Friday, January 17, 2014

KAMPENI ZA UDIWANI,CHADEMA YAANZA KINYOOONGEE,WANACHAMA WACHACHE WAJITOKEZA

PICHA NYINGINE CHINI----------

Wananchi  wakiwa  katika mkutano wa kampeni za chadema kata ya Nduli, Iringa, leo

Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa  (kushoto) akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Nduli Ayub Mwemba  leo wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa Chadema
Sehemu ya  wananchi  waliofika katika mkutano  huo

Na Francis Godwin Blog 
       
         IKIWA ni  siku  mbili  toka  katibu  wa chama  cha mapinduzi (CCM) wilaya ya  Iringa Hassan Mtenga  kumwagiza  mstahiki meya  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Aman Mwamwindi  kufuatilia kero  mbili za  wananchi ikiwemo ya wagonjwa  kukosa dawa katika Hospital ya  mkoa na kujua fedha za  ruzuku ya  jimbo la Iringa mjini  ziko  wapi na zinafanya  nini, mbunge  wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa adai kuna  kiasi cha Tsh milioni 30 nyingine  za mfuko wa jimbo.
 Huku mbunge Msigwa akiwaomba radhi  wananchi  wachache  waliofika katika mkutano  huo kwa kudai  kuwa haukutangazwa  vya kutosha  .

Hatua ya  katibu  huyo kuagiza  kufuatilia  fedha  hizo ni baada ya  jimbo  hilo kukabiliwa na changamoto mbali mbali na  fedha  hizo  zinazotolewa na Rais zimelenga  kusukuma maendeleo majimboni ila alihoji kwanini Manispaa ya Iringa fedha  zinakaa bila kazi.

Akizungumza katika mkutano  wake wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Nduli  leo ,Msigwa alisema  kiasi  hicho  cha Tsh 30m zipo hadi  sasa.

“Naomba  kuwahakikishieni nitaendelea  kutafuta  vyanzo  vingine  vya  mapato  ili  kusaidia kero za maji  hapa Nduli ….mimi nasema ukweli namba mnipe Ayub Mwenda nitafanya  nae kazi”

Pia  Mbunge Msigwa amesema  kuwa  katibu  wa CCM Hassan Mtenga si saizi yake  ila  yeye  saizi yake ni akina  waziri  mkuu Mizengo  Pinda,waziri wan chi  ofisi ya  waziri mkuu sera na uratibu wa bunge na mbunge wa ISimani Wiliam Lukuvi na katibu mkuu  wa CCM Bw Kinana na  sio  yeye .

“Nataka  kuwahakikishia kuwa  huyu mimi  si  saizi yangu  saizi  yake ni akina Frank Nyalusi  diwani  wa Mvinjeni  (Chadema) na katibu  mwenzake wa Chadema Iringa mjini  Suazana Mgonakulima.

Wao  wanasema amekuja  kwa ajili ya  kunishughulikia mimi ila nasema njia  aliyojia atatitoka na njia  hiyo hiyo kama  walikuwepo akina Charles Charles na  wametoka zaidi ya makatibu  7  iwe  yeye .

Hata  hivyo katika mkutano  huo ambao idadi ya  watu  ilionekana ni ndogo  zaidi  ukilinganisha na hali halisi  ya  nguvu  ya  Chadema   iliyokuwepo  jimbo la Iringa mjini ,bado  mbunge huyo  alitumia mkutano huo kuwaomba radhi  wananchi kutokana na mahudhurio hayo hafifi kwa madai  haukutangazwa vya  kutosha.

Kampeni  za  uchaguzi  mdogo  wa kata  hiyo ya  Nduli  zimeanza  rasmi leo kwa Chadema  kufungua  pazia  hilo huku wao CCM wanataraji  kuzindua kampeni  hizo katika  eneo hilo la Nduli Januari 26 mwaka huu

Uchaguzi  huo mdogo umekuja  kufuatia kifo cha aliyekuwa  diwani wa kata   hiyo Idd Rashid  Chonanga  aliyefariki  duni kwa ugonjwa mapema mwaka  jana.
Kwa  upande wake  mgombea  udiwani wa Chadema  katika kata  hiyo ya  Nduli Ayub Mwenda  ambae  alipata  kuwa mwenyekiti wa kijiji  cha Nduli kabla ya  CCM kumsimamisha nafasi  hiyo kutokana na kuwa na tuhuma za ubadhilifu  wa fedha  za maendeleo ,alisema  kuwa yeye ana  risiti  za fedha  zote ambazo alikuwa akikusanya na  kuwa kusimamishwa kwake nafasi ya uenyekiti ni uoneu uliofanywa na aliyekuwa katibu wa CCM wilaya  ya Iringa mjini Lusiana Mbosa na  kuwaomba  wananchi  kumkubali  sasa ili awe  diwani wa kata  hiyo.
Wachambuzi  wa masuala ya  kisiasa mjini Iringa  wanadai  kuwa kipimo cha  kukubalika ama kutokukubalika kwa mbunge Msigwa katika jimbo  hilo kwa mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu na mwaka huu katika chaguzi  za  serikali za mitaa ni uchaguzi huo wa kata ya Nduli

No comments: