Thursday, October 31, 2013

KUWA WA KWANZA KUONA VIWANGO VIPYA VYA UFAULU WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE NA SITA,ZIRO YAFUTWA SASA NI DV 5

KATIBU MKUU WA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI BW PR SIFUN MCHOME AKIIZUNGUMZA NA WANAHABARI
Jedwali Na 1
MUUNDO WA ALAMA NA UFAULU
ALAMA
UWIGO WA ALAMA
IDADI YA ALAMA
TAFSIRI
A
75 - 100
26
Ufauli Uliojipambanua
B+
60 - 74
15
Ufaulu bora sana
B
50- 59
10
Ufaulu mzuri sana
C
40 - 49
10
Ufaulu mzuri
D
30 - 39
10
Ufaulu Hafifu
E
20 - 29
10
Ufaulu hafifu sana
F
0 - 19
20
Ufaulu usioridhisha

Kwa aina hii ya muundo wa alama, na kwa kuwa muundo wa GPA utaanza kuandaliwa na wadau kuelimishwa kabla haujaanza kutumika, katika kipindi hiki mpaka wakati huo, muundo wa madaraja utakuwa kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 2 hapa chini.
Jedwali Na 2
MUUNDO WA MADARAJA
MUUNDO WA ZAMANI
MUUNDO MPYA
MAELEZO
POINTI
DARAJA
POINTI
DARAJA
7-17
1
7-17
I
Kundi la ufaulu uliojipambanua na bora sana
18-21
II
18-24
II
Kundi la ufaulu mzuri sana
22-25
III
25-31
III
Kundi la ufaulu mzuri na wa wastani
26-33
IV
32-47
IV
Kundi ufaulu hafifu
34-35
0
48-49
V
Kundi la ufaulu usioridhisha

Wataalamu wa mifumo ya mitihani watalifanyia kazi zaidi jedwali hili la madaraja ili liweze kutumika kwa ufanisi katika kipindi hiki cha mpito.
Kwa mantiki hii, Daraja Sifuri linafutwa na kuwekwa daraja litakalojulikana kama Daraja la Tano na ambalo litakuwa ndilo la mwisho kabisa katika ufaulu.
          HITIMISHO
Mabadiliko haya yamefanyika ili kuendelea kuimarisha mfumo wetu wa elimu na kuweka wazi taratibu mbalimbali kwa ajili ya mitihani na masuala mengine. Yako mambo mengi mengine ambayo hayana budi kuendelea kuimarishwa ikiwemo mfumo wa mitaala, walimu, mazingira ya kujifunzia na kufundishia pamoja na vitabu na vifaa vingine muhimu katika elimu. Masuala haya yanaendelea kuangaliwa kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ama Big Results Now (BRN). 
          Ushirikiano wa wadau wote ili kuleta tija kwenye elimu ni muhimu sana na hivyo wizara itaendelea kuwashirikisha wadau wote kwa kadri itakavyohitajika na wadau pia wanaombwa wasiache kuishirikisha wizara pale watakapokuwa na jambo lolote ambalo linahitaji ushirikiano ili kwa pamoja tuweze kupata mafanikio katika sekta ya elimu.

Imetolewa,

KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDINBC YAJIPANGA KUBORESHA HUDUMA ZAKE

AFISA MAHUSIANO WA NBC EDDIE MHINA AKIMTAMBULISHA MKURUGENZI HUYO KWA WANAHABARI
        Benki ya NBC imeelezea dhamira yake ya kutaka kuwafurahusha wateja kwa huduma zake nzuri ikiwa ni pamoja na kuondoa kwero mbalimbali ambazo zinaikabili benki hiyo

          Akizungumza na wanahabari leo jijini dar es salaam katika benki hiyo wakati akifunga wiki ya huduma kwa mteja katika benki hiyo mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo MIZINGA MELU amesema kuwa wamejipanga kukuza na kupanua huduma zake kwa njia mbalimbali jambo litakalowafanya wadeja kuipenda na kuifurahia benki hiyo.

          Kuhusu swala la foleni kubwa katika benki hiyo ambalo limekuwa likilalamikiwa na wateja wengi mkurugenzi huyo amesema kuwa kwa sasa wameanzisha huduma ya mobile bank ambayo amesema kuwa inaweza kuwa ni suluhisho katika tatizo hilo
MKURUGENZI HUYO ALIPATA NAFASI YA KUZUNGUMZA NA WATEJA MBALIMBALI WALIOKUWA WANAPATA HUDUMA KATIKA BENK HIYO

UKIINGIA MLANGONI EWE MTEJA UNAKUTANA NA CHAI SAAFIIMKURUGENZI MTENDAJI WA BENK HIYO MIZINGA MELU AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI
WATEJA KARIBUNIMKURUGENZI HUYO LEO ALIAMUA KUINGIA KAZINI NA KUWASIKILIZA WATEJA WAKE MWENYEWE

Wednesday, October 30, 2013

BREAKING NEWZ KUTOKA ARUSHA--MAUAJI

Mama mmoja  amepigwa risasi na polisi  kujeruhiwa  vibaya  maeneo ya mapato arusha.chanzo cha  tukio hilo kinasema kwamba mama huyo alifika maeneo hayo na kupaki gari yake akitaka kuingia bank lakini akaambiwa eneo hilo halifai kupaki gari.Mama huyo alipaki gari na kuingia bank alipotoka alikuta gari lake limetolewa upepo na ndipo vurugu ilianzaa baina yake yeye na polisi.       

        Vurugu ilipokuwa kubwa mama huyo aliwaambia polisi kwamba wasimtishie bunduki hata yeye anayo na alipotaka kuitoa polisi wakampiga risasi.Mama huyo ni muuzaji maarufu wa madini  jijini arusha.Mama huyo amekimbizwa hospitali na yupo chumba cha upasuaji.CHANZO CLOUDS FM