Saturday, January 4, 2014

HII NDIO FUJO YA JANA MAHAKAMA KUU KATI YA WAFUASI WA ZITTO NA WALE WA CHADEMA

 
Dar es Salaam,Tanzania

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeahirisha kutoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa jana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe (Chadema), kuhusu ombi la kuitaka Mahakama hiyo kuizuia Kamati Kuu ya Chama hicho, kutomjadili katika kikao ambacho kilipangwa kufanyika leo jijini Dar es Salaam.





Wanachama wa Chadema, wakitwangana nje ya Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam. 

Jaji John Utumwa alisitisha kutoa hukumu hiyo mpaka siku ya Jumatatu saa 4:00 asubuhi.Hata hiyo baada ya Jaji huyo kuahirisha kesi hiyo, nje ya Mahakama hiyo kulikuwa na vurugu kubwa baada ya kundi linalo unga mkono maamuzi ya Chadema kutwangana na kundi linalo muunga Zitto Kabwe.

 

Mwanachama wa Chadema, anayepinga hoja za Zitto Kabwe, akimtwanga mfuasi wa Zitto Kabwe. 

Hatua hiyo ilisababisha Askari wa Jeshi la Polisi kuingilia kati, huku wakiungana na upande wa Chadema na kuwatwanga marundi wafuasi wa Zitto waliokuwa na mambango kama ilivyokuwa kwa wenzao wa Chadema.

Kesi hiyo ilifunguliwa juzi na wakili wa Mbunge huyo Albert Msando huku wakili wa Chadema Tundu Lissu akiweka pingamizi,hata hivyo Jaji John Utumwa wa Mahakama hiyo alitupilia mbali mapingamizi yote yaliyowekwa na Tundu Lissu,

No comments: