Saturday, January 11, 2014

YANGA NOMA,YAANZA MAZOEZI UTURUKI YAKUTANA NA ROBETO CARLOS,YAPIGA NAE PICHA


 
HABARI KAMILI-------------
Mara baada ya kuwasili salama jana jioni katika hoteli ya Sueno Beach Side eneo la Manavgat pembezoni kidogo ya jiji la Antalya nchini Uturuki, kikosi cha klabu bingwa nchini Tanzania bara Young Africans leo asubuhi kimeanza mazoezi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu pamoja na mashindano ya kimataifa barani Afrika.

Yanga iliwasili huko majira ya saa 11:00 jioni kwa saa za huko ikiwa ni sawa na saa 12 kwa saa za Afrika Mashariki na moja kwa moja kikosi kilielekea katika mji wa Manavgat ambapo ndipo ilipo hoteli ya Sueno Beach Side ambapo msafara mzima umefikia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumiwa Rockersports na afisa habari wa klabu hiyo Baraka Kizuguto, amsema hoteli hiyo ya Sueno Hotel Beach Side ni hoteli kubwa yenye hadhi ya nyota tano, ambayo ina jumla ya vyumba 760, mabwawa ya kuogelea,viwanja viwili vya mpira vya mazoezi kimoja kikiwa na nyasi za kawaida na kingine nyasi za bandia.

Kocha msaidizi wa Young Africans Charles Boniface Mkwasa amesema anashukuru kikosi chake kimefika salama na wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri kiafya na kifikra hivyo anatarajiwa mazoezi yatakayoanza leo yatasaidia kuiweka timu katika hali nzuri na kuwa tayari kwa mashindano.

"Kazi yangu kubwa ni kukiandaa kikosi kiwe katika hali nzuri ili pindi tutakaporejea nchini timu iwe fiti na tayari kwa ajili ya mashindano, kwa hali ilivyo nzuri na mazingira naamini timu itabadilika na kurejea nchini ikiwa katika kiwango cha kizuri cha ushindani" alisema Mkwasa

Young Africans inatarajia kucheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya timu ya Ankara Sekerspor iliyopo Ligi Daraja la Kwanza nchini Uturuki.

Aidha timu ya Sivasspor iliyopo Ligi Kuu nchini Uturuki inayonolewa na mchezaji wa zamani Real Madrid na timu ya Taifa ya Brazil Roberto Carlos pia imeweka kambi katika hoteli ya Sueno na leo asubuhi kabla ya Young Africans kuanza mazoezi waliweza kupiga picha ya pamoja na gwiji huyo.

No comments: