Wednesday, February 12, 2014

BUNGE MAALUM LA KATIBA,JUKWAA LA KATIBA LATOA TAMKO KALI LA KUKOSOA UTEUZI,SOMA HAPA



MJUMBE WA KAMATI YA UONGOZI YA JUKWAA LA KATIBA NDUGU HEBRON MWAKAGENDA AKITOA TAMKO HILO LEO MBELE YA WAANDISHI WA HABARI

                                       TAARIFA KWA UMMA

        JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tumeendelea kufuatilia mchakato wa kuandikakatiba mpya ya Tanzania kwa umakini mkubwa tangu mchakato huu ulipoanzishwarasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 31 Disemba 2010.

             Katika kufuatilia mchakato wa kuandika katiba mpya JUKWAA LA KATIBATANZANIA tumekuwa na utaratibu wa kutoa tarifa kwa Umma kuhusu uendeshajiwa zoezi hili ambalo ni la muhimu sana kwa watanzania wote bila kujali itikadi, rangi,umri, jinsia, kazi wala elimu. Lengo la kutoa taarifa kwa umma ni katika kukuza demokrasia na kuongeza ushiriki wa wananchi kwenye mchakato wa kuandika
katiba mpya.

           Mchakato wa katiba kwa sasa unaelekea kwenye hatua ya bunge maalaum la katibaambalo Rais ameliitisha na linategemea kuanza vikao vyake mnamo tareheJumanne 18/02/2014 mjini Dodoma. JUKWAA LA KATIBA TANZANIA linapenda kutoa tarifa kwa Umma juu ya mambo yafuatayo;
ENDELEA KUSOMA TAMKO HILO------


                       1. RASIMU YA PILI YA KATIBA
JUKWAA LA KATIBA TANZANIA linapenda kuipongeza Tume ya Mabadiliko yaKatiba kwa kutoa rasimu ya pili ya katiba yenye mwanzo mzuri kwa kuingiza baadhiya mawazo ya wananchi kama yalivyokua yanatolewa wakati wa ukusanyaji maonina wakati wa kujadili rasimu ya kwanza ya katiba kwenye mabaraza ya katiba.

           Rasimu ya pili ya katiba iliyokabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya   Muungano tarehe 30/12/2013 ndiyo itakayojadiliwa kwenye bunge maalum la katiba wakati wa vikao vyake Dodoma. Hii imeonyesha jinsi Tume ilivyokuwa sikivu na
kuwapa wananchi kile wanachoona kinawafaa katika Katiba mpya kwa kuzingatia maoni na michango mbalimbali waliyoitoa kwa Tume.

     2. SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA SURA 83 TOLEO LA MWAKA 2012

 Lilikuwa ni wazo jema na zuri kwa Serikali kuandika katiba katiba mpya kwa kuongozwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, 2012 ili usimamizi uwe wa uwazi zaidi na madhubuti. Ingawa sheria hii imeshafanyiwa marekebisho mara mbili, JUKWAA LA KATIBA TANZANIA bado limeendelea kubaini upungufu katika sheria
hii hata kwa kipindi hiki cha uteuzi wa wabunge 201 ambao sio wabunge wa kawaida wala sio wajumbe wa baraza la wawakilishi. Sheria hii imempatia Rais wa Jamhuri wa Muungano mamlaka ya kuteua wabunge 201 kutoka makundi kama walivyobainishwa kwenye sheria na ilivyotangazwa kwenye gazeti la serikali la
tarehe 07/02/2014.

      Kutokana na sheria hii kuminya demokrasia ya wananchi kuchagua wajumbe wao moja kwa moja kwenye bunge maalumu la katiba, iliyataka makundi haya kupendekeza idadi ya wajumbe 4-9 ili Rais aweze kuchangua wale atakaoona wanafaa kuwa wajumbe wa bunge maalum la katiba. JUKWAA LA KATIBA tulipaza sauti kupinga sheria hii, na tunaendelea kupaza sauti kuwa sheria hii imedumaza demokrasia na kufifisha matarajio ya watanzania walio wengi. Kutokana na ubovu
wa sheria hii, Rais amapewa madaraka ambayo kidemokrasia yalipaswa yaachwe mikononi mwa wananchi wenyewe.

          Hivyo basi, JUKWAA LA KATIBA TANZANIA  limebaini baadhi ya upungufu kwenye baadhi ya makundi katika upatikanaji wa wajumbe 201 waliotangazwa hivi karibuni; Kwanza, Katika kundi la taasisi zisizokuwa za kiserikali (20), Kutokana na sheria hii kuwa kandamizi Rais ameteua baadhi ya wajumbe katika kundi hili ambao JUKWAA KATIBA TANZANIA linaamini kuwa hawakupaswa kuwepo kwenye kundi hili kwa kuwa kwa namna moja au nyingine sio wadau katika sekta hii au kwa upande  mwingine inaonekana wazi hawawakilishi mawazo ya sekta hii kama ifuatavyo;
     
      Watu watano (5) kati ya watu 20 hawajulikani kabisa kwenye sekta hii.

      1. Ndugu Kingunge Ngombale Mwiru- huyu ni kada mkongwe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na waziri mstaafu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano.  Kwa kifupi, ni wazi kuwa mjumbe huyu hana rekodi zozote katika sekta ya  taasisi zisizokuwa za kiserikali.

    2. Ndugu Paul Kimiti- Huyu ni mwanasiasa mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na waziri mstaafu wa serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,
rekodi yake kwenye sekta hii inatia shaka.

     3. Ndugu Sixtus Raphael Mapunda- Huyu ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana  Chama cha Mapinduzi (UVCCM), huyu ni kiongozi wa chama cha siasa hivyo hakupaswa kabisa kuteuliwa kwenye kundi hili.

    4. Ndugu Elizabeth Maro Minde- Huyu ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi hivyo uwepo wake kwenye kundi la taasisi zisizokuwa za kiserikali unatia shaka.

    5. Ndugu Fortunate Moses Kabeja-Huyu taarifa zake hazijulikani kabisa kwenye sekta husika na hata tulipotumia mtandao wa google kutafuta habari zake hazijulikani popote duniani.
Pili, katika kundi la watu wenye malengo yanayofanana (20), Katika kundi hili, JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tuliongea na kutoa maoni kuwa kundi hili litatoa  mwanya kupatikana wajumbe ambao itakuwa vigumu kubaini uteuzi wao  umezingatia vigezo gani. Sheria kutosema malengo yanayofanana ni yapi hili  lilikuwa tatizo ambalo tumeendelea kulipigia kelele wakati wote. Upungufu huu  umeonekana kwa wajumbe sita (6) kwenye uteuzi wa wajumbe kwenye kundi hili
ambapo baadhi ya uteuzi unatia shaka.

1. Ndugu Paulo Christian Makonda- Huyu ni katibu wa Uhamasishaji
chipukizi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)

2. Ndugu Julius Mtatiro- Huyu ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha
Wananchi (CUF)

3. Ndugu Jesca Msambatavangu – Huyu ni mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa

4. Ndugu Abdallah Majura Bulembo- Huyu ni mwenyekiti wa Jumuiya ya
wazazi taifa Chama cha mapinduzi (CCM) na mjumbe wa kamati kuu

5. Ndugu Dr. Zainab Amir Gama- Huyu ni mbunge mstaafu wa Chama cha
mapinduzi (CCM)

6. Ndugu Hassan Mohamed Wakasuvi- Huyu ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora. Kwa kifupi, uteuzi huu umeendeleza dhana ya kwamba mchakato huu hasa bunge
maalumu la katiba litakuwa limeshamili wajumbe ambao ni wanasiasa kuliko  makundi mengine. Na pia ni vigumu kuelewa wajumbe hawa wana malengo gani  yanayofanana hadi kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa wajumbe wa bunge  maalum la katiba. Majina ya wajumbe toka Zanzibar katika makundi yote mawili tuliyoyafanyia
uchambuzi tunaendelea kutafuta taarifa zake na tutazitoa pindi zoezi ya uchambuzi  litakapokamilika.
               3. MUUNDO WA BUNGE MAALUM LA KATIBA
Kulingana na sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sheria hii inatamka aina tatu za
Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:-
(i) Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(iii) Wajumbe 201 kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko
ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.
Makundi hayo ni kama ifuatavyo;
4
a. Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)
b. Taasisi za Kidini (20)
c. Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42)
d. Taasisi za Elimu (20)
e. Watu wenye Ulemavu (20);
f. Vyama vya Wafanyakazi (19);
g. Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);
h. Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);
i. Vyama vya Wakulima (20); na
j. Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).
Ingawa sheria hii iliwapatia wabunge wote wa bunge la Jamhuri ya Muungano na
wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuingia kwenye bunge maalum la katiba
halikuwa wazo baya sana, ila JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tulipendekeza na
tunaendelea kusisitiza kuwa ilipaswa wajumbe hawa wachaguliwe na wananchi upya
au wawe theluthi moja (1/3) ya idadi ya wajumbe wote wa bunge maalum la katiba.
Na makundi yaliyoainishwa kwenye sheria ya mabadiiliko ya katiba Kifungu 22 (1c)
walipaswa kuwa theluthi (2/3) ya idadi ya wajumbe wote wa bunge maalum la katiba.
Kitendo cha waheshimiwa wabunge na Wawakilishi kuingia kwa idadi yao (438) dhidi
ya wajumbe wasio wabunge wala wawakilishi (201) hakina uwiano na hii ndiyo
sababu kuu tunaamini kabisa majadiliano kwenye bunge maalum la katiba
yatatawaliwa na maslahi ya kivyama na kisiasa.
Pia hata katika hawa wajumbe wengine (201) bado vyama vya siasa vimepewa
wajumbe (42) katika (201) na bado hata kwenye makundi mengine tumeona namna
Mheshimiwa Rais alivyoteua wajumbe ambao bila kificho wanaingia kwenye kundi la
wanasiasa. JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tunaendelea kusisitiza kuwa bunge
maalum la katiba litatawaliwa na maslahi ya kisiasa hasa kwa kuzingatia
Mheshimiwa Rais hivi karibuni amekutatana na vyama vya siasa ili kupata msimamo
wa vyama kuelekea bunge maalum la katiba. Hii inatia shaka na kuzidi kutoa picha
kuwa wajumbe waliowengi watajinasibisha kwenye bunge maalum la katiba kwa
kufuatana na itikadi zao za vyama.
4. MAPENDEKEZO YALIYOPITA
Kama tuliyosema hapo awali wakati wa hatua mbalimbali kwenye mchakato huu wa
kuandika katiba, JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tumekuwa tukitoa mapendekezo
na kuendelea kusisitiza masuala muhimu ambayo yalipaswa ama yanapaswa
kuendelea kufuatwa katika kukamilisha mchakato wa kuandika katiba mpya.
A) Tulipendekeza toka awali kuwa Mheshimiwa Rais asiteue wajumbe wa Tume
ya mabadiliko ya katiba Tanzania pendekezo ambalo lilipuuzwa na kutupwa
kapuni. Bado ni imani yetu kuwa pendekezo hili lilipaswa kufuatwa na
kutekelezwa ili kukuza demokrasia shirikishi katika kuandika katiba mpya
5
kwani katiba sio ya chama, mtu wala taasisi yoyote, katiba ni ya wananchi
wote.
B) Tulipendekeza pia haikuwa demokrasia sheria kumpatia Mheshimiwa Rais
mamlaka ya kuteua wajumbe (201) kwenye bunge maalum la katiba kwa
kuwa katika kuwateua wajumbe hawa atakuwa amekandamiza uhuru wa
wananchi walio wengi ambao kama wangelipewa nafasi ya kuchangua
wawakilishi wao labda ingelikuwa tofauti na alivyoteua Rais. Tunaendelea
kusisitiza kuwa haikuwa sawa kwa Mheshimiwa Rais kuteua wajumbe hawa,
Rais aendelee kuteua viongozi watakaomsaidia kutekeleza majukumu yake
na sio kuteua wabunge wa bunge maalum la katiba kama ilivyofanyika hivi
karibuni.
C) Tulipendekeza kuwa haikuwa sahihi kutumia kamati za maendeleo ya kata
(WDC) wakati upatikanaji wa mabaraza ya katiba ya wilaya ili kujadili Rasimu
ya kwanza ya katiba kwa kamati hizi zinaongozwa na madiwani ambao wengi
ni wa chama kimoja ya CCM ambao waliendesha mijadala kwa misingi ya
vyama vyao. Kwenye mabaraza haya, viongozi wa siasa walitumika sana
kuhakikisha mawazo ya vyama vyao yanapenya na kuingia kwenye Rasimu
kwa kuandaa wachangiaji ambao tayari walikuwa wameshapewa maneno ya
kuongea au kuchangia wakati wa mikutano.
D) Tulipendekeza uwepo waTume ya mabadiliko ya katiba wakati wa majadiliano
kwenye bunge maalum la katiba, pendekezo hili lilitupwa. Hivyo basi, Tume
ya mabadiliko ya katiba imefutwa kabla ya kumaliza jukumu lake la msingi,
tunazidi kusisitiza kuwa kitendo cha kuifuta Tume ni kinyume na utaratibu wa
kuandika katiba na kutokuwepo kwa Tume hii kunatia shaka kwamba
inawezekana baadhi ya watu, vikundi au vyama vya siasa wakatumia fursa hii
kubadilisha maudhui yote au kwa sehemu kubwa ndani ya Rasimu na kuleta
mambo mapya yenye tija kwa watu au kikundi cha watu wachache.

