BREAKING NEWZZZ---TANZANIA YASHTAKIWA MAHAKAMA YA KIMATAIFA ICC,NI KUTOKANA NA KAULI YA RAISI NA ILE YA PINDA BUNGENI

MKURUGENZI WA KITUO HIKO DEUS KIBAMBA AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI


   Na Karoli Vinsent
           
         KAULI aliyopata kuitoa Waziri Mkuu Mizengo Pinda bungeni kuwataka polisi wawapige wapinzani, na kauli ya juzi ya Rais Jakaya Kikwete kuwaagiza wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wajibu mapigo pale wanaposhambuliwa na wapinzani, imeelezwa kuliingiza taifa vitani,
             
      Nacho Kituo Cha taarifa kwa Wananchi (TCIB)kimeanza mawasiliano na Mwendesha Mastaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya uharifu dhidi ya Binadamu(ICC) Bi Fatou Bensouda kumwomba atume timu ya wataalamu wake kuja Tanzania kufanyia  Uchunguzi na Tathmini kuhusu kauli hizo iliwaweze kuifungulia mashtaka Serikali ya Tanzania.
         
         Hayo,yasemwa Leo,jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kituo hicho, Deus Kibamba wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo alisema wameamua kufanya Maamuzi hayo kwa kuona Amani ya nchi inaanza kutoweka kutokana na viongozi kutoa matamshi yanayochochoe  uvunjifu wa amani.
ENDELEA HAPA----------

        “Tumeamua kuchukua hatua hii kufanya mawasiliano na Mwendesha Mastaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya uharifu dhidi ya Binadamu(ICC) Bi Fatou Bensouda baada ya kuwa na hofu kuwa tukiachi matamshi”
    
      “ haya  yaendelee,kunaweza kutokea fujo kubwa na kupelekea mauaji ya ajabu huko tunapoelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,leo kiongozi mkubwa kama Rais anatoa kauli hizi tena mbaya,hivi anafikiria wakati anatoa kauli hizi,leo anafikiri amani hii ikivunjika yeye nani atabaki hapa”alisema Kibamba
     
     Kibamba ambaye ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Nchini alisema Taifa la Tanzania litaingia kwenye machafuko kwani nchi ya Jirani ya Kenya dalili zake zilikuwa kama za Tanzania.
    
        “Mimi kwenye uchaguzi wa Kenya wa Mwaka 2007 nilikuwepo na Dalili za machafuko zilitokana na viongozi kama hawa kutoa kauli za kukashifu na katoa amasa kwa wananchi kulipiza kisasi,leo hawo greengurd wakishambulia redgurd au redgurd wakiwashambulia Greengurd kunamtu atapona,manaake amani ya nchi ndio inavunjika hapo”alisema Kibamba.
        
       Ikumbukwe tamko la Kibamba limekuja kutokana na kauli ya Rais kikwete, wakati  Akifungua mkutano wa NEC ya CCM juzi mjini Dodoma, Rais Kikwete aliwataka wanachama wa chama hicho kuacha unyonge kwani uvumilivu waliokuwa nao umefika kikomo chake.
         
      Alisema chama hicho kinaingia kwenye uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kalenga mkoani Iringa, kinashindana na vyama vingine ambavyo alisema ni wagomvi, maana kwao ugomvi ndiyo sehemu ya mwongozo wa kufanya kazi ya siasa.
      
     “Tulizungumza nalo hilo kwenye Kamati Kuu, tulikubaliana kuacha unyonge. Ndiyo, kwenye Kamati Kuu tumekubaliana, tumesema jamani watu wote waende wakaseme tumekubaliana kuacha unyonge,” alisema huku akicheka na kupigiwa makofi na wajumbe wa NEC.
   
       Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, alitolea mfano wa tukio lilitokea Kahama mkoani Shinyanga, ambapo kijana mmoja alitolewa macho kwa bisibisi, na tukio la Igunga ambapo kijana mmoja alimwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.
     
      “Acheni unyonge na hata katika taarifa ya habari leo (jana) mtoe hivyo hivyo. Na muache habari zote mseme hii tu (waandishi wa habari). Uvumilivu una ukomo wake,” alisema huku wajumbe wakiendelea kumpigia makofi.
     
      “Nalisema kwa sababu yanayotokea yanasikitisha sana. Pale Igunga kijana yule wamemmwagia tindikali, pale Kahama kijana ametolewa macho kwa bisibisi,” alisema.
     
       Uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga lililopo mkoani Iringa unatarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu, huku tayari vyama vya CCM na CHADEMA vikiwa vimetaja wagombea wao.
       
       Katika hatua nyingine kituo hicho cha kuwasemea wananchi kimezengumzia uchaguzi mdogo wa madiwani kata 27 na kusema uchaguzi huo ulikuwa na kasoro nyingi sana ikiwemo idadi ndogo ya wapiga kura pamoja vitendo vya utekaji pamoja na utesaji walivyokuwa wanafanyiwa wagombe na wapiga kura.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.