Monday, January 20, 2014

TIGO SASA YAJA NA KAMPENI MPYAAA,UKINUNUA LAINI YA 1000 UNARUDISHIWA HELA YAKO.SOMA ZAIDI

MENEJA WA CHAPA WA TIGO AKIZUNGUMZA LEO

Kampuni ya simu za mkononi tanzaniaTIGO katika kuhakikikisha kuwa watanzania wote wanapata huduma za simu kwa bei nafuu sasa imezindua rasmi huduma yake mpya ambao ni utaratibu wa kuwarudishia wateja wake gharama zote za  za manunuzi ya laini za simu kwa kuwapa muda wa maongezi na kuwapa salio katika acount zao za tigo pesa.

    Akizungumza na wananahabari jijini dar es salaam wakati wa uzinduzi wa utaratibu huo maarufu kama RUDISHIWA PESA YAKO  meneja chapa wa kampuni hiyo WILLIAM MPINGA amesema kuwa kuanzia sasa wateja watakaonunua laini za mtandao wa tigo kwa gharama ya shilingi 1000 watapewa muda wa maongezii wa shilingi 500 na kuwekewa salio la 500 katika account zao za tigo pesa.

    Amesema kuwa hii ni wazi kuwa mteja sasa anapewa laini ya tigo bure kabisa bila malipo kwani gharama zake zinarudi zote.ambapo amesema kuwa kampeni hiyo inalenga katika kuwapa fursa watanzania wengi zaidi uwezo wa kupata huduma za mtandao huo ambao kwa sasa umekuwa ukisifiwa sana kwa huduma zake bora na imara.

      MPINGA amesema kuwa kampeni hiyo itatangazwa katika maeneo mbalimbali ikwemo radio na tv kwa lengo la kuwajulisha watanzania wengi zaidi

No comments: