Friday, January 3, 2014

MPYAAAA---BANK KUU YA TANZANIA YATOA SARAFU YA SH 50,000/-HII HAPA

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000.
Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alisema jana kuwa sarafu hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa ajili ya kumbukumbu tu na haitaingizwa katika mzunguko wala kutumika kwa kulipia malipo ya aina yoyote.
Sarafu hii imetolewa maalumu kama maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar, haitatumika kwa manunuzi.  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT ilimnukuu Profesa Ndulu akisema sarafu hiyo imetolewa kwa idadi ya vipande 3,000 kwa ajili ya tukio hilo na kuwahimiza wananchi kuinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.


No comments: