Thursday, January 9, 2014

SOMA HISTORIA FUPI YA ERNEST JUMBE MANGU,IGP MPYA WA JESHI LA POLISI TANZANIA



mwanza        IGP Ernest Jumbe Mangu alizaliwa mwaka 1959 mkoani Singida na alipata elimu ya Sekondari katika  Shule ya Tumaini mwaka 1981.
         
      Alijiunga na Jeshi la Polisi katika Chuo cha Polisi Moshi (CCP)  Agosti 17 mwaka 1982 na kuhitimu Juni, mwaka 1983 ambapo alipata mafunzo ya awali ya Polisi.
ENDELEA NAYO HAPO------
 
          
     Mwaka 1987 alipata mafunzo ya sheria kwa ngazi  ya cheti katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Novemba mwaka 1992 alitunukiwa shahada ya kwanza ya sheria (LLB) katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
        
       Juni mwaka 2010, alitunukiwa shahada ya udhamili katika  masuala ya usalama katika Chuo Kikuu Cha Usalama cha Marekani.
         
        Akiwa ndani ya Jeshi la Polisi amepandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Koplo wa  Polisi (1988), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1992), Mkaguzi wa Polisi (1995), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (1997), Mrakibu wa Polisi (2002), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2004), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2006), Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi (2010), Naibu Kamishna wa Polisi (2013) na Kamishna wa Polisi (2013).
       
          Amewahi kufanya kazi Dar es Salaam katika ngazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya (OCCID) na pia Naibu Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mwanza mwaka 1996 akimsaidia Aliyekua RCO wakati huo, Said Mwema. Pia amefanya kazi Dodoma.
          
         Alipoteuliwa kuwa IGP Saidi Mwema alifanya kazi kwa karibu na Mangu akiwa mmoja wa wasaidizi wake muhimu makao mkuu ya Polisi kabla ya hupewa majukumu ya kiuongozi. 
         
         Vilevile kamanda huyo aliwai kufanya kazi katika kitengo cha ionterpor yaani polisi wa kimataifa

No comments: