Tuesday, January 7, 2014

HAYA SASA KUTEKWA NA KUPIGWA KWA MWENYEKITI WA CHADEMA TEMEKE,CHADEMA WENYEWE WATAJWA KUHUSIKA,KISA ANAMSHABIKIA ZITTO,KOVA AAPA KUWAKAMATA WOTE


 Karoli Vinsent       

        CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimeingia kwenye kashfa nzito baada ya kuhusishwa kwenye utekaji wa Mwenyekiti wa Chadema  wilaya ya Temeke Joseph Yona.
Taharifa toka ndani ya jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amapo mwandishi wa mtandao huu amezipata baada ya kuthibitishwa na Kamisha wa kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova Mbele ya Waandishi wa Habari leo
ENDELEA HAPO-----------



     Zinasema Jeshi hilo la polisi linafanyia uchunguzi wa kina kuhusu tukio la kutekwa nyara ,kupigwa na kujeruhiwa na hatimaye kutupwa vichakani dhidi  ya mtu anaitwa Joseph Yona miaka 32 mkazi wa Temeke mtoni kwa Azizi Ally.Taharifa hiyo inasema ni mwenyekiti wa chadema  wilaya ya Temeke ambaye pia ni Mtaalam wa Maabara chuo cha Elimu (DUCE) kilichopo Changombe.

       Vilevile  taharifa hiyo inafafanua  mnamo tarehe 7 mwezi huu saa 5 usiku eneo la Union ,mlalaamikaji huyo alienda kuaomba msaada  kwa mlinzi wa kampuni binafsi aitwaye Ismail Swalehe ili aende kituo cha polisi kuripoti.Ndipo milinzi huyo alikubali na kumpeleka kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Union,ndipo mwenyekiti huyo ndipo alipowasiliana na mkuu wa polisi kawe  ambaye alifika eneo la tukio hilo akifuatana na Rpc wa kinondoni Acp Camilius Wambura.

         Maofisa wa Polisi walimuhoji Mlalamikaji Kuhusu Majeraha aliyonayo usoni ba sehemu mbalimbali.Ndipo mlalamikajia aliweza kujieleza ndipo akasema yeye ni mkazi kwa Azizi Ally wilaya ya Temeke na kwamba ilpofika saa 5.Kamili usiki ya tarehe 6 mwezi huu alikuwa akipata kinywaji katika Grocery ya Mgumbini akiwa na wenzake watatu walikuwa wakimalizia Vinywaji.Ghafla walitokea watu sita ambao walimtaka aende nao walijitambulisha kuwa wao ni maofisa wa Polisi katika kituo cha kati.

       Ndipo  katika watu hao sita aliweza kumtambua mtu mmoja kuwa ni mwanachama mwenzake wa chadema na alipojalibu kuulizia kuhusu huyo mtu walimwingiza ndani  ya Gari aina Land Cruiser na kufunga kitambaa usoni na kuondoka naye.

      Katika hatua nyingine mlalamikaji alizidi kusema waliomteka walianza kumhoji ni kwa nini anaendelea kumshabikia Zitto Kabwe wakati ni  mtu anayeharibu chama chao yaani chadema.pili  walimtaka akawaonyeshe rafiki yake ambaye anajulikana kwa jina  Habibu Mchange.ndipo walizidi kumpiga mpka wakampelekea majeraha kwenye jicho na kichwani.

         Uchunguzi wa awali unaonyesha wazi kuwa tukio hili lina uhusiano wa moja kwa moja na mgogoro unaoendelea katika chama cha siasa cha chadema juu ya Zitto kabwe na wenzake.Aidha kabla ya tukio hili,mlalamikaji alikuwa anapokea simu nyingi za vitisho kutoka kwa viongozi  wa ngazi mbalimbali  wa Chadema ambao anadai anawafahamu.

          Vilevile Taharifa hiyo inasema Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam  limeanza uchunguzi wa sakata hilo
Uchunguzi wa mwandishi wa mtandao huu umebaini nkuwa Habibu Mchange ni miongoni mwa watu wanaosakwa sana na wanasiasa kutokana na kuhusika katika mipango ya kukihujumu chama hicho.

        Wachambuzi wa masuala ya mambo ya kisiasa waliozungumza na mtandao huu wanasema siasa za Tanzania zimekuwa hazistawi kutokana na wanasiasa wa vyama  vikuu vya upinzani kuwa na tamaa za pesa na kujionyesha kuwa wanashabikia upande mmoja wasiasa

No comments: