Wednesday, July 31, 2013

SIMBA YASAJILI MWINGINE.SOMA HAPA





Wekundu wa Msimbazi Simba leo wamekamilisha usajili wa mshambuliaji Betram Mwombeki aliyekuwa anasoma Marekani.

      Mshambuliaji huyo alikuwa kwenye majaribio kwa wekundu hao ambao amefaulu na kupewa mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia timu hiyo na ameusaini mbele ya kaimu makamu mwenyekiti Joseph Itangáre Kinesi.

        Mwombeki mwenye mwili mkubwa anakumbukwa kwa kutupia bao kwenye mchezo wa kirafiki ambao wekundu hao wa Msimbazi walicheza dhidi ya URA kwenye uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.

        Simba wanaendelea kuimarisha kikosi chao na safu ya ushambuliaji ikiwa tayari pia imemsajili mshambuliaji kutoka Burundi Hamissi Tambwe.

KINACHOENDELEA UCHAGUZI WA ZIMBABWE


Wapiga kura Zimbabwe

         Raia wa Zimbabwe wanapiga kura katika uchaguzi wa Urais unaotajwa kuwa na ushindani mkali huku kukiwa na madai ya udanganyifu. Rais Robert Mugabe wa miaka 89 amesema atang'atuka ikiwa yeye na chama chake cha Zanu-PF watashindwa.

           Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai na chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) wamelalamikia Zanu-PF kwa kuhitilafiana na utaratibu wa uchaguzi ili kunyakua ushindi, lakini chama tawala kimekanusha madai hayo.Shughuli za kampeini zimekua ghasia zozote huku kukiwa na visa vichache sana vya kuwatisha wapiga kura.


           Vyama vya Zanu-PF na MDC viliunda serikali ya muungano mwaka wa 2008 baada ya muafaka wa kumaliza ghasia za baada ya uchaguzi kufuatia matokeo ya Urais yaliyozua utata. Bw.Tsvangirai alishinda awamu ya kwanza, lakini akajiondoa kwa raundi ya pili akilalamikia mashambulizi yaliyolenga wafuasi wake.

      Serikali ya Zimbabwe imewapiga marufuku waangalizi wa magharibi kuchunguza uchaguzi wa leo. Hata hivyo Muungano wa Afrika{AU}, Kanda ya Kusini mwa Afrika{SADC} na makundi ya kijamii nchini Zimbabwe yamekubaliwa kufuatilia jinsi uchaguzi utakavyoendeshwa.

        Watu milioni 6.4 wamejiandikisha kupiga kura hii, na maelfu walijitokeza kwenye kampeini za uchaguzi. Matokeo yanatarajiwa kutolewa kwa siku tano zijazo.Mwandishi wa BBC aliyeko Harare amesema kuna foleni ndefu katika vituo vya kupigia kura leo ikiwa siku ya mapumzoko kuhakikisha raia wanapata nafasi ya kuamua serikali mpya.

            Mshindi wa moja kwa moja sharti apate asili mia 50 ya kura zote kutangazwa Rais. Ikiwa hakuna mgombea atapata kura hizo, raundi ya pili imepangwa kufanyika Septemba 11. Uchaguzi huu ndio wa kwanza kufanyika Zimbabwe chini ya katiba mpya iliyopitishwa mnamo mwezi Machi mwaka huu.

SOURCE BBC SWAHILI

BREAKING NEWZZ---TCRA YATANGAZA RASMI KUZITAMBUA BLOG KAMA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA

BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WA BLOG NA VYOMBO VINGINE VYA HABARI VILIVYOHUDHURIA KATIKA WARSHA HIYO MAPEMA LEO ILIYOKUWA INAHUSU MATUMIZI MAZURI YA MITANDAO YA MAWASILIANO


MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA TCRA PR NKOMA AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI NA WAMILIKI WA BLOG LEO KUHUSU KAMPENI HIYO YA KUHAMASISHA MATUMIZI MAZURI YA MAWASILIANO

          MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA TCRA IMETANGAZA RASMI KUZITAMBUA BLOG KAMA VYOMBO VYA HABARI NCHINI KUTOKANA NA MCHANGO WAKE MKUBWA KATIKA MASWLA YA HABARI KWA SASA 

              HAYO YAMESEMWA NA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA HIYO PR NKOMA WAKATI WA WARSHA FUPI YA KUHAMASISHA MATUMIZI MAZURI YA MAWASILIANO NCHINI AMBAPO AMESEMA SECTA HIYO IMEKUWA KWA HARAKA SANA KITU AMBACHO KINAONYESHA KUWA NI NJIA NZURI ZAIDI YA KUPATA HABARI NCHINI KWA SASA

            AIDHA MAMLAKA HIYO IMEAHIDI KUWAKUTANISHA WAMILIKI WA BLOG NCHINI KWA LENGO LA KUWAPA SEMINA JUU YA MATUMIZI MAZURI YA BLOG ZAO NA JINSI GANI YA KUTAMBULIKA ZAIDI.

MSANII MRISHO MPOTO NAYE ALIKUWEPO KWANI AMETUNGA WIMBO MAALUMU WA KUHAMASISHA MATUMIZI MAZURI YA MAWASILIANO AMBAO AMESHIRIKIANA NA BANANA ZORO


Tuesday, July 30, 2013

TAARIFA KWA UMMA----NAFASI ZA KAZI ZILIZOTANGAZWA LEO JULY 30


TUNAOMBA RADHI HAUTOWEZA KUAPLY KUPITIA HAPA TEMBELEA WEBSIT YA WIZARA HUSIKA

Business Relationship Manager-SME-(One Post)
Tanzania Postal Bank (TPB)
Main Purpose of the Job

 Directly work with customers to deepen and secure new business relationships through the analyses of needs and provision of products and services.
Creatively tailor products to meet individual customer needs. Responsible for the growth of quality Business loans portfolio

Analyses and reviews quality of potential and existing business to ensure maximum profitability. Maintain accurate and up-to-date records of all actual and attempted customer interactions.
Conduct customer meetings that have defined call objectives, desired outcomes and a well-constructed plan.

Provide feedback to senior management, marketing and product management on customer's needs and the efficiency of marketing strategies and tactics.
Liaise and provide leadership in areas of expertise, particularly in the provision of products and services to customers.

Application Instructions:

CLICK HERE TO APPLY

Deadline: Aug 12, 2013

Manager Information System Officer 
Azania Bank Limited 
Tasks and Responsibilities
-Administer existing enterprise database system (Oracle), troubleshooting database problems and report anomalies to the seniors for corrective measures.
-Ensure that all database backups prescribed' in database backup 'procedures are adhered to.
-Monitor ATM connection status with Umoja Switch network' and attend any IT related ATM operations issue on day to day basis.
-Perform daily end user support and troubleshooting user problems in relation to applications used in the Bank
-Update operating system patches and authorized configuration changes
-Install and configure new hardware and software as per delegated authority
-Take part in running End of Day I Beginning of Day programs as per agreed timetable.
-Monitor status of bank's CCTV systems and ensuring that the bank is inforf!1ed on their current status at all the times.
Application Instructions:

CLICK HERE TO APPLY

Deadline : None

General Support Officer 
SNV Tanzania
Main Responsibilities
· Record financial transactions in ledger system
· Prepare and check monthly, quarterly and annual financial accounts
· Forecasts and project depletion for submission to the Finance Officer
· Follow up on receipts and payments
· Reconcile bank balances and manage liquidity levels, based on guidelines of the Finance Officer and Financial procedures
· Take care of petty cash and supplier payment
· Correction account for SNV Accounts and accruals for all prepayments costs
How to apply?

CLICK HERE TO APPLY

Deadline: Monday, August 12, 2013

Retail Sales Manager
Oil Gas Industry
Duties & Responsibilities
1.Provides overall supervision to the activities and employees of the Retail Sales Department and assigned region.
2. Strategic Planning
Prepares a strategic sales plan for the assigned region and sends to the General Manager for negotiation and approval.
Monitors trends in the market and recommends adjustments as required.
3. Annual Sales Planning
Develops and obtains approval for the annual sales plan for the assigned region.
This includes discussion and negotiation of quantity, the nature of various schemes the staff incentive policy, marketing budgets, resources and manpower.
Prepares forecast for products.
Application Process

CLICK HERE TO APPLY

Deadline : 8 August 2013.

Head of Monitoring and Training 
National Bank of Commerce
Deadline : 11th, August 2013

Construction supervisor 
The International Rescue Committee (IRC)
Deadline : Aug 2nd, 2013

Customer Service Officers 
Azania Bank Limited
Deadline : None

Insurance Officer 
Azania Bank Limited
Deadline : None
Business Performance Analyst
Azania Bank Limited
Deadline : None

Credit Officers
Azania Bank Limited
Deadline : None

Branch Operations Executive 
Azania Bank Limited
Deadline : None

Accounts Officer 
Azania Bank Limited
Deadline : None

CHADEMA YAPATA UGENI KUTOKA ULAYA,YAWAELEZA MAUAJI YALIYOTOKEA HAPA NCHIN

MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA WA VYAMA VYA DEMOCRASIA DUNIAN BW ARIS KALAFATIS AKIWA NA KATIBU WA BARAZA LA VIJANA LA CHAMA CHA DEMOCRASIA NA MAENDELEO  CHADEMA LEO WAKATI WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA UGENI HUO 

        CHAMA CHA DEMOCRASIA CHADEMA KIMEPATA UGENI WA WATU ZAIDI YA 33 KUTOKA UMOJA WA VIJANA WA VYAMA VYA DEMOCRASIA DUNIANI AMBAO AMBAO WALIKUTANA NA VIONGOZI WA VIJANA WA CHADEMA KUJADILI MAMBO MBALIMBALI IKIWEMO MWENENDO WA DEMOCRASIA YA TANZANIA PAMOJA NA MAMBO AMBAYO YANAKIKUMBA CHAM HICHO HAPA TANZANIA

            AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM LEO MWENYEKITI WA CHAMA HICHO AMBACHO KINAJUMUISHA NCHI MBALIMBALI ZIKIWEMO HISPANIA NA UJERUMANI AMESEMA KUWA WAMEKAA NA VIONGOZI WA CHADEMA NA KUELEZWA MAMBO MBALIMBALI YANAYOJITOKEZA HAPA TANZANIA IKIWEMO UKANDAMIZWAJI WA DEMOCRASIA NA MAUAJI YA WANAHABARI NA WANAHARAKATI JAMBO AMBALO AMEEMA KUWA LIMEANZA KUKIDHIRI HAPA NCHINI


Monday, July 29, 2013

KAMISHNA KOVA AREJEA KWA HARI MPYA ATANGAZA KULIFANYA JIJI LA DAR KUWA KAMA HONGKONG,ATAMBULISHA MAKAMANDA WAPYA

BAADHI YA PEMBE ZA NDOVU ZILIZOKAMATWA NA JESHI HILO

KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM S KOVA AKIONYESHA BAADHI YA NYARA ZA SERIKALI AMBAZO JESHI HILO LIMEFANUKIWA KUKAMATA KATIKA OPERATION ZAKE JIJINI DAR ES SALAAM

JESHI LA POLISI PIA LIMEFANIKIWA KUKAMATA LUNDO LA FUNGUO BANDIA AMBAZO HUTUMIKA NA WAALIFU KATIKA KUFANYA UJAMBAZI

             BAADA YA KUTOKUWEPO NCHINI KWA MUDA KIDOGO KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM  ALIYEKUWA KATIKA ZIARA NCHINI MAREKANI AMEREJEA KWA KASI MPYA NA KUWATANGAZIA WAALIFU WOTE KUWA MUDA WAO UMETIMIA NA SASA JIJI LA DAR LITAFANA NA LILE LA HONGKONG

             AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO KOVA AMESEMA KUWA ZIARA YAKE HIYO ILIKUWA YA KUJIFUNZA JINSI NCHI ZA WENZETU WANAVYOWEZA KULINDA MAJIJI YAO NA KUSEMA AMEKUJA NA MAUJIZI KIBAO YA KULILINDA JIJI LA DAR.

           KAMANDA KOVA PIA AMETUMIA NAFASI HIYO KUWATAMBULISHA ASKARI WAPYA WA JESHI HILO WALIOMALIZA MAFUNZO YAO AMBAO WATAFANYA JIJI KATIKA KANDA HIYO
HAWA NIA ASKARI WAPYA WA JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM AMBAO KOVA AMEWATAMBLISHA LEO RASMI KUENDELEZZA JIHUDI ZA KUFANYA JIJI LA DAR ES SALAAM KUWA NA AMANI


WAANDISHI WA HABARI WA BLOG WAZALILISHWA HIVI POLISI LEO NA MWANDISHI MWENZAO

MTOA KAULI

            WAANDISHI WA HABARI WA MATUKIO MBALIMBALI TANZANIA WANAOJISHUHULISHA KATIKA KUANDIKA HABARI  KATIKA MITANDAO MBALI  NIKIMAANISHA BLOG NA WEBSITES AMBAO NDIO SORCE KUBWA SANA YA HABARI KWA SASA LEO WAMEJIKUTA KATIKA WAKATI MGUMU SANA BAADA YA KUZALILISHWA NA KUAMBIWA KUWA TAALUMA YAO HAITAMBULIKI KATIKA TAALUMA YA UANDISHI WA HABARI TANZANIA
            
            SAKATA HILO AMBALO LIMEZUA UGOMVI MKUBWA LIMETOKEA MAPEMA LEO JIJINI DA ES SALAAM MAKAO MAKUU YA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM AMBAPO KAMA KAWAIDA YA KAMISHNA WA POLISI KANDAMAALUM ANA DESTURI YA KUTOA MATUKIO YA JESHI LA POLISI YALIYOJIRI KWA WIKI NZIMA
        
              WAANDISHI WA HABARI TULIKUSANYIKA KWA WINGI AKIWEMO MMLIKI WA BLOG HII YA HABARI24 NA WAANDISHI WA HABARI KUTOKA VYOMBO MBALIMBALI TANZANIA KWA LENGO LA KUMSIKILIZA KAMISHNA KOVA ANA JAMBO GANI KWA WATANZANIA NDIPO KIZAA HICHO KILIPOIBUKA 
            
            MMOJA KATI YA WAANDISHI WA HABARI ANAYETAMBULIKA KWA JINA LA KHAMIS MPIGA PICHA WA KITUO CHA CHANEL TEN ALIAMUA KUFANYA UZALILISHAJI HUO KWA KUANZA KUTOA KAULI MBAYA NA AMBAZO WENGI WALIZIONA NI CHAFU NA HAZIFAI NA KUFIKA MBALI KWA KUSEMA KUWA HAO SIO WAANDISHI WA HABARI NI WEZI TU.
          
             NAOMBA NINUKUU MANENO YA BW HUYO KHAMIC hakuna waandishi wa habari wa blog,hwatambuliki,hawajasoma,hawana taaluma,na hawaruhusiwi kuwa hapa.HADI SASA MTANDAO HUU HAUJAJUA CHEO CHAKE KATIKA JESHI LA POLISI HADI KUFIKIA KUWAAMBIA WAANDISHI WA HABARI MAMBO KAMA HAYO 
                    
        MTANDAO HUU UNATAKA YAFUATAYO YAFANYIKE,MTOA KAULI AFUTE KAULI ZAKE ZOTE ALIZOTOA ZA KUWADHALILISHA WAANDISHI WA HABARI,NA PIA MMILIKI WA MTANDAO HUU AMBAYE NI MHITIMU WA DIPLOMA YA UANDISHI WA HABARI NA SASA ANASUBIRI MUDA AKACHUKUE DIGREE YAKE ANAMUOMBA MHUSIKA KUTOKA JESHI LA POLISI AWAOMBE WAANDISHI HAO WA HABARI RADHI KWA NIABA YA BW KHAMIC AMBAYE WAANDISHI HAO WANADAI HAWAMTAMBUI.

BREAKING NEWZZZ.YAMETIMIA.WAZIRI MKUU PINDA KUPANDISHWA KIZIMBANI ALHAMIC KWA KAULI ZAKE BUNGENI

PASIANCE MLOWE MTAFITI WA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU  AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM


MKURUGENZI UWEZESHAJI NAYE ALIKUWEPO KATIKA MKUTANO HUO

            KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA KIMETANGAZA RASMI KUMPANDISHA MAHAKAMANI SIKU YA ALHAMISI WAZIRI MKUU WA TANZANIA MH MIZENGO PINDA KUFWATIA KAULI YAKE ALIYOITOA BUNGENI MNAMO MWEZI WA SITA KAULI AMBAYO ILIPINGWA NA WATU WENGI SANA

           AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM MKIRUGENZI WA MABORESHO NA UTAFITI BW HAROLD SUNGUSIA AMESEMA KUA UAMUZI HUO UMEKUJA BAADA YA KUONA JUHUDI ZA KUMTAKA WAZIRI PINDA KUWAOMBA WATANZANIA RADHI KUGONGA MWAMBA KITU AMBACHO AMESEMA KUWA NI KITENDO AMBACHO KIMEASHIRIA KUPANIA.

           BW SUNGUSIA AMESEMA KUWA SIKU YA ALIHAMISI WANAWASILISHA KESI YA KUMSTAKI WAZIRI MKUU KATIKA MAHAKAMA AMBAYO BADO HAWAJAIWEKA WAZI KWA WANAHABARI

          KAMA UTAKUMBUKA WAKATI WA VURUGU ZA ARUSHA NA ZILE ZA MTWARA WAZIRI MKUU AKITOA KAULI KUWA ,ukufanya fujo na umeambiwa usifanye fujo utapigwa tu,na mimi na sema wapigeni maana tumechoka

HABARI 24 BLOG ITAKUWA NA WEWE SIKU YA ALIHAMIC KUKURIPOTIA KESI HIYO

AROLD SUNGUSIA MKURUGENZI WA MABORESHO NA UTAFITI  KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU.


Sunday, July 28, 2013

KONGAMANO LA AMANI DAR--JESHI LATUHUMIWA KUWABAKA KINAMAMA WA MTWARA



     


         WAKATI LEO KUKIWA KUMEFANYIKA KONGAMANO KUBWA SANA LA AMANI JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA CHUO KIKUU KATIKA UKUMBI WA NKURUMA,KONGAMANO HILO LIMEIBUA MAMBO AMBAYO MENGINE KAMA NI KWELI YAMETOKEA BASI NI AIBU KATIKA TAIFA

         AKIZUNGUMZA WAKATI AKICHANGIA KATIKA KONGAMANO HILO NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI CUF  JULIUS MTATIRO  AMELISHUTUMU JESHI LA TANZANIA LILILOKWENDA MTWARA KUIMARISHA ULINZI WAKATI ULE WA MVUTANO WA GESI NA KUDAI KUWA JESHI HILO LIMEENDESHA ZOEZI LA UBAKAJI KWA KINAMAMA WA MKOA HUO KIPINDI KILE CHA VURUGU

         AMESEMA KUWA ANATAMBUA KUWA JESHI LA TANZANIA LINA SIRI NYINGI SANA JUU YA HAYO ILA ANA USHAHIDI WA KUTOSHA KUWA JESHI HILO LILIFANYA UCHAFU HUO NA CHAMA CHAKE KILIKUTANA NA MAMA AMBAYE ALIFANYIWA KITENDO HICHO NA DACTARI KUDHIBITISHA KUBAKWA KWA MAMA HUYO JAMBO AMBALO LIMEPINGWA VIKALI NA MWAKILISHI WA JESHI HILO ALIYEHUDHURIA KATIKA KONGAMANO HILO

          AIDHA KABLA YA BW MTATIRO KUTOA TUHUMA HIZO NAYE KATIBU MKUU WA CHADEMA MH DK SLAA AMBAYE NAYE ALIHUDHURIA WAKATI AKICHANGIA AMELITUPIA LAWAMA JESHI LA POLISI NA MAJESHI MENGINE KWA KUENDESHA VITENDO VYA KIHUNI KATIKA VURUGU ZA MTWARA NA KUWAASA KUACHAMARAMOJA MAMBO HAYO KWANI NI UONEVU WA WAZI KWA WANANCHI,HUKU AKISEMA   KUWA ANA USHAHIDI WA MAMBO AMBAYO ANAYAZUNGUMZA.

KATIKA KONGAMANO HILO LILIHUDHURIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA KISIASA PAMOJA NA WA SERIKALI AMBAPO KATIKA SERIKALI ILIWAKILISHWA NA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MH NCHIMBI AMBAPO WAKATI AKIFUNGA KONGAMANO HILO AMEKANUSHA TAARIFA HIZO ZA JESHI KUWABAKA BAADHI YA WANAWAKE WA MTWARA NA KUSEMA KUWA YEYE NDIYE WAZIRI HUSIKA NA HANA TAARIFA KAMA HIZO NA HAJAWAHI KUSEMA KITU HICHO NA KUWATAKA WATANZANIA KUTISIKILIZA MAMBO YANAYOSEMWA BALI WAFANYE UTAFITI WA MAMBO HAYO

MH  NCHIMBI AMEUPONGEZA UONGOZI WA UDASA KWA KUANDAA MDAHALO HUO AMBAO PIA AMESEMA USIWE MWISHO BALI UWE NI MWANZO ILI WATANZANIA WAPATE NAFASI YA KUIJADILI AMANI YAO MIAKA HAMSINI IJAYO

COSTAL UNION YAITAFUNA SIMBA JIONI HII MKWAKWANI


          BAO pekee la kiungo wa kimataifa wa Kenya, Crispin Odula, jioni hii limeipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba SC ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa nyumbani, Mkwakwani, Tanga. 

              Huo unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Coastal inayofundishwa na Mzanzibari, Hemed Morocco kwenye Uwanja wa nyumbani, baada ya Jumatano kuifunga 1-0 URA ya Uganda, bao pekee la mshambuliaji mpya kutoka Polisi Morogoro, Kenneth Masumbuko.

           Kwa Simba SC, iliyo chini ya mwalimu mkongwe, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ hicho ni kipigo cha pili mfululizo, baada ya wiki iliyopita kufungwa 2-1 na URA Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

            Katika mchezo wa leo uliovuta mashabiki wengi uwanjani, Coastal ilipata bao lake hilo pekee dakika ya 53 baada ya kuipasua vizuri ngome ya Simba SC, iliyoongozwa na beki kutoka Afrika Kusini, Vincent Mabusela.
Simba SC ilipata nafasi mbili ambazo ilishindwa kuzitumia, moja Sino Augustino alipiga shuti kali likagonga mwamba baada ya Wekundu wa Msimbazi kufanya shambulizi la kushitukiza- na Abdulhalim Humud ‘Gaucho’ dakika ya 16 naye aliipasua ngome ya Coastal, lakini akapiga shuti kali juu ya lango.

           Zahor Pazi aliisumbua mno ngome ya Coastal alipoingia kuchukua nafasi ya Sino kipindi cha pili, lakini hakuweza kufunga tu.
Kikosi cha Coastal Union leo kilikuwa; Shaaban Kado, Mbwana Bakari/Hamad Hamisi dk84, Othman Omary, Juma Nyosso, Marcus Ndahele, Jerry Santo, Uhuru Suleiman/Abdi Banda dk73, Crispin Odula/Suleiman Kassim ‘Selembe’ dk54, Keneth Masumbuko, Haruna Moshi ‘Boban’ na Danny Lyanga.
Simba SC; Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Rahim Juma, Vincent Mabusela/Miraj Adam dk78, Jonas Mkude, Said Ndemla/Marcel Kaheza dk 25, Abdulhalim Humud, Sino Augustino/Zahor Pazi dk46, Ramadhan Chombo ‘Redondo’ na Ramadhani Singano ‘Messi’/Twaha Shekuwe.

CHANZO: BIN ZUBEIRY

Saturday, July 27, 2013

PICHA JINSI STARS ILIVYOCHEZEA KICHAPO JANA HUKO UGANDA.TANZANIA 1 UGANDA 3

TAIFA STARS IKIINGIA UWANJANI
KIKOSI CHA UGANDA

AMRI KIEMBA NA NGASA WAKIFURAHIA BAO LAO MOJA JANA

HAWA NI MASHABIKI WALIOJITOA KWENDA UGANDA KUISAPOT TANZANIA ILA TUKAPIGWA 3 KWA MOJA



HABARI ZOTE KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI ZINAPATIKANA HAPA



DSC 0003 f899b
DSC 0004 b0bd0
DSC 0005 72034
DSC 0007 f447f

DSC 0008 32219
DSC 0010 8e31b
DSC 0011 658d7
DSC 0012 8f10e
DSC 0013 e36e4
DSC 0014 a0a80
DSC 0015 78c0d
DSC 0016 a6882
DSC 0017 b77a2
DSC 0018 0e097

MTANZANIA AZINDUA KITABU CHAKE CHA MASHAIRI KWA AJILI YA SHULE ZETU,WATANZANIA WATAKIWA KUMPA USHIRIKIANO,MENGI NAYE APONDA MFUMO WA ELIMU TANZANIA

                    C.E.O WA CAMARA EDUCATION TANZANIA AMBAYO NI TAASISI INAYOJISHUGHULISHA NA UTOAJI WA MAFUNZO YA ICT,KUTOA PIA VIFAA VYA COMPUTER,NA PIA OFFLINE WIKIPEDIA ANAITWA EDNA HOGAN AMBAYE NDIYE ALIYETUNGA KITABU HIKI CHA MASHAIRI

              BI EDNA ANASEM KUWA DHUMUNI LAKE KUBWA LA KUTUNGA MASHAIRI HAYO NA KUYASAMBAZA KATIKA MASHULE NI BAADA YA KUONA WATANZANIA WENGI HAWANA MUAMKO WA KUSOMA VITABU NDIPO ALIPOONA NI BORA AKAANZA KATIKA MASHULE MBALIMBALI HAPA TANZANIA ILI WAWEZE UFAIDI MASHAIRI HAYO

            ANASEMA KUWA HAKUWA NA LENGO LA KUJA KUWA MYUNZI WA MASHAIRI ILA ALIJIKUTA ANAFANYA HIVYO BAADA YA KILA SIKU KATIKA MAISHA YAKE YAKE YA KAWAIDA KUKUTANA NA MAMBO AMBAYO ALIBIDI AWE ANAANDIKA MASHAIRI NA MWISHO WA SIKU KUONA NI BORA AKATOA KITABU HICHO

              DADA HUYO AMBAYE WENGI WAMEMUITA SHUJAA NI MOJA KATI YA MASHUJAA WA TANZANIA KWA SASA KWANI KUTUNGA KITABU CHA MASHAIRI NA KUFANIKIWA KIKIPELEKA MASHULENI SIO KAZI NDOGO.

           ANASEMA KUWA LENGO LAKE NI KUHAKIKISHA KUWA KITABU HICHO KINAFIKA SEHEMU KUBWA YA TANZANIA IKIWEMO VIJIJINI NA SEHEMU NYINGINE,HUKU AKITOA SHUKRANI ZAKE KWA SERIKALI NA WADAU WA ELIMU WALIVYOMPA USHIRIKIANO HADI KUFANIKISHA ADHMA YAKE HIYO

ANATOA WITO KWA VIJANA WA KITANZANIA KUJIJENGEA TAMADUNI YA KUSOMA VITABU KAMA NCHI ZA WENZETU KWANI VITABU VINAELIMISHA SANA NA NI JAMBO NZURI KUSOMA VITABU

PROFESA ULIMWENGU ALIKUWA NI MOJA KATI YA WASOMI WALIOVUTIWA SANA NA KITABU HICHO NA KUJA KUMPA USHIRIKIANO MWANADADA HUYO JANA KATIKA HAFLA FUPI YA UZINDUZI WA KITABU HICHO AMBACHO YEYE AMEKIELEZEA KAMA MTUNZI WAKE BI EDNA NI MTU AMBAYE ANA MOYO WA KUDHUBUTU NA ATAFIKA MBALI KWA JITIHADA ZAKE HIZO ALIZOZIONYESHA


BAADA YA MGENI RASMI KUWASILI KATIKA UKUMBI AMBAO ULIFANYIKA HAFLA HIYO

BW MENGI AKITOA MACHACHE
KATIKA UZINDUZI HUO MH MENGI ALIUTUMIA PIA KUTOA MAONI YAKE JUU YA ELIMU YA TANZANIA N A MWENENDO WAKE KWA SASA AMBAPO MH MENGI ALIONYESHA WASIWASI WAKE KATIKA UTOAJI WA ELIMU YA TANANZANIA,MH MENGI ANASEMA KUWA HAIWEZEKANI ELIMU YA TANZANIA KUWA MWALIMU AKIFELI NDIO ANAWEZA KWENDA KUSOMA UALIMU JAMBO AMBALO AMESEMA KUWA HALIMJENGI MTANZANIA AMA MWANAFUNZI BALI LINASHUSHA ELIMU YA TANZANIA KWA SANA

UZINDUZI RASMI WA KITABU HICHO ULIFANYWA NA MH REGNAD MENGI MWENYEKITI MTENDAJI WA MAKAMPUNI YA IPP AMBAPOKWENYE PICHA HAPO ANAONEKANA AKIWA NA C.E.O WA CAMARA EDUCATION TANZANIA WAKINYANYUA KITABU HICHO ISHARA YA UZINDUZI RASMI

KATIKA HAFLA HIYO PIA ULIFANYIKA MCHANGO WA PAPO KWA HAPO ILI KUHAKIKISHA KITABU HICHO KINAFIKA MBALI AMBAPO MH MENGI ALICHANGIA ZAIDI YA MILION 50 NA KUAHIDI KITABU HICHO KIENDE KATIKA SHULE ZAIDI YA 31 ZIKIWEMO ZA MKOANI KILIMANJARO

CHADEMA YAENDELEA KUPINGA KODI ZA SIMU,MNYIKA ATOA NAMBA YA CHENGE CHANIKA LEO ASEMA WATANZANIA WAMPIGIE WAMUHOJI,

WANANCHI WA JIMBO LA UKONGA WAKIWA WANASIKILIZA KWA UMAKINI YALE YALIYOKUWA YANAENDELEA KATIKA MKUTANO HUO WA ADHARA ULIOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA CHANIKA JIJINI DAR ES SALAAM 


PEOPLEEESS POWER NDIO JAMBO LILILOKUWA LINAENDELEA HAPA WANANCHI WAKIONYESHA MAPENZI YA CHAMA CHAO

MABERE MARANDO AKIWASILI VIWANJANI HAPO MAPEMA KUWAHUTUBIA WANANCHI HAO


GRACE SHELUKINDO VITI MAALUM PIA ALIKUWEPO NAYE ALIPATA NAFASI YA KUZUNGUMZA NA WANACHAMA HAO NA KUWATAKA KUTOKATA TAMAA KWANI USHINDI WA CHAMA HICHO UPO KARIBU NA WAJIANDAE KUPOKEA USHINDI

         CHAMA CHA DEMOCRASIA NA MAENDELEO CHADEMA KIMEENDELEA KUPINGA VIKALI KANUNI YA TOZO YA KODI ZA SIMU ILIYOTANGAZWA NA SERIKALI NA KUTAKIWA KILA MWENYE SIMU KILIPIA SHILINGI ELFU MOJA.
           AKIZUNGUMZA LEO KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA KATIKA JIMBO LA UKONGA KATIKA VIWANJA VYA STENDI YA UKONGA MBUNGE WA UBUNGO KWA TIKETI YA CHAMA HICHO MH JOHN MNYIKA AMESEMA KUWA KAMWE CHAMA CHAKE HAKIWEZI KUKUBALI TOZO HIYO AMBAYO NI MZIGO MKUBWA KWA WANANCHI
            MH MNYIKA KATIKA KILE AMBACHO KIMEONEKANA NI KITU CHA TOFAUTI AMETOA NAMBA YA SIMU YA MH ENDRU CHENGE KWA MAMIA YA WANANCHI KATIKA MKUTANO HUO ILI WAMPIGIE NA KUMUULIZA KWANINI ANAUNGA MKONO KODI HIYO
         AMESEMA KUWA SIO KITU CHA AJABU KUTOA NAMBA HIYO KWANI KAMA YEYE NI KIONGOZI WA WANANCHI LAZIMA WANANCHI WAWE NA NAMBA YALE HIYO
            KATIKA MKUTANO HUO PIA ULIHUDHURIWA NA VIONGOZI KADHAA WA KAMATI KUU YA CHAMA HICHO AKIWEMO MH MABERE MARANDO

VIJANA WA RED BREGADE WAKIWA KAZINI KUHAKIKISHA KUWA ULINZI WA VIONGOZI NA WANACHAMA HAO UPO SAWA KABISA,HIKI NDIO KIKUNDI AMBACHO KIMEKUWA KIKIPINGWA SANA HIVI KARIBUNI NA BAADHI YA VIONGOZI WA SERIKALI AKIWEMO MWENYEKITI WA CCM KWA KILE WANACHODAI KITAVUNJA AMANI


MH MNYIKA AKIWAHUTUBIA WANANCHI HAO NA KUWATAKA KUTOKUOGOPA KWA LOLOTE SASA NA KUSONGA MBELE,HUKU AKISISITIZA KUWA KODI YA SIMU IMEPITISHWA NA VIONGOZI WA CCM NA SIO BUNGE NZIMA HIVYO WATAENDELEA KUIPINGA HADI MWISHO


HAPA SASA AKAAMUA KUWEKA WAZI NAMBA YA MH CHENGE NA KUWAAGIZA WANACHAMA HAO KUMPIGIA NA KUMUULIZA KWANINI KAPITISHA TOZO ZA LAINI ZA SIMU