Thursday, January 16, 2014

MNYIKA KUKUTANA NA WAATHIRIKA WA HIFADHI YA BARABARA YA MOROGORO JUMAPILI HII

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
            Jumapili tarehe 19 Januari 2014, katika ukumbi wa Luguruni Park Makondeko waathrika wa hifadhi ya barabara ya Morogoro watakutana na wabunge wa majimbo matatu nao ni Mhe John Mnyika wa Jimbo la Ubungo, Mhe Selemani Said Jafo wa Jimbo la Kisarawe na Mhe Sylvester Francis Koka wa Jimbo la Kibaha Mjini kuweka mikakati ya kukomesha vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu hususan haki ya makazi ambavyo vimekuwa vikitendwa na Wizara ya Ujenzi na Tanroads dhidi ya wananchi wanaoishi pemezoni mwa barabara ya Morogoro  kati ya Ubungo hadi Tamco Kibaha. Mkutano huo utaanza Saa 8.00 mchana.
ISOME YOTE HAPO----------


    Tanzania imeridhia mikataba ya kimatifa ya haki za binadamu na matamko mbali mbali ya kimataifa vinavyolenga kulinda “Haki za Makazi” za wananchi na kupinga “Uhamishwaji wa Kimabavu” (Forced Eviction),  kama vile “The Charter of the United Nations, the Universal Declaration of Human Rights, the Vienna Declaration and Programme of Action the 1993 World Conference on Human Rights, and the 2005 World Summit Outcome Document, The International Covenant on Economic, Social and Cultural Rights, Habitat II conference in Istanbul and the Earth Summit in Rio, and excerpts from the UN Committee on Economic, Social and Cultural Rights, General Comment No. 4, the UN Commission on Human Rights, Resolution 1993/77, and 24/2008.

  Licha ya Tanzania kuridhia mikataba iliyotajwa hapo juu, Wizara ya Ujenzi na Tanroads wamekuwa kwa muda mrefu sasa wakivunja haki za binadamu za wananchi kwa makusudi kwa  kuingia isivyo halali katika ardhi na makazi ya wananchi walioko nje ya mita 30 kutoka katikati ya barabara ya Morogoro, pande zote mbili kutokea Ubungo hadi Tamco Kibaha, hata baada ya mahakama kuu kitengo cha ardhi kutamka kuwa ardhi hiyo ni mali halali ya wananchi kupitia hukumu yake katika shauri namba 80 la 2005 lililotolewa uamuzi na Jaji S. B. Bongole tarehe 31 Mei 2013.

     Hivi karibuni Desemba 2013, mawaziri wanne wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Mhe Balozi Hamisi Kagasheki, Mhe Emmanuel Nchimbi, Mhe David Mathayo na Mhe Shamsi Vuai Nahodha walilazimika kujiuzuru kufuatia tuhuma za ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu zilizoanishwa katika taarifa ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira.
Asante
Chrizant Kibogoyo
Mwenyekiti

No comments: