Thursday, January 16, 2014

UREJESHWAJI WA ADA ZA LESEN ZA KIBIASHARA,CHAMA CHA WAFANYABIASHARA WA VIWANDA NA KILIMO WAIJIA JUU SERIKALI,SOMA WALICHOKISEMA



Na Karoli Vinsent
        
         MIEZI michache kupita tangu Serikali itangaze urejeshwaji wa ada ya leseni za kibiashara nchi nzima,Chama cha Wafanya biahara wenye  viwanda na Kilimo  wameitaka serikali kusitisha mpango huo.
         
            Hayo yalisemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama  hicho Dk Piter Chasawilo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake,ambapo alisema utaratibu  ulio tangazwa na Serikali juu ya urejeshwaji wa ada ya leseni na kulipia kila mwaka  utaratibu huo unaenda kinyume na sheria.
ENDELEA HAPA----------

        
            “Utaratibu  huu mpya unaenda na kinyume na sheria ya Leseni ya mwaka 1972 na hasa marekebisho yake ya mwaka 2004 ambayo yaliwezesha  leseni za biashara kutolewa bure na maramoja tu kwa kipindi cha maisha yote ya biashara”alisema Dk Chasawilo
             Dk Chasawilo,alizidi kuongeza kuwa tayali kumekuwepo na malalamiko mengi kwa jumuiya ya wafanyabiashara juu ya urejeshwaji wa ada ya leseni na sekta binafsi inailalamika Serikali kwa kutoishirikisha katika urejeshwaji  wa utaratibu  huu ambao unaiathiri sekta hii moja kwa moja na sekta binafsi inaamini kuwa serikali imelenga kuongeza mapato bila kuzingatia nia ya urasimishaji wa sekta isiyo lasmi ilikuarakisha maedereo ya uchumi kwa ujumla.
            
         Aidha,Dk Chasawilo alisemahakuna muongozo uliotolewa na serikali kuelekeza namna maombi ya leseni yatakavyo shugulikiwa.na kusema hii inatoa mwanya kwa maofisa husika kuongeza usumbufu kwa wafanyabiashara  watakapotaka leseni hizo.na vilevile kuongeza urasimu kufanya Biashara kwani mfanyabiashara  atalazimika kupia mlolongo wa utaratibu kila mwaka
            
           Katika hatua nyingine chama hicho kimezindua utaratibu mpya ambao  utakuwa ni wa ujumbe mfupi  yaani (SMS MOBILE SYSTEM) ambapo lengo kubwa ni kuwashirikisha wadau ili kuweza kuishawishi serikali kwa kutumia takwimu sahihi  juu ya madhara yanayotokana  na urejeshwaji wa ada hii ya leseni

No comments: