yalizuka kwani wajumbe walikuwa wazungumza kwa sauti za juu na jazba kiasi

     Huku wakikosa imani na Zitto Kabwe kwa kitendo chake cha  kukisariti chama hicho,kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kilichopo ndani ya mkutano huo jana kilisema ajenda ya kumfukuza Zitto Kabwe jana ilikuwa ukitawala na kufikia hatu ya kifika hatua ya kumvua uongozi wa chama hicho na pia na kutaka apewe siku kazaa kwann asivuliwe uwana chama wa chama hicho.

Uchunguzi uliofanywa na Habari24 umebaini, uwenda yale yalioandikwa kwenye wakala uliosambazwa kwenye mitandao juu ya hujuma  anayofanya zitto kabwe na kushikiliana na baadhi ya maofisa wa usalama wa taifa kuhusu kukiujumu chama hicho uwenda ikawa sababu iliyowafanya baadhi ya wajumbe wa mkuto huo kumfukuza zitto kabwe,

Ikumbukwe baada ya kusambaa kwa walaka huo kwenye mitandao ya kijamii wenye kichwa cha habari walaka wa siri kuhusu Zitto kabwe,Zitto kabwe mwenyewe aliibuka na kuupinga walaka huo na baadhi ya viongozi wa chadema pia waliupinga walaka huo wakisema huwenda ni ujuma za baadhi ya watu wasiokitakia jema chama hicho.

Katika hari ya kushangaza mwandishi wa blogs alishuhudia kwenye mitandao wa kijamii amabapo uliwekwa walaka huo, katika hali ya kushangaza baadhi viongozi wa chama cha chadema waaliweka alama ya ku like kama kuunga mkono yale yalioandikwa kwenye walaka ule na pia jambo jingine walaka ule ulichapishwa kwenye  blog ya kiongozi wa chadema na jina tunalo tunaliifadhi na kutia mashaka kuhusu ukweli walaka huo

Habari hii imeandikwa na Karoli vinsent pamoja na kushirikiana na Gazeti la mwananchi pamoja na vyanzo mbalimbali ndani ya chadema

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.