Sunday, January 5, 2014

WALIOPENDEKEZWA NA CHADEMA ILI WATEULIWE NA RAISI BUNGE LA KATIBA



    Kamati Kuu CHADEMA leo kimewapendekeza Prof Abdallah Safari, Mabere Marando,Nasra Juma Baruan na Method Kimomogolo ili wateuliwe na Rais Bunge la Katiba.
 
   Professor Abdallah Safari ni mwanasheria nguli wa chama hicho na pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani.Huku Method Kimomogolo ni mwanasheria maarufu wa Chama hicho ambaye ameongoza kesi nyingi zilizokwishafunguliwa dhidi ya Chadema na viongozi wake.
 
     Wasifu wa Mabere Marando kila mtu anaujua kwani ni nguli aliyeongoza Mageuzi Tanzania tokea kabla ya mfumo wa vyama vingi.Kwa sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu Chadema na ni mmoja wa wanasheria wake huku akiwa pia Makamu Mkiti wa Chadema Kanda ya Pwani.

       Rais anatarajiwa kuteua majina mawili tu kutoka Chadema na kwa mujibu wa sheria ni sharti katika wateuliwa hao mmoja atoke Zanzibar na pia lazima mmoja awe mwanamke.

No comments: