Monday, March 25, 2013

KIBANDA YUKO FITI KWA SASA

KIBANDA YUKO FITI KWA SASA


 
  


Pichani ni Mhariri Mtendaji wa New Habari Cooperation, Absolom Kibanda ( katikati) akiwa na Hoyce Temu (kushoto)  na Angela Semaya nchini Afrika Kusini wakati akina dada hao walipomtembelea kumjulia hali. Kwa Mujibu wa Hoyce Kibanda anawasilimu sana Watanzania wote nay eye yupo vizuri sasa akiendelea na matibabu.


JUKWAA LA KATIBA TANZANIA YAITAKA TUME YA KATIBA KUSHIRIKISHA WANANCHI KATIKA SWALA ZIMA LA MCHAKATO WA UTAFUTAJI WA MAONI YA KATIBA MPYA 

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba (aliyvalia Shati jekundu) akifafanua Jambo Mbele ya Waandishi wa Habari leo katika Makao Makuu ya Ofisi ya Jukwaa la Katiba jijini Dar es Salaam ambapo amezungumzia Mchakato wa Kura za maoni juu ya Rasimu ya Katiba Mpya Zimbabwe na Mafunzo Makuu kwa Mchakato wa katibba Mpya Tanzania.

Amesema kuwa Moja ya Sababu iliyosababisha Zimbabwe kukosa Katiba yenye uhakika ni kukosekana kwa Elimu ya Uraia kwa Wananchi pamoja na kutoshirikishwa kwa Wananchi katika Swala zima la Mchakato wa kutafuta Maoni.

Bw Kibamba amesema kuwa, yanahitajika Marekebisho ya Haraka ya Sheria ya Mabadiliko ya katiba ya Mwaka 2011 ili kuboresha Bunge la katiba na kura ya Maoni ikiwemo kuweka tarehe Muhimu za Matukio. "Marekebisho hayo yalikwisha andikwa na  Mhe, Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete na itakuwa ni kumwangusha endapo hayatatekelezwa", amesema Kibamba. Amesema kuwa, Mabadiliko yanayohusu muundo na Uteuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Sheria Zote zinazohusu uchaguzi yafanyike sasa ili kuondoa hofu iliyopo Nchini kuwa tume hii inatumika  kubadilisha matokeo au kuchakachua kama inavyojulikana mitaani. Ameongeza kuwa, Wananchi wanapaswa kushirikishwa katika mchakato mzima hadi kupatikana kwa katiba mpya, kwani wasiposhirikishwa watakata tamaa na kuacha mchakato mzima kubaki kuwa ni wanasiasa pekee, ambapo jambo hilo linapelekea kuwepo kwa mwitikio mdogo sana katika mchakato mzima wa wa kura ya maoni ya katiba mpya. Aidha ameongeza kuwa, kutokana na uchaguzi wa Zimbabwe Tanzania inapaswa kujifunza kuwa, kuchelewa kwa fedha kwa ajili ya kura za Maoni, ambapo Zimbabwe walipata fedha za kuendeshea shughuli nzima za kura ya Maoni siku chache kabla ya zoezi la kupiga kura ya maoni ambapo fedha nyingi zilipatikana kwa kuchelewa, ambapo Tanzania inajifunza kuwa  maandalizi ni jambo la Msingi yaani upatikanaji wa Fedha za uhakika mapema.  

Thursday, March 21, 2013

Z. ANTO KUTOA KAZI MPYA SIKU YA PASAKA


 

 


BAADA ya kuwa kimya kwa muda mrefu, mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ally Mohamed ‘Z. Anto’ usiku wa Pasaka anatarajia kutambulisha kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Tanzania’.


 

Akizungumza Dar es Salaam, Z.Anto alisema kazi hiyo ataitambulisha katika ukumbi wa Mnyaru nite club uliopo jijini Arusha.

 

“Nashukuru mungu kwa kupata shoo hii ambayo itanipa nafasi ya kuitambulisha ngoma yangu mpya, tukiwa na kundi zima la Solid Ground Famili kutoka Mabimbo jijini Dar es Salaam,” anasema.

 

Z.Anto anawaomba wakazi wa Arusha wajitokeze kwa wingi siku hiyo ili waweze kupata burudani iliyoenda shule kutoka kwake na kundi hilo ambalo lililiteka soko la muziki huo kipindi cha nyuma.

 

Mkali huyo alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Kisiwa cha Malavidavi’ licha ya kuwa na vibao vingi ambavyo vilivyofanya vizuri katika soko la muziki huo.

CHUO KIKUU HURIA KUSHIRIKIANA NA CHUO CHA TRIUMPHANT COLLAGE KUTOKA NAMIBIA


 

Mkuu wa Chuo Kikuu huria nchini Tanzania Prof, Tolly Mbwette akibadilishana Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano wa Kitaaluma baina ya chuo kikuu huria na Chuo kikuu cha Trimphant Collage-Widhoek Namibia. Anayepokea Mkataba ni Elizabeth Kiyangi Mkurugenzi Mtendaji wa Triumphant Collage.

Vyuo vikuu nchini Tanzania vimeshauriwa kuhakikisha vinajitanua kimataifa katika kutoa elimu yake jambo ambalo limetajwa kuwa litasaidia wanafunzi wa Tanzania kujifunza mambo mapya katika nchi nyingine.

Hayo yamesemwa leo na mkuu wa chuo  kikuu huria cha Tanzania Prf TOLLY MBWETTE wakati akisaini mkataba wa makubalioano ya ushirikiano na serikali ya Namibia kupitia chuo chake cha TRIUMPHANT COLLEGE mkataba wenye malengo ya kushirikiana kitaaluma baina ya vyuo hivyo viwili.


Prof, MBWTTE amesema kujitanua kimataifa ni jambo muhimu ambalo amesema moja kati ya faida zake kubwa ni kusaidia wanafunzi kupata elimu bora na yenye viwango vya kimataifa zaidi.

Aidha amesema chuo kikuu huria kimekuwa ni chuo kikuu cha kwanza kusaini mkataba wa kimataifa wa kusaidia katika elimu jambo ambalo amesema liafaa kuigwa kwa vyuo vingine ili visaidie katika kukuza elimu ya Tanzania.Mkuu wa Chuo Kikuu huria nchini Tanzania Prof, Tolly Mbwette (kulia) pamoja na Elizabeth Kiyangi Mkurugenzi Mtendaji wa Triumphant Collage wakiweka sahihi kwenye Mkataba wa Kushirikiana kitaaluma Baina ya Vyuo hivyo viwili.


Magazeti Leo Alhamisi

100 6755 5cc91
 

100 6760 3f560

100 6761 ce094

 

100 6763 438c8

 

100 6764 09891


WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKIWA VATICAN ROMA
IMG_0290Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  na Mkewe Tunu wakifanya mahojiano na mtangazaji wa Radio Vatican, Padri Richard Mjigwa (katikati)  kweye  moja kati ya studio  za Raido hiyo Mjini Roma walikohudhuria sherehe za  kusimikwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Diuniani, Papa Francis 1 Machi 20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

IMG_0507Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  na Mkewe Tunu wakiongozwa na Padri  Alquine Nyirenda wa Makao Makuu  ya Shirika la Watawa wa Benedikti, Roma kutoka kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro la Roma walikohudhuria  sherehe za  kumsimikwa kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis 1 kwenye viwanja vya Kanisa hiloMachi 19,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

IMG_0541Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakipata maelezo  kuhusu historia ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro la Roma kutoka kwa Padri Alquine Nyirenda wa Makao Makuu ya Shirika la Watawa wa wa Benedikti, Roma walikohudhuria sherehe za kusimikwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, Machi 202013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) IMG_0768Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Chakula (FAO), Jose Graziano da Silva wakati alipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo Mjini Roma, Machi 20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) IMG_0777Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisikiliza jambo kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO Bw. Jose Graziano da Silva kabla ya kusaini kitabu cha wageni baadae walifanya  mazungumzo yao katika   makao makuu ya FAO mjini Roma, Machi 20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) IMG_0784

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO Bw. Jose Graziano da Silva baada ya mazungumzo yao wakati alipotembelea  makao makuu ya FAO mjini Roma, Machi 20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAGUNDUZI watakiwa kugundua VITU VITAKAVYOWASAIDIA WANANCHI KATIKA JAMII: DK. MWERU

 
 

Watafiti nawanasayansi nchini Tanzania wametakiwa kufanya tafiti za kiungunduzi ambazozitaleta manufaa na kusaidia jamaii ya watanzania .

Hayo yamesemana leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dr. Mwele Malecela(pichani juu)wakatiwa semina ya siku moja ya wagunduzi mbalimbali iliyoandaliwa kwa pamoja kati yaNIMR na Shirika la Grand Challenges la
nchini Canada.

Dkt. Malecela amesema umefika wakati sasa kwa wagunduzi mbalimbali wa Kitanzaniakuanza kungundua njia mbalimbali za kuweza kutatua matatizo yaliyopo katika jamii hasa katika sekta ya afya.

Semina hiyo ya siku moja ilikuwa na lengo la kuhamasisha wangunduzi sekta ya afyaambapo baadhi ya wanasayansi wagunduzi kadhaa walitoa taarifa zao za awali za namna ya kukabiliana na matizo kadha hasa kwa Mama na mtoto.

Wagunduzikadhaa waliweza kuzungumzia gunduzi zao katika semina hiyo na miongini mwa hizoni pamoja na ile ya hali ya Utapiamlo unaofanywa na Dkt. Magreth Kagashe kutokaTaasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Bianadamu Ifakara ambayo inafanyika katika Vijiji vya Kilombero.

Ugunduzimwingine ni wa namna ya kusafisha maji na kuyaweka katika hali salama kupitianjia ya Takasa maji, na kuyaweka taika hali salama nay a usafi ugunduzi unaofanyana Kijakazi Mashoto na Ugunduzi mwingine ni matumizi ya Maua ya Rosella katika kukabiliana na Upungufu wa damu kwa mama na mtoto.

Dkt.Malecela amesema ya kuwa ugunduzi unaofanyika sasa na kupewa fedha na GrandChallenge ya Canada unatakiwa uwe ugunduzi ambao utaleta mabadiliko na kubadili maisha ya wananchi.

“Maranyingi wanasayansi wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali na kugundua matatizomengi katika jamii lakini mara chache watafiti hawa wametafuta suluhisho yahayo matatizo au magonjwa katika jamii hizo …kwahiyo hivi sasa wanasayansi wagunduziwa kitanzania umefikia hatua ya kugundua vitu ambavyo vitasaidia jamii,” alisemaDkt.Malecela.

Aidha nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Grand Challenge Canada, Peter Singer alisema kuwa
jumlya ya miradi 16 ya ugunduzi inayofanywa na wanasayansi wa kitanzania
itapatiwa fedha kupitia taasisi hiyo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Grand Challenge Canada, Peter Singer akizungumza na waandishi
wa habari mara baada ya semina hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya NIMR jijini Dar
es Salaam leo.Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dr. Mwele Malecela
akipiga picha na Afisa Mtendaji Mkuu wa Grand
Challenge Canada, Peter Singer mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari Makao
Makuu ya NIMR jijini Dar es Salaam leo.


Monday, March 18, 2013

ASKARI WA USALAMA BARABARANI AGONGWA NA GARI MPAKA KUFA NI BAADA YA MSAFARA WA RAIS KUPITA

Akizungumza na WAPO Radio FM kwa njia ya simu akiwa katika hospitali ya Muhimbili, Kamanda wa Kipolisi kwa mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela amesema marehemu WP2492 Koplo, Elikiza Nnko wa Usalama wa Barabarani, baada ya kupewa taarifa kuwa magari ya msafafa wa Rais yameshapita yote, alirudi barabarani ili kuongoza magari mengine pasipo kujua kuwa dereva mwenye gari Landrover Discovery lenye namba za usajili T328BML mali ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), alipoona msafara umepita, kwa kasi alichomoa gari na kutaka kuiunga ionekane kuwa ipo kwenye msafara wa Rais ili apate kupita kwa urahisi, na ndipo aliposababisha ajali na kifo na kisha kutoroka kuelekea maeneo ya Ubungo na kujichanganya na magari mengine. Jeshi la polisi limeshachukua hatua ya kuwasiliana na viongozi wa TAG ili kumpata mhusika.

Bofya kifute cha pleya hapo kuisikiliza taarifa hiyo.

 


Mchana wa leo tovuti ya GPL imeripoti tukio la kusikitisha la kifo cha Askari Polisi wa usalama Barabarani, aliyetambulika kwa jina la Elikiza (pichani juu, bofya kuona picha iliyofichwa nyuma yake), baada ya kugongwa na gari katika eneo la Bamaga, Sinza jijini Dar es Salaam.

Maelezo ya WillyIAm (via JF) yanayofuatia picha yanatoa taarifa zaidi:

Picture

Ndugu zangu, huyu mama alitusimamisha sisi tupishe msafara, tukaipisha na yeye akakaa pembeni, ulikua msafara wa magari zaidi ya 50 na yalikua speed kubwa tuu zikiwemo na ambulance.

Sasa huyu mama kosa lake pengine ni hili:

Alihisi kuna watu wameunga tela msafara wa jamaa so akawasimamisha mungu saidia alisimamisha gari 2 zilizokua in a very high speed. Bila ya kuangalia nyuma ya zile gari akaanza kuruhusu gari from Shekilango road na hapo ndipo Discovery 4 kama sio 3 ilipofika kwenye mataa ikiwa na speed kama 120 hivi ikashindwa kusimama na kutanua ili isigongane mna magari yanayo-cross from Shekilango.

Jinsi gani ambavyo kifo kinamuita mtu mama yule alikua upande wa TBC badala ya kua upande wa sinza so jamaa alichofanya ni kukwepa madaladala hamadi traffic huyu hapa jamaa akapita. Sasa sisi tulichokua tunakiona sekunde ya kwanza ni kua jamaa kapanda ukingo ya barabara na kusepa, ila baada ya sekunde kumi niligundua kua kuna tukio zaidi ya tulichokiona nikashuka as i was walking ndio nikaona kofia ya traffic akili ikanijia sasa na wala sikutaka kwenda kuona maana wanaotazama waliniashiria kua si kitu kizuri kutazama.

Ila nimejifunza kua maisha haya jamani hatujui lini ni siku yetu, yule mama nina uhakika kabisa hakujua kama angekutwa na lililomkuta.

Binafsi nimechukulia kama fundisho kwangu, sina mtazamo kama wa wachangiaji wengi wa juu yangu

WAIMBAJI WA TAMASHA LA PASAKA WATAMBULISHWA DARMwimbaji wa nyimbo za injili, Upendo Nkone akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa kuwatambulisha wanamuziki wataoshiriki tamasha la Pasaka jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama na kulia ni mwimbaji Bonny Mwaitege. (Picha na Habari Mseto Blog)Mwimbaji wa nyimbo za injili, Bonny Mwaitege akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa kuwatambulisha wanamuziki wataoshiriki tamasha la Pasaka jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama.Mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwatambulisha baadhi ya waimbaji watakaoshirika katika tamasha la Pasaka 2013.
WAIMBAJI Upendo Nkone na Boniface Mwaitege wamesema tamasha la mwaka huu wamejipanga vilivyo kufikisha neno la mungu kwa waamini watakaojitokeza siku ya tamasha hilo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza na waandishi wa habari, Nkone alisema inaonekana ana wapenzi wengi zaidi katika nyimbo za kumtukuza mungu ndio maana wamemchagua kupitia ujumbe mfupi wa simu za mkononi, hivyo ana deni la kuwalipa siku hiyo.

“Nimepata furaha kwa waamini kutambua kazi yangu, ndio maana na mimni najihisi nna deni, na nawaahidi kuimba wimbo mpya siku hiyo ambao “Nimebaki na Yesu” ambao unachochea ibada kwa waamini,” alisema Nkone.

Nkone alisema uimbaji wa nyimbo za injili ni mgumu iwapo utafanya vibaya na jamii pia itakukataa ambako pia waamini wanatakliwa kuisoma biblia na kuielewa sambamba na kumuomba mungu kwa dhati ya kweli.

Naye Mwaitege alisema amefurahi kupata bahati ya kuwa mmoja wa wahudumu wa neno la mungu siku hiyo kwa sababu tamasha la mwaka jana hakupata bahati ya kushiriki kwa sababu alikuwa safarini nchini Kenya.

“Mwaka jana nilitamani kuimba pamoja na Rebecca Malope lakini bahati haikuwa yangu, ingawa nimepata bahati ya kuimba na Sipho Mwakabane ambaye naye anatokea Afrika Kusini kama Malope na Watanzania wenzangu kama akina John Lissu, Upendo Kilahiro na Rose Muhando,” alisema Mwaitege.


Aidha Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama alisema siku ya Tamasha utafanyika uzinduzi wa albam ya kundi la Gloria Celebrations ‘Kwetu Pazuri’ itakayojulikana kama ‘Kuweni Macho’ ambayo itauzwa siku hiyo.

 

Tamasha hilo ambalo litafanyika pia katika mikoa ya Mbeya Aprili Mosi, Iringa Aprili 3, Aprili 6 mkoani Dodoma na Mwanza Aprili 7.


Viingilio katika tamasha hilo kwa VIP ni shilingi 50,000, Viti maalum shilingi 10,000, Viti vya kawaida 5000 na watoto shilingi 2000.

Mgeni rasmi katika tamasha hilo ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Tuesday, March 12, 2013

HIZI NDIZO ALAMA HASA.. ZA DINI YA KISHETANI FREEMASONAlama hii inapendwa kutumiwa sana na wengi wa watu hasa vijana lakini pia wazee, na wanatumia kwa kuiga na pasipo kujua kwamba ni alama ya Kishetani.Alama nyingine wakati wa kusalimiana kwa kushikana  mikonoHii ni alama kuu ya KifreemasonAlama nyingineHata hii pia

KWA HISANI YA MAASINDA BLOg

BASI LA KILIMANJARO LILIVYOPATA AJALI JANA

Baadhi ya abiria wakiwa nje ya basi lao la Kilimanjaroo Express lenye namba za usajili T860 BVA walilokuwa wamepanda wakitokea jijini Dar kuelekea jijini Arusha mapema leo asubuhi,ajali hiyo imetokea eneo la Mombo ambapo chanzo cha ajali hiyo kinaelezwa kuwa ni dereva wa basi hilo alikuwa akimkwepa muendesha baiskeli,matokeo yake basi hilo likakosa mwelekeo na kupinduka,aidha katika jali hiyo inaelezwa kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa lakini hakuna aliyepoteza maisha.

HABARI NA MAASINDA BLOG

RAIS KIKWETE AMTEMBELEA MZEE YUSUF MZIMBA ALIYELAZWA MUHIMBILI KWA KUGONGWA NA BODABODARais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Mzee` Yusuf Mzimba, mmoja wa wazee marufu wa Klabu ya Dar es salaam Young Africans (YANGA) ambaye amelezwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiuguza majeraha kufuatia kugongwa na BodaBoda wiki iliyopita Barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam. Mzee Mzimba amevunjika mguu wa kushoto na kupata majeraha ya usoni na mikononi. Hadi jana hali yake ilikuwa inaendelea vyema na Rais Kikwete amempa pole nyingi kwa maumivu aliyoyapata na kumtakia apate nafuu ya haraka. PICHA NA IKULUhabari na maasinda blog

MWANAFUNZI AANGUKIA KWENYE DIMBWI LA MAJI YA MVUA NA KUFARIKI BAADA YA KUSHTULIWA NA HONI YA GARI

Picture

Wananchi pichani wanaonekana wakiwa na huzuni wakati wa zoezi la kuokoa mwili wa marehemu aliyefariki kutokana na kuingia katika eneo la kijitoupele akienda skuli asubuhi leo wakati mvua ikinyesha na kusababisha ajali hiyo.
Inataarifiwa kuwa watoto hao walikuwa wawili wakipita eneo hilo  na kushitushwa na honi ya gari ya daladala iliokuwa ikiwapita, ndipo ikabidi kusogea pembeni. Watoto wale wawili wakateleza katika  eneo hilo. Mmoja wao alijitahidi kutoka na kutaka kumuokoa mwezake lakini akashindwa kutokana na nguvu ya maji yaliokuwa yakipita katika mtaro huo unaokatiza barabara.


Jitihada za wananchi zilishindikana kuuopoa mwili huo uliokuwa umeganda katika mtaro huo na kikosi cha zimamoto wakachukua jitihada za kuchimba sehemu ya pili ya barabara hiyo na kuupata

Picture

Wananchi wakiangalia sehemu uliotolewa mwili wa Mwanafunzi wa Darasa la Kwanza wa skuli ya Kijitoupele , baada ya kuteleza na kuingia katika mtaro wa maji na huku mvua ikinyesha na kusababisha kuchukuliwa na maji na kuvutwa katika mtaro huo na kusababisha kifo chake, wakati akienda skuli asubuhi leo.na Picha ya chini ni eneo aliloteleza na kuingia katika mtaro huo katika eneo hilo wananchi wakiangalia baada ya kutolewa.

Picture

Gari la Wagongwa la Kikosi cha Uokozi Zanzibar likiondoka sehemu ya tukio baada ya kufanikiwa kuupata mwili wa mwanafunzi wa darasa la kwanza wa skuli ya Kijitoupele, baada ya kuteleza na kuingia katika mtaro huo ulioko katika barabara ya kwenda fuoni eneo la Kijitoupele Zanzibar.

Picture

HABARI KWA HISANI YA MAASINDA BLOG

WATEJA WATAHADHARISHWA WIZI WA MITANDAO YA SIMU

02 af8ba

Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Mtondoo akitoa hutuba wakati wa Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Kanda ya Mashariki  iliyofanyika katika Wilaya yake ya Mafia,semina hiyo ilikuwa na  lengo la kutoa elimu  kwa wannchi wa Wilaya hiyo juu ya Haki na wajibu wa watumiaji wa huduma za Mawasiliano, katikati ni Mkurugenzi wa Watumiaji na watoa huduma za Mawasiliano Dk. Raymond Mfungahema,(Kulia ) Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mohamed Kimbule.


 

MAMLAKA ya Mawasiliano nchini, kanda  ya mashariki imetoa rai kwa watumiaji wa mitandao ya  simu za mkononi  kuwa macho na wizi unaofanywa na watu wenye  nia ya kujipatia fedha kwa njia ya  udanganyifu, ambapo  idadi kubwa ya wateja wa  simu wamejikuta wakilalamikia  wizi huo.

Mojawapo mwa udanganyifu ni pamoja na mmiliki wa simu kutumiwa ujumbe unahitaji kutuma fedha kwa ajili ya kulipia gharama za huduma kwa njia mtandao ili hali anayetumiwa fedha  hizo hafahamiki.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Watumiaji na watoa huduma za Mawasiliano Dk. Raymond Mfungahema wakati alipokuwa akitoa mada  ya kazi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)   kwa viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mfia waliohudhuria katika Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Masharaiki

 Afisa Utumishi Mkuu,Esuvatie Masinga katika  Semina   ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Kanda  ya Mashariki, iliyofanyika kisiwani Mafia.

Semina  hiyo iliyofanyika Machi 7a mwaka huu  iliwashirikisha wadau mbalimbalimbali wa mawasiliano  wilayani Mafia, wakiwemo watendaji wa  serikali  wa ngazi ya kitongoji, kata na tarafa na wilaya.

Katika semina hiyo iliyohudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya Mafia, Sauda Mtondoo ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi,Masinga  alisema, wizi wa mitandao ya simu ni changamoto iliyo mbele ya wateja ambayo inaweza ikakabiliwa kama kila mmoja atakuwa na ufahamu  wa kubaini  ujanja na mbinu  zinazofanywa na wajanja wachache.

Alisema ili kukabiliana na mbinu na ujanja wa wachache hao, wamiliki wa simu za mkononi wanatakiwa kuwa macho ujumbe wowote  unaozungumzia  utumaji wa fedha iwe kwa njia ya ujumbe mfupi ama mawasiliano ya moja kwa ya simu wa watu wasiowajua.

Amesema,wateja wengi wamekuwa wakitumiwa  ujumbe unaowataka watume fedha kwa watu wasiowajuwa  wakiamini kuwa wanatuma fedha hizo kwa makampuni ya  simu, jambo ambalo si kweli, kwani makampuni yote ya  simu yana namba zao za utambulisho  pindi wanapoendesha zoezi lolote la kihalali.

"Utakuta mmiliki wa simu ya mkononi  anatumiwa ujumbe  unaomtaka atume kiasi cha fedha kwa mtu asiyemjua, huku asitambue anatuma  fedha  hizo kwa ajili ya kulipia  huduma gani. Hili ni tatizo lililo katika  changamoto inayohitaji wateja kubaini aina hii ya wizi  kwa njia ya mitandao ya simu" alisema Masinga.

Alisema, wateja wa simu wana wajibu wa kubaini ujanja wa watu wachache kwa kutilia mashaka ujumbe ama simu  yoyote inayoelekezwa kwao na inayohitaji  fedha kwa kuchukua  hatua ya kuwasiliana na makampuni ya  simu  husika kubaini kama kuna kuna mahitaji ya namna hiyo.

Katika  hotuba yake, Mkuu wa Wilaya Mafia, Sauda Mtondoo aliiomba  TCRA kutilia mkazo suala la uelimishaji  umma pindi  kunapotokea changamoto  za matumizi ya huduma mbalimbali zilizo chini ya mamlaka  ili kuwaongezea uelewa watumiaji.

Alisema, elimu  kwa umma juu ya huduma ngeni inawasaidia kuwaondolea usumbufu wateja  hivyo kwenda na kasi ya utandawazi na kuwaondolea usumbufu  ambao unaweza ukawapa mwanya wajanja  wachache kunufaika.

Aidha alipongeza  hatua ya TCRA kutoa elimu ya matumizi ya ving'amuzi kwa muda mwafaka, jambo lililosaidia  kuwaondolea wateja usumbufu pindi mamlaka hiyo ilipotangaza hatua ya Tanzania  kuacha kuanza kutumia  mfumo wa  kidijitali kwa baadhi ya mikoa  nchini.

"Ni jambo la kufurahisha kwamba TCRA imetoa elimu  kwa umma kuhusu namna ya kuweka antena hizo ili picha ziweze kuonekana  katika maana halisi ya dijitali.Vilevile  faraja kusikia kuwa mamlaka inawasiliana na  watoa  huduma za kurusha matangazo ya dijitali ili waweke vizuri mitambo yao na kuongeza mitambo kule ambako haipo ili matangazo yawafikie watazamaji wengi" ilisema Mkuu  huyo wa wilaya.

Pia aliitaka mamlaka kuyabana makampuni ya mawasiliano ya simu  inayobuni utaratibu wa kujipatia fedha kwa njia za kuwataka watumiaji wa simu za mkononi kuingia katika utumaji wa  fedha kwa njia ya ujumbe mfupi ili hali huduma hiyo siyo lazika kwa wateja.

Alisema hatua ya watumiaji kukatwa fedha kwa  huduma isiyo  ya lazima humuongezea mzigo  mteja na kuwayafaidisha makampuni ya simu jambo  linazua manung’uniko  yasiyo  ya lazima.

Aliitaja mfano wa huduma  hizo za kuchangia fedha ni pamoja na nyimbo za miito ya simu ambayo haina ulazima kwa mteja hivyo kuwaagiza wachangie  bila ridhaa ya  mteja wa simu ya mkononi ni hatua  inayowaongezea mzigo wamiliki wa  simu  za mkononi.

Kwa upande mwingine washiriki wa semina hiyo walipata mafunzo ya mfumo wa anuani za makazi na Posta Kodi iliyotolewa na Patrice Lumumba  ambaye aliwataka wananchi wa wialya hiyo kuwa makini na kujua anuni za makazi yao.

HABARI KWA HISANI YA MJENGWA BLOG

AFDB WASAIDIA MAJI ZANZIBARIKatibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto) akibadilishana hati na  Mwakilishi wa AfDB nchini Tonia Kandiero mara baada ya kusaini makubaliano leo jijini Dar es salaam ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wa kuipatia Tanzania shilingi bilioni 34.8 za kusaidia mradi wa maji Zanzibar.Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto) na  Mwakilishi wa AfDB nchini Tonia Kandiero wakisaini makubaliano leo jijini Dar es salaam ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wa kuipatia Tanzania shilingi bilioni 34.8 za kusaidia mradi wa maji Zanzibar.

HABARI KWA HISANI YA MJENGWA BLOG

meza ya magazeti leo jumanne

 

j 002 8605d

j 003 1e2be

j 004 d346e

j 005 0230d

j 006 bcb23

 

 

j 007 58e98

j 008 dd7b0

 

j 009 e6134

 

j 010 236a0

j 001 437c5