Monday, January 20, 2014

VITUKO KIAPO KWA MAWAZIRI WATEULE WA JK MMOJA ACHEMKA KUAPA

Huyu  ndie  naibu  waziri wa elimu na mafunzo ya  ufundi Jenista Mhagama  aliyepasha  wakati wa kula kiapo leo 

naibu  waziri wa fedha Bw Mwigulu Nchemba  ambae  ametinga kula kiapo na jezi za Taifa

VIOJA mbali mbali  vimejitokeza wakati wa mawaziri  wateule wa Rais Dr Jakaya  Kikwete  wakila  kiapo baada ya  naibu  waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi mbunge wa Peramiho mkoani Ruvuma Jenista Mhagama  kulazimika  kula  kiapo  kurudia  kiapo mara tatu tofauti na  wenzake ambao  waliapa mara mbili kutokana na  naibu waziri  huyo kuchemka mara ya  kwanza mbele ya Kikwete .

Mbali ya Mhagama  kuchemka na kuingia katika  rekodi ya kurudia kiapo mara tatu pia naibu katubu mkuu wa CCM ambae ni naibu waziri wa fedha Bw Nchemba yeye  alitinga katika viwanja  hivyo  huku akiwa kawaida na  jezi  za timu ya Taifa tofauti na wengine ambao  walifika  wakiwa  wameulamba  suti vikali .


Hata   hivyo  wapembuzi wa mambo  wanadai  kuwa  kuchemka kwa Mhagama  katika zoezi hilo ni kutokana na kutokuwa na imani kama angeteuliwa  kuingia kushika nafasi hiyo  nyeti na  unaibu  uwaziri 

No comments: