.

SAKATA LA MBUNGE WA BAHI KUFANYA UFISADI,NAPE AZUNGUMZA NA MTANDAO HUU,SOMA ALICHOKISEMA HAPA.


Na Karoli Vinsent.


        IKIWA imepita siku moja kupita Baada ya Kamati ya Uchunguzi iliyoundwa na Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, kumtia hatiani Mbunge wa Bahi, Omar Badwel (CCM), akidaiwa kutumia vibaya fedha za Mfuko wa Jimbo.

      Chama cha Mpinduzi CCM,kimesema kinasubili ripoti ya Baraza la Madiwani wa halmashauli hiyo ili kiweze kumchukulia hatua Mbunge huyo.

       Hayo,aliyasema leo na Katibu wa Itikadi na ueneze wa Chama cha Mapinduzi CCM Nape Nnauya,wakati wa Mahojiana kati ya mwandishi wa Mtandao huu na kiongozi huyo,ambapo Nape alisema kwa sasa bado hajapata taharifa nzima inayomuhusu Mbunge huyo zaidi ya kusika kwenye Vyombo vya Habari.
ENDELEA HAPA------------


       “Mimi taarifa hiyo nimeiona kwenye Vyombo vya habari ila sisi kama chama tunasubili ripoti nzima ya Baraza la Madiwani na tujilizishe juu ya Tuhuma zinazomkabili na ili tuweze kumchukulia hatua,sisi kama chama”alisema Nape

      Mbunge huyo ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa katika halmashauri moja mkoani Pwani, anadaiwa kutumia fedha za mfuko huo kinyume na malengo, huku pia taratibu za manunuzi zikiwa zimekiukwa.

         Mwandishi wa Mtandao huu alipotaka kujua ni hatua Gani chama kitamchukulia mbunge huyo,Nape alisema kwa sasa hawezi kusema ni hatua gani chama hicho kitamchukulia mpaka watakapopata taarifa nzima juu ya tuhumu zinazomkabili mbunge huyo.

      Ikumbukwe Hoja binafsi ya kuundwa kwa kamati hiyo ilitolewa mwishoni mwa mwaka jana na Diwani wa Kata ya Lamaiti, Donald Mejitii (CCM), akitaka matumizi ya fedha hizo za Mfuko wa Jimbo la Bahi yachunguzwe.

       Baada ya kamati hiyo kuundwa na kufanya kazi, juzi ilirejesha taarifa yake ikibainisha kuwa fedha hizo zimetumika vibaya tofauti na lengo la mfuko.

       Mejitii katika hoja yake alidai kuwa Badwel alitumia vibaya fedha za mfuko huo ambazo zilitolewa kwa vikundi, ununuzi na usambazaji wa majembe ya kukokotwa na ng’ombe kwa kipindi cha Agosti mwaka jana.
Akisoma taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Kamati, Julius Chitojo, ambaye ni Diwani wa Kata ya Zanka, alisema kuwa walibaini kwamba wananchi walidanganywa kwa kuuziwa majembe hayo wakielezwa ni chapa Zimbabwe wakati ni chapa ya Jogoo.

       Kamati pia ilibaini kuwa majembe hayo yaliuzwa kwa bei ya juu kuliko ilivyokubaliwa na Kamati ya Mfuko wa Jimbo.
“Pia tumebaini kuwa makusanyo ya fedha kutokana na mauzo ya majembe hayo hayajarudi halmashauri ili wananchi wengine waweze kunufaika na mfuko huu wa jimbo.

       “Badala yake fedha hizi zimechukuliwa na Said Kayumbo kwa maelekezo kuwa anampelekea mbunge Badwel,” alisema Chitojo.
Hata hivyo, aliongeza kuwa baadhi ya wananchi wamepata mgawo wa majembe ya bure wakati wengine wameuziwa, na pia fedha za vikundi ziliingizwa katika akaunti ya Jumuiya ya Akiba na Maendeleo Bahi (Basada) kinyume cha utaratibu.

        Kwamba, hadi kufikia Oktoba 30 mwaka jana, fedha za vikundi tisa zilikuwa bado hazijawafikia walengwa.
“Fedha za mchango wa kusafisha kisima cha maji katika Kijiji cha Chibelela zilichukuliwa na mbunge Januari na Februari 2013 na hazikuwa zimerejeshwa mpaka kufikia Oktoba 30 wakati baraza lilipounda kamati ya uhakiki.

       “Aidha, mbunge aliendelea kukaa na fedha hizo huku akijua wazi kuwa halmashauri imekwishalipa fedha zote,” alisema Chitojo.
Katika mradi wa maji Chibelela, alisema zaidi ya sh milioni 1.7 zilikusanywa kwa wananchi na alikabidhiwa mbunge.

       Alisema kuwa halmashauri ilitoa fedha zote sh milioni nne ambazo zilikuwa gharama za mradi huo na ziliingizwa katika akaunti ya Kijiji cha
Chibelela namba 50502300434.

     Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa wananchi walidanganywa kwa kupewa risiti za ada ya kujiunga na Basada badala ya zile za ununuzi wa majembe na kudai kuwa hiyo inaashiria kuwaibia.

    “Mbunge ndiye aliyewapa kazi Basada ya kukusanya fedha za majembe na alikuwa akiongozana nao kwenye mikutano mbalimbali ya kukabidhi majembe.

      “Wananchi waliuziwa majembe kwa nusu bei ya sokoni yaani sh 110,000 kwa jembe wakati huo, kumbe yalinunuliwa na halmashauri kwa sh 170,000 hivyo walipaswa kutoa sh 85,000 na sio 110,000,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa kamati hiyo ilibaini kuwa majembe yaliyosambazwa ni 85 yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 14.4 kati ya 78 yaliyouzwa kwa sh 110,000 ambapo ni sawa na sh milioni 8.5.

        “Kutokana na uhakiki huu, kamati imebaini ya kuwa ni kweli matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo hayapo sawa sawa. Kamati hii inatoa maoni kuwa baraza lichukue hatua stahiki dhidi ya mbunge pamoja na kurejesha fedha sh 2,750,000 alizozipokea msaidizi wake.
“Pia arejeshe sh 1,950,000 ambazo ni ziada ya bei iliyokubaliwa, sh 5,440,000 za majembe 32 hayajawafikia walengwa na milioni 4.3 hazijapelekwa kwa vikundi,” alisema mwenyekiti huyo.

        Kamati hiyo iliitaka Basada kurejesha fedha za halmashauri ambazo walikusanya na kuzitumia kiasi cha sh 4,180,000 pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria kwa kutoa risiti ambazo sio za ununuzi wa majembe. Vile vile fedha za Mfuko wa Jimbo zitolewe kama ruzuku na sio mkopo.
Ripoti hiyo ina viambatanisho mbalimbali ambavyo vinadhihirisha fedha hizo kupokelewa na mbunge pamoja na msaidizi wake Kayumbo zikiwa zimesainiwa na kuandikwa kwa mkono.

        Katika utetezi wake, Badwel alisema kuwa inawezekana kuwa kuna tatizo katika mfuko huo na kudai kuwa yaliyopo katika ripoti hiyo mengine ni ya kweli, lakini mengine sio ya kweli.
“Katika ripoti hii sijaona sehemu ambayo mimi nilitoa majembe ambapo katika mzunguko huu na mimi nilipeleka majembe 58 kwa ajili ya wananchi wangu.

      “Nadhani mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni… mbona nimetoa orodha ya vijiji ambavyo nimetoa majembe yaliyotolewa kwa Mfuko wa Jimbo na mengine ambayo sio ya mfuko?” alihoji.
Alisema kuwa lazima atendewe haki kwani yeye hakushinikiza aina ya majembe na kudai kuwa huu ni mwaka wa tatu majembe ya Mfuko wa Jimbo yanatolewa kwa sh laki moja.

   “Sasa mimi nitasema nini, kuna vikundi vitatu kweli hatujavipa fedha kwa sababu vilikuwa na milioni moja kila kimoja kutoka maendeleo ya jamii.

       “Hii taarifa haijanitendea haki, imejaa siasa, imenidhalilisha ili nijiuzulu, lakini leo nasema hajiuzulu mtu na hii haijafanywa leo, imeanza tangu nikiwa mwenyekiti wa halmashauri na nilijiuzulu,” alisema.


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.