Tuesday, February 11, 2014

BUNGE LA KATIBA--TUNDU LISU APINGA UTEUZI WAKE,ASHANGAA MAGAZETI YANAYOPOTOSHA KUHUSU POSHO YA WABUNGE HAO


Na Karoli Vinsent


      SIKU chache Baada Rais Jakaya Kikwete kutangaza majina ya wajumbe wa Bunge la Katiba,Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimepinga uteuzi huo na kusema uwezekano wa kupata katiba mpya upo shakani kutokana na kuwepo na wabunge wa katiba wasiokuwa na Sifa katika bunge hilo.

       Hayo,yalisemwa Leo wakati wa mahojiano kati ya Mwandishi wa Mtandao huu na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu kuhusu msimamo wa chama hicho kuhusu Uteuzi huo ,ambapo alisema uteuzi huo umejaa ubabaishaji mkubwa.

       “Ikulu kujaza watu wao kwenye bunge la katiba, tumeona CCM wamekuwa na wajumbe wengi kuliko vyama vingine vya kisiasa  na Taasisi zingine,na sisi Chadema tulisema tangu mwanzo endapo tukimwachia Rais ateuwe wajumbe wa katiba ni kupelekea kupata katiba ya kibabaishaji”
ENDELEA HAPA--------


      “ Hao walioteuliwa kila anayezungumza  anasema asante Rais kwa kuniteua,hii ni dalili tosha hao wajumbe ni watu wa Rais,na bunge limejaa watu wa Rais,na kwa mpango huo hilo sio bunge la katiba mpya”alisema Lissu
Tundu Lissu ambaye ni Mbunge wa Singinda Mashariki CHADEMA  na Vilevile ni miongoni mwa Wajumbe watakao kuwepo kwenye Bunge hilo la Katiba linalotalajiwa kuanza Jumatatu ijayo,alisema atapambana katika bunge hilo la katiba na kuhakikisha katiba inayopatikana iwe ya wananchi na sio ya wanasiasa.

       “Tutapambana mpaka mwisho tuhakikishe katiba inayopatikana  iwe ya Wananchi na sio ya wanasiasana kama ikishindikana tutajitoa katika bunge hilo na Tutawashirikisha wananchi”alisema Lissu
Kuhusu Posho kuwa kubwa kwa wajumbe wa Bunge la Katiba mpya

       Tundu Lissu alisema hao wanaandika hivyo watakuwa wanapotosha Umma,
“Malipo ya wabunge yanaamuliwa na Rais na Sheria inasema hivyo,na Rais anafanya hivyo kwa kutumia walaka na inatakiwa itolewe walaka kwenda kwa wabunge wa Katiba na hao wanaoandika hivyo wameona huo walaka?hata mimi sijaona huo walaka wala sijapata”.


          Ikumbukwe Gazeti la Tanzania Daima Toleo la Februari 10 mwaka huu lilsema kila mbunge wa Bunge la Katiba atapata milioni 49 kwa siku 70 yaani kila siku mbunge wa Katiba anapata laki saba kwa siku.taharifa hiyo imepingwa na viongozi na kusema sio ya kweli.

No comments: