.

RIPOT MAALUM ---------HALI YA KISIASA TANZANIA SIO SHWARI,CHADEMA YAONYESHA PICHA ZA MAKADA WAO WALIOKATWA MAPANGA NA VIJANA WA CCM,WAMTUPIA LAWAMA RAISI KIKWETE ,WASEMA YEYE NDIO ANAWATUMA,KAULI YAKE YA KUWATUMA CCM WAKAPAMBANE SASA YAWA GUMZO MJINI APEWA SIKU TATU AOMBE RADHI


HUYU ALIKATWA MAPANGA

MKURUGENZI WA OGANAIZESHENI NA MAAFUNZO WA CHADEMA AKIONYESHA BAADHI YA PICHA ZA KADA WAKE AMBAYE ALIKATWA NA MSUMENO WA MBAO SHINGONI NA WATU WANAODAIWA KUWA WA CCM KATIKA MOJA YA CHAGUZI ZAKE HAPA NCHININa Karoli vinsent
         
        CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Nchini (CHADEMA) kimebaini kuwa serikali ya Tanzania kupitia viongozi wake wa juu  Rais Jakaya Kikwete  ndiye anayetuma Jeshi la Polisi pamoja na  makada wa Chama cha mapinduzi CCM kuteka makada wa chama Chadema.

        Pia,Chadema wamebaini pia ulipuaji wa Bomu uliofanyika katika mkutano wa chama hicho katika uwanja wa Soweto mkoani Arusha mwaka jana mpango huo, uliandaliwa na Rais Kikwete kwa lengo kuwalipua viongozi wajuu wa chama hicho.

           Hayo,yalisemwa leo na Mkurugenzi wa origanizesheni wa Chama cha Chadema Bensoni Sengo Kagaila wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari makao makuu ya Chama hicho Jijini Dar es Salaam.

     Ambapo ,alisema kutokana na Kauli aliyoisema Kikwete kuwahamulu Makada pamoja na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM kulipiza kisasi na kuacha unyonge ni dalili za kiongozi huyo kuhusika katika vitendo vya utekaji na utesaji wanavyofanyiwa wanachama wa chadema.
 ENDELEA HAPA----------PICHA NYINGINE ZITAKUJIA BAADAE


    “Chadema tumebaini kuwa Vitendo wanavyofanyiwa wanachama wetu na pia viongozi wetu na vilevile ulipuaji wa mkutano wa chama chetu mkoani Arusha  Rais Kikwete anahusika ushahidi huko wazi kutokana na Kauli yake”

    “Kauli hii anayosema Rais Kikwete ya wanachama wa chama cha Mapinduzi kuacha uvumilivu  ni kauli ya kuleta Vita ndani ya nchi,kwani Rais huyo ameshindwa kutumia hata Jeshi kutuliza fuju adi kuamulu wanachama wa chama hicho,huyo ni kiongozi kweli maana anaongea kama mtu wa Manzese”

     “kiukweli tutakufa nae maana Kauli yake itapelekea nchi kwenda kumwaga damu,maana Rais huyu ndiye anayetangaza amani harafu Rais huyuhuyu ndiye anayeleta Vita”alisema Kagaila

     Bensoni,ambaye pia ni Msimamazi wa Uchaguzi wa Kanda mbalimbali za Chadema alisema Hata kauli aliyoitoa wazili mkuu bungeni  Dodoma kuhusu kupiga kwa watu watakao kaidi amri ya Jeshi la Polisi inaonekana wazi ajaitoa yeye bali alitumwa na Rais Kikwete.

     “Hata Kauli aliyoitoa Waziri mkuu bungeni kuwaruhusu Jeshi la polisi kupiga tu inaonekana Rais kikwete ndiye aliemtuma.hivi  Huyu ni Kiomgozi gani huyu?je Kama ameshindwa kuongoza atuachie nchi yetu,Leo anavyotangaza Vita ndani ya nchi tafsiri yake ni nini”

     “Chadema tunasema hatutokubali amani ipotee kwa sababu ya Rais kikwete tutakwenda mbali,yeye utulivu na amani ameichoka mpaka anataka Vita basi aondoke mzee huyo” Alihoji Kagaila

     Aida,chadema Wamempa siku tatu Rais Kikwete kufuta Kauli yake lasivyo Chadema kitachukua Maamuzi Magumu.

      kumbukweTamko hili la Chadema  limetokana na kauli ya Rais kikwete, wakati Akifungua mkutano wa NEC ya CCM mwishoni mwa wiki mjini Dodoma, Rais Kikwete aliwataka wanachama wa chama hicho kuacha unyonge kwani uvumilivu waliokuwa nao umefika kikomo chake.

      Alisema chama hicho kinaingia kwenye uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kalenga mkoani Iringa, kinashindana na vyama vingine ambavyo alisema ni wagomvi, maana kwao ugomvi ndiyo sehemu ya mwongozo wa kufanya kazi ya siasa.

     “Tulizungumza nalo hilo kwenye Kamati Kuu, tulikubaliana kuacha unyonge. Ndiyo, kwenye Kamati Kuu tumekubaliana, tumesema jamani watu wote waende wakaseme tumekubaliana kuacha unyonge,” alisema huku akicheka na kupigiwa makofi na wajumbe wa NEC.

        Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, alitolea mfano wa tukio lilitokea Kahama mkoani Shinyanga, ambapo kijana mmoja alitolewa macho kwa bisibisi, na tukio la Igunga ambapo kijana mmoja alimwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.

      “Acheni unyonge na hata katika taarifa ya habari leo (jana) mtoe hivyo hivyo. Na muache habari zote mseme hii tu (waandishi wa habari). Uvumilivu una ukomo wake,” alisema huku wajumbe wakiendelea kumpigia makofi.

       “Nalisema kwa sababu yanayotokea yanasikitisha sana. Pale Igunga kijana yule wamemmwagia tindikali, pale Kahama kijana ametolewa macho kwa bisibisi,” alisema.

      Uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga lililopo mkoani Iringa unatarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu, huku tayari vyama vya CCM na CHADEMA vikiwa vimetaja wagombea wao.

      Katika hatua nyingine kituo hicho cha kuwasemea wananchi kimezengumzia uchaguzi mdogo wa madiwani kata 27 na kusema uchaguzi huo ulikuwa na kasoro nyingi sana ikiwemo idadi ndogo ya wapiga kura pamoja vitendo vya utekaji pamoja na utesaji walivyokuwa wanafanyiwa wagombe na wapiga kura.

        Ndipo Kauli hiyo ikakifanya Kituo Cha taarifa kwa Wananchi (TCIB)kimeanza mawasiliano na Mwendesha Mastaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya uharifu dhidi ya Binadamu(ICC) Bi Fatou Bensouda kumwomba atume timu ya wataalamu wake kuja Tanzania kufanyia  Uchunguzi na Tathmini kuhsu kauli hizo iliwaweze kuifungulia mashtaka Serikali ya Tanzania.        Vilevile Chadema,ambacho ni Chama Kikuu cha upinzani Nchini kimemtakaMsajili wa vyama vya Kisaisa Nchini Pamoja na Tume ya Uchaguzi nchi kwenda Kwenye makambi ya Greengurd ambayo inasemekana ni Makambi yanayomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM kwani yanatoa mafunzo ya kijambazi.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.