               5. MAPENDEKEZO YA SASA
A. Bunge la Maalum la katiba liwe huru na lionyeshwe moja kwa
moja
Bunge Maalum la Katiba litaanza vikao vyake mnamo Jumanne tarehe 18/02/2014
mjini Dodoma kwa takribani siku 70 hadi 90. Wajumbe wa bunge hili tayari
wameshajulikana, hivyo tunawataka katika kujadili Rasimu ya katiba ili kupata katiba
inayopendekezwa majadiliano ni muhimu yakajengeka kwenye misingi ya uhuru wa
kutoa maoni na kuchangia hoja. Pasiwepo na vitisho vya aina yoyote ile wakati wa
majadilianao na bunge hili ni vyema likaonyeshwa moja kwa moja na vyombo vya
habari vyote nchini ili wananchi wapate kusikia na kuona mwenendo wake ili wakati
6
wa kura ya maoni waweze kufanya maamuzi ambayo watakuwa wanafahamu kwa
nini wameamua kuchukua maamuzi hayo.
Kwa upande mwingine wajumbe hawa ni sharti waepukane na malumbano ya
namna yoyote ambayo hayana maslahi kwa taifa, waweke kando ushabiki wa
kivyama, udini, ukanda na namna yoyote ile ya ushabiki usiokuwa na tija kwa taifa
letu ili waweze kujadili rasimu ya katiba kwa maendeleo ya taifa kwa miaka mingi
ijayo kama alivyowasihi Rais wa Jamhuri Mheshindiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
B. Hoja kuu kwenye bunge maalumu la katiba iwe rasimu ya pili ya
katiba
Kumekuwepo na kauli tofauti kuhusu maudhui yaliyomo kwenye rasimu ya pili ya
katiba. Kwa mfano kauli aliyoitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwamba bunge maalum la katiba linayo mamlaka ya kubadilisha rasimu kwa namna
yoyote ile wakati wa vikao vyake. Kauli hii inatia shaka kwa kuwa kama bunge
maalum la katiba likifanya mabadiliko makubwa ya kimaudhui inamaanisha kazi
kubwa na nzuri iliyofanywa na Tume ya mabadiliko ya katiba itakuwa haina maana
tena na itakuwa imetumia fedha za umma bila faida yoyote. Hivyo, tunapendekeza
kuwa hoja kuu kwenye bunge maalum la katiba iwe ni kujadili rasimu na sio kufanya
marekebisho kwenye rasimu na kama marekebisho yanafanyika yasiondoe maudhui
ya kifungu husika. Na endapo kutakuwa na hoja inayokosa muafaka basi kifungu
hicho kiachwe kama kilivyo kwenye rasimu.
C. Kuimarisha uendeshaji wa kura ya maoni kwa kuwa na Tume huru ya
uchaguzi na kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura
JUKWAA LA KATIBA TANZANIA linaona kwamba ili kuimarisha demokrasia katika
upigaji kura ya maoni unatarajiwa kufanyika mara baada ya bunge maalum la katiba
basi ni muhimu kuimarisha uendeshaji wa kura hiyo kwa kuwa na Tume huru ya
uchaguzi na kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura na kuandikisha wapiga
kura wapya. Kwa kuwa Zanzibar wameshaboresha daftari na kuandikisha wapiga
kura wapya, kwa upande wa Tanzania bara bado hawajaanza kufanya lolote ingawa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza nia ya kuboresha daftari la kudumu la
wapiga kura. Hivyo, tunapendekeza zoezi hili lifanyike mara moja ili wananchi
waweze kutimiza haki yao ya kidemokrasia ya kupiga kura.
D. Elimu ya uraia
JUKWAA LA KATIBA TANZANIA linasisitiza kwamba elimu ya uraia ni muhimu kwa
ajili ya wananchi kupata uelewa juu ya katiba wanayotaka kuipigia kura ili waweze
kupiga kura wakiwa wanajua wanapigia kura kitu gani (informed consent). Kifungu
cha 38(2) kinasema...... Tume italazimika, na vyama vya siasa na vyama vya kijamii
vinaweza kutoa elimu ya uraia na uhamasishaji juu ya Katiba inayopendekezwa kwa
muda usiozidi siku thelathini kuanzia siku ya kuchapishwa katika Gazeti la Serikali.
7
Muda wa kutoa elimu ya uraia kwa siku thelathini hautoshi hata kidogo,
tunapendekeza uongezwe na kuwa miezi mitatu.
E. Matokeo Ya Kura Ya Maoni
Katika kifungu cha 41(5) cha sheria ya Kura ya Maoni ya Mwaka 2013 kinaeleza
kwamba “Pale ambapo wingi wa kura halali zilizopigwa kwenye kura ya maoni
zitakuwa ni “HAPANA” Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
1977, itaendelea kutumika”. Dhana hii kwamba nchi inaweza kuendelea kutumia
katiba 1977 baada ya mchakato mrefu na wa gharama kubwa, na kuwapa ufahamu
wananchi juu ya upungufu mkubwa wa katiba hii, haifai na ni hatari. Aidha JUKWAA
LA KATIBA TANZANIA linapendekeza kwamba ni muhimu kutambua maeneo
yaliyosababisha katiba inayopendekezwa kupigiwa kura ya hapana na kuyaweka
wazi ili wananchi wayajadili na kufikia muafaka kabla ya marudio ya kupiga kura
mara ya pili.
JUKWAA LA KATIBA TANZANIA pia linapendekeza kuwa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ifanyiwe marekebisho makubwa katika
maeneo yote yaliyoainishwa kuwa na kasoro wakati wa mchakato wa katiba mpya
na kama yamepatiwa muafaka yaingizwe kama utaratibu wa mpito wa kukamilisha
utengenezaji wa katiba mpya.
Kwa sababu ya kuharakisha katiba hii hasa kuhusu suala zima la uchaguzi wa
mwaka 2014/2015. Sheria za uchaguzi zifanyiwe marekebisho na uchaguzi wa
mwaka 2015 ufanyike na viongozi watakaoingia madarakani ndio waendelee
kusimamia mchakato wa kuandika katiba mapya kuliko hii kasi tunayoenda nayo
ambapo bado kuna mambo mengi yenye kukinzana na maswali yasiyo na majibu
kuhusiana na mchakato huu na katiba ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
na Katiba ya Zanzibar.
6. HITIMISHO
Tunahitimisha kwa kusema kuwa tangu mchakato wa kaundika katiba mpya
ulipoanza mambo mengi yameshafanyika ikiwa ni pamoja na kutunga sheria ya
mabadiliko ya katiba, kuunda Tume ya Mabadiliko ya katiba, kukusanya maoni kwa
watu binafsi, mashirika na kutoa rasimu ya katiba, kuendeshwa kwa mabaraza ya
katiba kwa ajili ya kuipitia rasimu ya katiba na kutoa maoni kwa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba, Tume Kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba, Rais kuteua wajumbe 201 wa
bunge la katiba na sasa tunasubiria bunge maalum kuanza vikao. Hata hivyo ili
mchakato huu wa kuandika Katiba mpya uweze kukamilika kwa ufasaha na kutoa
katiba yenye maslahi kwa wananchi walio wengi, ni muhimu:
 Bunge maalum la Katiba liendeshwe kwa uhuru na lionyeshwe moja kwa
moja kwa wananchi
 Tuwe na Tume huru ya uchaguzi
8
 Daftari la wapiga kura liboreshwe kabla ya kura ya maoni kufanyika
 Tume ya mabadiliko ya katiba ni vyema ikarudishwa ili iweze kutoa
ufafanuzi wakati wa majadiliano ya bunge maalum la katiba ili kuepusha
uchakachuaji wa maudhui ndani ya rasimu ya katiba
 Majadiliano yalenge masilahi ya taifa na sio masilahi mengine yoyote
Pamoja tujenge taifa,
Imetolewa na;
Deus Kibamba
Mwenyekiti

No comments: