.

KOVA ATOA NENO LEO,NI KATIKA SEMINA YA VIONGOZI MBALIMBALI WA DAR ES SALAAM,SOMA ALICHOKISEMA,MBWA MWITU SASA BASI

         Kamishna wa polisi kanda maalum ya  dar es es salaam suleman kova amesema kuwa ni jukumu la viongozi wote wa dare s salaam kuhakikiksha kuwa jiji hilo linakuwa huru na salama ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa amani ya uhakika.
       
        Kamishna kova ameyasema hayo eo katika senmina iliyoandaliwa na manispaa ya ilala kwa viongozi wote wa ngazi za chini kuanzia ngazi za vitongoji yenye lengo la kuboresha maswala ya usalama jijini dare s salaam.
      
          Kova amesema kuwa ni lazima ifike mahala jiji la dare s salaam liwe na amani na uhuru ili ifike mahala dare s salaam iwe mfano wa kuigwa na majiji mengine tanznia na nje ya Tanzania.
      
        Anasema kwa kilamtaa lazima uwe huru na mbinu pekee ya kuwa huru nikushirikiana na viongozi wa mtaa na wa ngazi za chini.
Akizungumzia swala la vijana wahalifu wanaojiita MBWA MWITU kamishna kova amesema kuwa tayari ametoa agizo kwa viongozi wa mitaa hiyo kuhakikisha vijana hao wanakamatwa mara moja na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
      
        Katika semina hiyo ya viongozi mbalimbali wa mtaa mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya ilala mh RAYMOND MUSHI ambapo pamoja na mambo mengine amewataka watanzania kushirikiana kwa pamoja katika kuwafichua wahalifu kwani wananchi ndio walionao karibu zaidi

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.