Tuesday, February 11, 2014

EXCLUSIVE----PICHA ZA YULE JAMBAZI WA TARIME NA NAMNA ALIVYOFARIKI BAADA YA KUKIRI KUUA WATU TISA..

http://www.thebesttz.blogspot.com/Mtuhumiwa wa mauaji ya watu tisa na unyang'anyi wilayani Tarime mkoani Mara, aliyekuwa akihojiwa   Polisi kwa tuhuma zilizokuwa zikimkabili, amefariki katika Hospitali ya Wilaya  wakati akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa pumu.http://www.thebesttz.blogspot.com/
Kamanda wa Polisi Tarime na Rorya, Kamishina Msaidizi Justus Kamugisha, alisema kuwa mtuhumiwa huyo jina lake halisi ni Charles Kichune (38) na alifariki usiku wa kuamkia jana wakati akitibiwa ugonjwa huo hospitalini.
ENDELEA HAPA-----------
Majina mengine aliyokuwa akiyatumia kwa mujibu wa Kamanda Kamugisha ni pamoja na Josephat Chacha na Charles Msongo.
"Mwili wa marehemu upo chumba cha maiti katika Hospitali ya Wilaya ukisubiri kufanyiwa uchunguzi na kuchukuliwa na ndugu zake," alisema Kamanda Kamugisha.
 
http://www.thebesttz.blogspot.com/
Baadhi ya raia waliouawa  ni pamoja na  David Yomami, Samuel Matiko, Robert Machumbe, Zakaria Marwa , Juma Nyaitara, Juma Mwita, Marwa Mwita na Erick Makanya.
Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda Kamugisha, Kichune baada ya kukamatwa alikiri Polisi kuhusika katika mauaji ya watu mbalimbali katika kata za Binagi, Turwa na Kitare katika vijiji vya Mogabiri, Kenyamanyori, Nkende na Rebu.
Kamanda Kamugisha alisema  mtuhumiwa huyo Kichune alikamatwa Februari 6 mwaka huu mkoani Tanga baada ya Polisi  kufuatilia mtandao wake baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
Baada ya kukamatwa, uchunguzi wa Polisi ulibaini kuwa  baada ya mauaji ya watu tisa, mtuhumiwa alikodisha pikipiki kutoka kijiji cha Kenyamanyori alikokuwa akiishi, hadi Musoma.
Alipofika Musoma, inadaiwa alihifadhi bunduki aina ya SMG na risasi kadhaa kwa mshirika wake, Marwa
Keryoba maeneo ya Bweri na alipokamatwa alimtaja  Keryoba kuwa ndiye anayetunza silaha hiyo.
Februari 7 mwaka huu, Polisi walifuatilia silaha hiyo kwa Marwa na kumkuta mtuhumiwa, ambapo alitakiwa kujisalimisha lakini alikaidi  na kuanza kurushia risasi  askari.
"Marwa aliuawa Februari 7 alfajiri Bweri Musoma, wakati alipotakiwa kujisalimisha na kukaidi na kuanza kurushiana risasi na askari," alisema Kamanda Kamugisha.
Kwa mujibu wa Kamanda Kamugisha, kuna mtuhumiwa mwingine sugu wa mauaji ya watu zaidi ya 10, Senso Magabe ameuawa katika majibishano na Polisi wiki iliyopita.
Hata hivyo katika majibishano hayo, wenzake watatu walifanikiwa kutoroka na msako unaendelea wilayani hapa ambapo wananchi wameombwa kutoa ushirikiano Polisi ili  kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao.
Kamanda Kamugisha alisema tayari watu wanne waliokuwa katika mtandao huo wa ujambazi wamefikishwa mahakamani kwa mashitaka ya unyang'anyi na mauaji.
Watuhumiwa waliofikishwa mahakamani ni pamoja na Kyoma Manguh, Marwa Mwita , Yohana Mgosi na Chacha  
Bugichere ambapo kesi zao zitatajwa Februari 19 mwaka huu.
Jana mamia ya wananchi wilayani Tarime walifurika kuona mwili wa Kichune maarufu Kenonke ambaye amekuwa tishio kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Polisi imetangaza zawadi ya Sh milioni moja  kwa
atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kukamata silaha za moto katika wilaya za Tarime na Rorya.
CHANZO MAASINDA BLOG

No comments: