Na Karoli Vinsent
CHAMA cha democrasia na maendeleo nchini “Chadema’
kimetishia kutoshiriki Uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 kama endapo Tume ya
Uchaguzi nchini haitofanya marekebisho kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura.ENDELEA HAPO--------
Hayo,yalisemwa leo na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe
wakati akizungumza na Waandishi wa Habari makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar
es Salaam,ambapo alisema Chama hicho kimeamua kufanya maamuzi hayo kutokana na
Tume hiyo kuwanyima Fursa vijana katika chaguzi mbalimbali hapa nchini.
“Tunaiambia Tume ya uchaguzi Nchini endapo hawatalifanyia
Marekebisho Daftari hili sisi hatutashiriki uchaguzi mkuu mwakani ili kuonyesha
chadema tunauchungu juu ya vijana ambao wanakosa fursa ya kupiga kura kwani
chadema tulifanya sensa tukabaini vijana Milioni tano wanakosa nafasi ya kupiga
kura kutokana na kutofanyiwa marekebisho Daftari hili”alisema mbowe
Mbowe ambaye
ni Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na pia ni Mbunge wa jimbo la Hai kwa
tiketi ya Chama hicho alisema kitendo cha tume hiyo kusema haina fedha huko ni
kuwadanganya Wananchi
“Sheria inasema wazi kabla ya uchaguzi kufika lazima Daftari
hilo lifanyiwe marekebisho ili kuwapa nafasi vijana waliofikisha umri wa kupiga
kura waweze kushiriki au hata wale waliopoteza kwa bahati mbaya kadi zao za
kupigia kura waweze kusaidiwa lakini leo tume hiyo inasema haina fedha,Chadema
tunasema huu ni ubabaishaji”alisema Mbowe
Katika hatua nyingine Chama hicho kimenzindua Ziara ya nchi
nzima kwa lengo la kukijenga chama hicho.
“Chadema tumeanza ziara ya Nchi nzima ili tuwafikia wananchi
popote walipo ili kuwapa ujumbe pamoja na kuwashirikisha na kuwapa nafasi
katika kujadiri matatizo yanayowakuta huko walipo kwenye sehemu zao za
kuishi”alizidi kufafanua Mbowe
Ziara hiyo
itachukua wiki tatu ambapo chama hicho kimesema kitatumia usafiri wa Ndege
pamoja na usafiri wa Bahari pamoja na nchi kavu kwa lengo la kuwafikia Wanachi
popote walipo.
Kuhusu Katiba mpya
Kuhusu katiba mpya Mwenyekiti huyo wa Chadema
ilikitadhaharisha Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na wabunge wake kuwa chadema
hawatokubali kutumia katiba ya zamani kwenye uchaguzi ujao
“Nasema chadema hatutakubali kurudishwa nyuma kwenye katiba
ya Zamani eti kwa hoja ya Wabunge wachache wa CCM pamoja na mwenyekiti wao,kwa
maslai yao binafsi na sisi Chadema tunasema hatutokubali kurudi nyuma na ili
tutumie katiba ya zamani” alisema Mbowe
Mbowe,alisema Maelezo ya Jaji Walioba yanaonyesha jinsi gani
wananchi wanataka katiba mpya.
No comments:
Post a Comment