Friday, February 14, 2014

KWA WALE MNAOTAKA KURUDIA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA HUU,HILI HAPA TANGAZO LENU TOKA BARAZA LA MITIHANI TANZANIA,SOMA KWA MAKINI



                                                         TANGAZO
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

                Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwakumbusha watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT)  mwezi Novemba,  2014  kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kilichoanza rasmi tarehe 1 Januari, 2014 kwa ada ya Shilingi 50,000/=kwa wanaojisajili CSEE na Shilingi 30,000/= kwa wanaojisajili QT  kitaishia tarehe 28 Februari, 2014.

         Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa bure na kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au Mpesa.
                                                     Imetolewa na:

KAIMU KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA.

No comments: